RAIS William Ruto amegeuza ziara yake ya siku 10 katika eneo la North Rift kuwa jukwaa la kushambulia wapinzani wake kisiasa huku akiwataka kueleza mipango yao ya maendeleo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027.
Akiwa katika kaunti za Nandi, Uasin Gishu, Elgeyo Marakwet na Baringo, Rais amekuwa akitetea rekodi ya serikali yake katika maendeleo huku akidai kuwa wapinzani hawana sera wala ajenda ya kuongoza nchi.
Pia amezindua kaulimbiu mpya ya kisiasa, “Usawa ni Sawa”, anayoitumia kueleza msimamo wake kuhusu usambazaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Akizungumza akiwa Kinyach, Baringo Kaskazini, Jumanne, Dkt Ruto alionya kuwa kuungana kwa wapinzani dhidi yake hakutawapa ushindi iwapo hawatakuwa na mipango madhubuti ya maendeleo.
“Wameanza kuungana kwa jina la umoja, lakini hata wakiungana bila kuwa na ajenda, hesabu ya kikabila haitawasaidia. Wanapaswa kuwa na mpango ambao Wakenya watajiona ndani yake,” alisema.
Alisema uchaguzi wa 2027 unapaswa kuamuliwa kwa sera na ahadi za maendeleo badala ya ukabila, chuki, wivu na ubaguzi.
Rais alidai kuwa serikali yake ina mpango wa kutekeleza miradi huku wapinzani wake wakikosa sera na manifesto wanayoweza kuwaeleza wananchi.
Kaulimbiu ya “Usawa ni Sawa” ilipigiwa debe katika mikutano ya Chama cha United Democratic Alliance (UDA) mjini Kapyego na Chebara, Kaunti ya Elgeyo Marakwet.
Dkt Ruto aliwaongoza wafuasi wake katika wimbo wa kuitikiana akisema: “Nikisema UDA, nyinyi mjibu ‘Usawa ni Sawa’. Nikisema ‘Usawa ni Sawa’, nyinyi mjibu ‘Mbele Pamoja’.”
Kaulimbiu hiyo inajiri huku Rais akitetea miradi yake ya barabara, umeme, nyumba za bei nafuu, elimu na afya, akisema uwekezaji huo unalenga kubadilisha maisha ya wananchi.
Pia alieleza wazi nia yake ya kuwania muhula wa pili, akiwataka wakazi wa North Rift kumpa kura kwa wingi.
“Nahitaji kura zaidi milioni moja katika eneo hili. Urais hupatikana kupitia kura na ninahitaji uungwaji mkono wenu ili nipate muhula mwingine wa kuwatumikia,” alisema.
Aliwataka vijana waliotimu umri wa miaka 18 kupata vitambulisho vya kitaifa na kujisajili kama wapigakura.
Rais pia alitetea mpango wa nyumba za bei nafuu dhidi ya wanaopinga ushuru wa nyumba, akisema mpango huo unazalisha ajira na kuwawezesha Wakenya kupata makazi bora.
Alidai mpango huo umeunda ajira milioni moja.
Katika kaunti ya Elgeyo Marakwet, alisema Sh15 bilioni zimetengwa kwa nyumba na miradi inayohusiana na mpango huo, ikiwemo zaidi ya nyumba 3,000 na mabweni wanafunzi.
Alisema Sh18 bilioni zimetengwa kwa kilomita 270 za barabara na Sh1.6 bilioni kuunganisha zaidi ya nyumba 10,000 na umeme.
Akiwa Baringo, alisema Sh22 bilioni zimetengwa kwa kilomita 350 za barabara, huku Sh2 bilioni zikilenga kuunganisha nyumba 25,000 na umeme.
Pia alitaja barabara ya Kipsaraman-Kinyach yenye urefu wa kilomita 55 na gharama ya Sh4.5 bilioni, akisema itarahisisha biashara na kuimarisha usalama katika Bonde la Kerio.
Katika sekta ya afya, Dkt Ruto alisema watu 365,000 wamejisajili katika Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) Elgeyo Marakwet, huku vituo vya afya vikipewa Sh1.2 bilioni.
Kitaifa, alidai zaidi ya watu 33 milioni wamejisajili katika SHA na vituo vya afya vimepokea zaidi ya Sh200 bilioni.
Ruto azindua kauli mbiu mpya, aponda upinzani

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…