MWANAMUME mwenye umri wa miaka 61, wanawe watatu na mkwe wao wamepoteza rufaa waliyowasilisha kupinga kifungo cha jumla ya miaka 100 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kumshambulia jirani yao kufuatia ugomvi uliotokea baa.
Kifungo cha watano hao mnamo Aprili 2024 kilitokana na kukwama kwa juhudi za upatanisho zilizofanywa na chifu wa kijiji chao.
Bw John Ritho Kiboi na wanawe walihukumiwa kwa kosa la kumshambulia Bw John Gichuki.
Wakati wa juhudi za upatanisho, familia hiyo ilikubali kumlipa Bw Gichuki gharama ya matibabu iliyofikia Sh800,000. Hata hivyo, walikataa kulipa na wakaamua kushughulikia suala hilo mahakamani.
Mkasa huu ulianza baada ya mzozo kati ya Bw Kiboi na Bw Gichuki ndani ya baa iliyopo katika kituo cha biashara cha Ganyuthe, eneo la Kieni Magharibi, kaunti ya Nyeri, usiku wa Novemba 17, 2019.
Wawili hao walikuwa wakibugia vileo, kila mmoja akiwa ameketi meza tofauti. Bw Gichuki alikuwa na mkewe, huku Bw Kiboi akiwa na wateja wengine, akiwemo mkwe wake Evans Waititu.
Chanzo cha mzozo huo kilisemekana kuwa maneno ya kejeli yaliyotamkwa na kundi la Bw Kiboi, ambapo Bw Gichuki alisikiliza mazungumzo yao yaliyokuwa yakimdhalilisha yeye na familia yake kwa kuwaita watu wa kiburi. Baada ya muda, mke wa Bw Gichuki aliondoka baa hiyo.
Baadaye usiku, Bw Gichuki alivamiwa akiwa njiani kuelekea nyumbani na watu watano wanaoaminika kuwa ni Bw Kiboi, wanawe watatu – John Ritho, Paul Kiboi, na Kenneth Wachira – pamoja na mkwe wake Waititu. Walimsababishia majeraha mabaya yaliyohatarisha maisha yake.
Ingawa shambulio hilo lilifanyika gizani bila shahidi wa moja kwa moja, Bw Gichuki alisema aliweza kuwatambua waliomshambulia, na maelezo yake yaliaminiwa na polisi pamoja na mahakama.
Wakili wao, Dkt Adrian Kamotho, alidai kuwa vipengele muhimu vya kosa hilo havikuthibitishwa pasipo shaka yoyote ya msingi, hasa kutokana na ukosefu wa kuwatambua kikamilifu washukiwa waliodaiwa kumshambulia mlalamikaji.
“Mahakama ilikosea kwa kutegemea ushahidi bila kuzingatia hali ya mwanga na muda ambao tukio linadaiwa kufanyika, hali iliyofanya iwe vigumu kwa shahidi kufanya utambuzi wa maana. Kwa hivyo, walioshtakiwa walipata hukumu isiyo ya haki,” alisema Dkt Kamotho.
Mzozo katika baa ulivyosukuma baba, wanawe 3 na mkwe jela miaka 100
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
BusinessHofu ya wagonjwa wa saratani kukosa matibabu kufuatia mabadiliko ya SHA
WAGONJWA wa saratani nchini wameibua wasiwasi kuhusu kucheleweshwa kwa matibabu, kukataliwa kwa maombi ya dawa na kupunguzwa kwa kiwango cha fedha wanacholipiwa na Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA). Wanasema mfumo mpya wa kuidhinisha matibabu umewalazimu kulipa fedha za ziada ili kupata huduma ambazo awali ziligharamiwa kikamilifu na bima ya afya. Katika Hospitali ya Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga (JOOTRH), kati ya maombi 30 ya matibabu yaliyowasilishwa kwa SHA Jumatatu, ni 12 pekee yaliidhinishwa. Daktari mmoja mtaalamu wa saratani alisema hata wagonjwa walioidhinishwa walitakiwa kuongeza fedha kutoka mifukoni mwao. Alitaja mgonjwa wa saratani ya utumbo aliyelazimika kulipa Sh20,000 kwa vipimo, licha ya kuwa awali gharama hizo zililipwa na SHA. Daktari alisema hali hiyo imacha wagonjwa wasiojiweza kifedha wakisimamisha matibabu kwa kukosa pesa za kuongeza. Mgonjwa mmoja wa saratani ya matiti alisema kiwango chake cha fedha za kununua dawa ya Letrozole kimepunguzwa hadi Sh5,400, ilhali anahitaji zaidi ya Sh20,000 kwa dawa hiyo inayosaidia kudhibiti ukuaji wa saratani inayochochewa na homoni. “Ninahitaji zaidi ya Sh20,000 kununua dawa zangu. Kiasi hicho kinapopunguzwa nalazimika kuongeza fedha za ziada. Bila dawa hizo huenda nishindwe kudhibiti homoni,” akaeleza. Mfumo huo mpya pia umeongeza muda wa kusubiri dawa hospitalini. Maombi ya matibabu sasa yanahitaji kupitishwa na muuguzi, daktari mtaalamu na mfamasia kabla ya kuidhinishwa. Muuguzi katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta alisema foleni katika kliniki za saratani zinaongezeka huku wagonjwa wakingoja vibali. Mgonjwa Mary Adhiambo pia alisema kituo cha saratani cha Texas kimeacha kuuza dawa kwa wagonjwa wanaopokea matibabu katika hospitali zingine, na badala yake kuwataka wahamie huko. Mabadiliko hayo yameathiri wagonjwa wanaotibiwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta na Hospitali ya Mafunzo, Rufaa na Utafiti ya Chuo Kikuu cha Kenyatta (KUTRRH), ambao awali walinunua baadhi ya dawa katika vituo vingine. Mkur
BusinessAnthropic sets IPO price at $83 per share, targets $1.5trn valuation
–Claude maker raises $81.3bn in world’s largest IPO, overtakes SpaceX as investors rush for AI, despite $104bn lossBy Vera Anyagafu, with agency report The artificial intelligence race just produced the biggest stock market debut in history. Anthropic, the United States artificial intelligence company behind the Claude chatbot, on Wednesday priced its initial public offering at […]
BusinessOyedele urges banks to prioritise agricultural lending
…Commissions Moniepoint Abuja branch By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The Minister of Finance and Coordinating Minister of the Economy, Taiwo Oyedele, has urged banks and other financial institutions to make loans more affordable and accessible to businesses, particularly those operating in the agricultural sector, to stimulate productivity and economic growth. Oyedele made the call […]
BusinessNasarawa attracts $2.3bn investments in seven years — Abdullahi
Records 21 reforms, 11 PPP projects worth ₦93bn By John Alechenu ABUJA — Nasarawa State has attracted more than $2.3 billion in investments over the past seven years following reforms and institutional development aimed at making the state more competitive and investor-friendly. The Managing Director and Chief Executive Officer of the Nasarawa Investment and Development […]