Alikuwa mzee kutoka Ikwiriri, Rufiji, lakini jina lake lilifika mbali zaidi ya mipaka ya eneo aliloishi. Alikuwa si mchezaji, si kocha wala kiongozi wa klabu, lakini kwa miaka kadhaa sauti yake ilikuwa miongoni mwa zilizotengeneza burudani na hamasa katika soka la Tanzania.