WAMILIKI wa matatu wameonya kuwa huenda nauli ikapanda kufuatia ongezeko la bei ya mafuta, wakisema hawawezi kuendelea kubeba gharama huku wakipata hasara.
Chama cha Wamiliki wa Matatu nchini (MOA) pia kimemkosoa Rais William Ruto, kikimtaka kutekeleza ahadi aliyotoa Mei kwamba bei ya dizeli, ambayo ndiyo tegemeo kuu la usafiri wa umma, italindwa dhidi ya ongezeko kubwa.
Mnamo Jumatano, Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) iliongeza bei ya petroli kwa Sh12.93 kwa lita, dizeli Sh9.90 na mafuta ya taa Sh28.49. Bei hizo mpya zilianza kutumika jana Oktoba 15 hadi Novemba 14.
Katika jiji la Nairobi, lita moja ya petroli itauzwa kwa Sh226.96, dizeli Sh227.76 na mafuta ya taa Sh219.87 ilhali katika kaunti ya Mombasa, petroli itauzwa kwa Sh223.81, dizeli Sh224.61 na mafuta ya taa Sh216.71.
EPRA imesema ongezeko hilo limetokana na kupanda kwa bei kimataifa ya bidhaa za mafuta yanayoagizwa kutoka nje, huku mzozo wa Mashariki ya Kati ukichangia kuvuruga usambazaji.
Mwenyekiti wa MOA Albert Karakacha alisema hatua hiyo imekiuka makubaliano aliyodai wafikia na Rais Ruto katika mkutano wa wadau wa sekta ya uchukuzi uliofanyika Ikulu ya Mombasa mwezi Mei.
“Rais alituahidi tukiwa Mombasa kwamba hataongeza bei ya dizeli. Tulikutana naye kama wadau wa sekta ya uchukuzi na akatuhakikishia kuwa bei ya dizeli italindwa. Leo imeongezeka kwa Sh9.90 kwa lita. Ahadi hiyo imevunjwa,” alisema Karakacha.
Alimtaka Rais kuondoa ongezeko hilo, akionya kuwa wamiliki wa matatu hawawezi kuendelea kubeba gharama huku mapato yao yakipungua.
Alisema gharama za tairi zimepanda kutoka Sh25,000 hadi kati ya Sh38,000 na Sh45,000, huku bima kamili ya magari ikipanda kutoka takriban Sh180,000 hadi Sh250,000.
Karakacha pia alilalamikia ushuru wa magari ya umeme, betri na vifaa vya kuchaji, akisema ahadi ya kupunguza ushuru huo ili kurahisisha mabadiliko kuelekea magari yasiyotumia mafuta ya petroli haijatekelezwa.
“Biashara yetu haiwezi kuendelea kupata hasara. Tutalazimika kupitisha gharama hizo kwa abiria. Tumesukumwa hadi ukutani,” alisema.
Aliongeza kuwa chama hicho kitafanya mkutano wa dharura kujadili hatua za kuchukua na kukubaliana kuhusu msimamo wa pamoja wa wanachama wake.
Onyo hilo limeibua hofu ya kupanda kwa gharama ya usafiri kwa wafanyakazi, wanafunzi na familia ambazo tayari zinakabiliwa na gharama kubwa ya maisha.
Mzozo huo unakumbusha mgomo wa Mei 18 na 19 uliosababisha usumbufu mkubwa wa usafiri Nairobi na miji mingine baada ya bei ya dizeli kupanda hadi Sh242.92 kwa lita.
Mgomo huo ulisitishwa baada ya mazungumzo na serikali, ambapo Rais Ruto alitangaza punguzo la ziada la Sh10 kwa lita ya dizeli katika kipindi cha bei cha Juni hadi Julai.
MOA sasa inataka serikali kurejesha ruzuku ya mafuta au kuanzisha hazina ya kudhibiti mabadiliko ya bei, pamoja na kupitia upya ushuru wa bidhaa za petroli.
Hata hivyo, Karakacha hakutaja kiasi ambacho nauli zitaongezeka, akisema uamuzi huo utafanywa baada ya wanachama kushauriana.
