GAVANA wa Siaya James Orengo amesema kuwa marehemu Raila Odinga alikuwa anajiandaa kuwania urais kwa mara ya mwisho katika uchaguzi mkuu wa 2027 kabla ya kifo chake mnamo Oktoba 15 mwaka jana.
Bw Orengo, ambaye alikuwa rafiki na mshirika wa kisiasa wa Raila kwa zaidi ya miaka 50, amesema mazungumzo yao hayakuwahi kuondoa uwezekano wa kinara huyo wa zamani wa ODM kuwania urais tena.
Katika mahojiano na Taifa Leo, Bw Orengo amesema kifo cha Raila kiliacha masuala mengi ya kisiasa bila kutatuliwa, huku akishutumu Serikali Jumuishi ya Rais William Ruto kwa kushindwa kutekeleza ajenda 10 walizokubaliana na marehemu.
Anasema Bw Odinga alikuwa bado na jukumu muhimu la kutekeleza katika kuongoza nchi na kusukuma mbele mageuzi ya kisiasa na kiuchumi.
“Nilishtuka na kukosa maneno. Kwa bahati mbaya, tulikuwa tumezoea kuamini kwamba Raila hangekufa,” akasema Bw Orengo kuhusu kifo cha rafiki yake.
Gavana huyo anakumbuka kwamba alifaa kukutana na marehemu Bw Odinga Siaya Oktoba 13 mwaka jana, siku chache kabla ya kifo chake. Raila alikuwa ametarajiwa kufunga mkutano wa uwekezaji na biashara wa kimataifa wa Siaya, lakini alimweleza Bw Orengo kwamba huenda asihudhurie.
Siku mbili baadaye, habari za kifo cha Raila zilipowafikia waandalizi muda mfupi kabla ya mkutano kuanza, waliamua kuahirisha shughuli hiyo.
Bw Orengo anasema Raila alistahili kupewa nafasi nyingine ya kuwania urais kwa sababu alikuwa bado na mchango wa kutoa kwa taifa.
“Katika mazungumzo yetu, hakuwahi kuondoa uwezekano wa kuwania urais tena,” akasema.
Pia amekosoa jinsi mwili wa Raila ulivyorudishwa nchini na mipango ya mazishi, akisema Wakenya na watu wengine barani Afrika walipaswa kupewa muda zaidi wa kumwomboleza kiongozi huyo.
Kuhusu ajenda 10, Bw Orengo anasema serikali haijaonyesha nia ya kutosha kutekeleza makubaliano hayo. Alitaja visa vya utekaji nyara, mauaji yanayodaiwa kutekelezwa kinyume cha sheria, kunyanyaswa kwa vyombo vya habari na matumizi makubwa ya fedha na serikali.
Anasema ajenda hizo zililenga pia kushughulikia ukosefu wa ajira kwa vijana, ufisadi na changamoto za utawala bora.
Bw Orengo amekosoa uongozi wa sasa wa ODM, akidai umeachana na misingi ya demokrasia, uzalendo na utawala wa kikatiba ambayo Raila alitetea. Alisema mabadiliko ya uongozi wa chama hicho yalipaswa kufuata katiba yake badala ya kuruhusu UDA na Rais Ruto kuingilia masuala yake ya ndani.
Gavana huyo pia amedai kuwa roho ya kisiasa ya Raila inaendelezwa zaidi na vuguvugu la Linda Mwananchi linalohusishwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino.
Amesisitiza kuwa eneo la Nyanza linapaswa kutanguliza demokrasia ya kikatiba na ugatuzi badala ya kutegemea ahadi za miradi ya maendeleo kutoka kwa serikali ya kitaifa.
Orengo: ‘Tinga’ alikuwa na nia ya kuwania urais 2027

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…