Ongezeko la bei ya mafuta: Wamiliki wa matatu wasema nauli itapanda
WAMILIKI wa matatu wameonya kuwa huenda nauli ikapanda kufuatia ongezeko la bei ya mafuta, wakisema hawawezi kuendelea kubeba gharama huku wakipata hasara. Chama cha Wamiliki wa Matatu nchini (MOA) pia kimemkosoa Rais William Ruto, kikimtaka kutekeleza ahadi aliyotoa Mei kwamba bei ya dizeli, ambayo ndiyo tegemeo kuu la usafiri wa umma, italindwa dhidi ya ongezeko kubwa. Mnamo Jumatano, Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) iliongeza bei ya petroli kwa Sh12.93 kwa lita, dizeli Sh9.90 na mafuta ya taa Sh28.49. Bei hizo mpya zilianza kutumika jana Oktoba 15 hadi Novemba 14. Katika jiji la Nairobi, lita moja ya petroli itauzwa kwa Sh226.96, dizeli Sh227.76 na mafuta ya taa Sh219.87 ilhali katika kaunti ya Mombasa, petroli itauzwa kwa Sh223.81, dizeli Sh224.61 na mafuta ya taa Sh216.71. EPRA imesema ongezeko hilo limetokana na kupanda kwa bei kimataifa ya bidhaa za mafuta yanayoagizwa kutoka nje, huku mzozo wa Mashariki ya Kati ukichangia kuvuruga usambazaji. Mwenyekiti wa MOA Albert Karakacha alisema hatua hiyo imekiuka makubaliano aliyodai wafikia na Rais Ruto katika mkutano wa wadau wa sekta ya uchukuzi uliofanyika Ikulu ya Mombasa mwezi Mei. “Rais alituahidi tukiwa Mombasa kwamba hataongeza bei ya dizeli. Tulikutana naye kama wadau wa sekta ya uchukuzi na akatuhakikishia kuwa bei ya dizeli italindwa. Leo imeongezeka kwa Sh9.90 kwa lita. Ahadi hiyo imevunjwa,” alisema Karakacha. Alimtaka Rais kuondoa ongezeko hilo, akionya kuwa wamiliki wa matatu hawawezi kuendelea kubeba gharama huku mapato yao yakipungua. Alisema gharama za tairi zimepanda kutoka Sh25,000 hadi kati ya Sh38,000 na Sh45,000, huku bima kamili ya magari ikipanda kutoka takriban Sh180,000 hadi Sh250,000. Karakacha pia alilalamikia ushuru wa magari ya umeme, betri na vifaa vya kuchaji, akisema ahadi ya kupunguza ushuru huo ili kurahisisha mabadiliko kuelekea magari yasiyotumia mafuta ya petroli haijatekelezwa. “Biashara yetu haiwezi kuendelea kupata hasara. Tutalazimika kupitisha gharama hizo kwa abiria. Tumesukumwa hadi ukutani,” alisema. Aliongeza kuwa chama hicho kitafanya mkutano wa dharura kujadili hatua za kuchukua na kukubaliana kuhusu msimamo wa pamoja wa wanachama wake. Onyo hilo limeibua hofu ya kupanda kwa gharama ya usafiri kwa wafanyakazi, wanafunzi na familia ambazo tayari zinakabiliwa na gharama kubwa ya maisha. Mzozo huo unakumbusha mgomo wa Mei 18 na 19 uliosababisha usumbufu mkubwa wa usafiri Nairobi na miji mingine baada ya bei ya dizeli kupanda hadi Sh242.92 kwa lita. Mgomo huo ulisitishwa baada ya mazungumzo na serikali, ambapo Rais Ruto alitangaza punguzo la ziada la Sh10 kwa lita ya dizeli katika kipindi cha bei cha Juni hadi Julai. MOA sasa inataka serikali kurejesha ruzuku ya mafuta au kuanzisha hazina ya kudhibiti mabadiliko ya bei, pamoja na kupitia upya ushuru wa bidhaa za petroli. Hata hivyo, Karakacha hakutaja kiasi ambacho nauli zitaongezeka, akisema uamuzi huo utafanywa baada ya wanachama kushauriana.

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…