MWANA wa mhubiri tata Paul Nthenge Mackenzie, Dan Mackenzie, ameeleza kuridhika kwake na hukumu iliyotolewa dhidi ya baba yake ya kupatikana na hatia ya kuua watoto 190 katika msitu wa Shakahola kati ya Januari 2021 na Septemba 2023.
Dan alisema hana sababu ya kuhuzunika kwa sababu ya mtu ambaye mafundisho yake yalimfanya aache shule akiwa Darasa la Saba na kujitafutia riziki kwa kuendesha bodaboda.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24, alisema hukumu hiyo imewaletea faraja familia zilizopoteza wapendwa wao katika mkasa huo, akisisitiza kwamba yeye mwenyewe alikuwa miongoni mwa walioathiriwa na mafundisho ya babake alipokuwa mtoto.
“Ni faraja kwetu na kwa waathiriwa waliopoteza wapendwa wao Shakahola. Haki imetendeka. Ilikuwa kipindi kigumu kwetu na kwa waathiriwa. Sasa tumepata faraja na tunasubiri hukumu ya adhabu,” alisema.
Dan, ambaye amejitenga na mafundisho ya kidini ya babake, alisema hakuhuzunishwa na uamuzi wa Jaji Diana Kavedza kwa sababu hakushiriki katika uhalifu huo.
“Sihuzuniki kwamba babangu amepatikana na hatia. Niko sawa na nimetulia kwa sababu sikuhusika. Ana hatia,” alisema katika Mahakama Kuu ya Mombasa, ambako Mackenzie na washtakiwa wenzake 28 walipatikana na hatia katika mashtaka yote 191 ya mauaji.
Hukumu hiyo ilimkumbusha Dan masaibu aliyopitia utotoni alipolazimishwa kufunga akiwa na umri wa miaka 12. Kukataa kwake kufunga kulizidisha uhasama kati yake na babake, na hatimaye akalazimika kuacha shule akiwa Darasa la Saba. Baadaye alianza kuendesha bodaboda mjini Malindi, kazi anayoendelea kufanya hadi sasa.
“Tulianza kufunga nilipokuwa na umri wa miaka 12. Nilikataa. Babangu alinikatia tamaa na kuniambia nijitegemee. Hivyo ndivyo nilivyoishia kuendesha bodaboda mjini Malindi,” alisema.
Dan pia alisimulia jinsi waumini wa kanisa hilo walivyompiga kwa karibu saa tatu kwa kukataa kuhudhuria ibada. Alimtaja Smart Mwakalama, naibu wa Mackenzie, kuwa miongoni mwa waliohusika.
“Nimeathiriwa na mambo ambayo babangu amekuwa akifanya huko Shakahola. Ndiyo maana sikuishia msituni, kwa sababu nilikuwa nimechoshwa naye. Nililazimishwa kufunga kwa wiki moja nilipokuwa na umri wa miaka 12. Waumini hao, akiwemo Smart Mwakalama, walinipiga kwa karibu saa tatu ili tu nihudhurie ibada,” alisema.
Mwakalama, mwanzilishi mwenza wa kanisa la Good News International Ministries (GNI), alielezwa kuwa mratibu muhimu wa usafirishaji wa wafuasi kutoka tawi la Furunzi mjini Malindi hadi msitu wa Shakahola.
Dan alisema alitambua uzito wa yaliyokuwa yakitendeka Shakahola baada ya babake kukamatwa Aprili 2023 na kesi kuanza kusikilizwa mahakamani.
“Hapo ndipo nilipogundua kwamba mambo aliyokuwa akitufanyia utotoni ndiyo aliyokuwa akifanya msituni,” alisema.
Pia alifurahia kuokolewa kwa ndugu zake watano, dada watatu na wavulana wawili, waliokuwa wakiishi na nyanya yao katika nyumba ya familia eneo la Furunzi tangu Mackenzie alipokamatwa. Dan alisema aliripoti hali yao kwa polisi, hatua iliyosababisha msako na kuokolewa kwao.
“Natumai sasa watakuwa na maisha mazuri,” alisema.
Wakati wa ziara ya Mahakama Kuu nyumbani kwa Mackenzie mwezi Juni, Dan aliambia mahakama kwamba ndugu zake walikuwa wamezama katika mafundisho ya babake na kwamba misimamo mikali ya kidini ilikuwa imekita mizizi katika familia.
Alitoa ushahidi huo katika kesi nyingine inayohusiana na mkasa huo, ambapo Mackenzie na wengine wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji kama uhalifu dhidi ya binadamu kuhusiana na vifo vya watu 53 katika kijiji cha Kwa Bi Nzaro.
Licha ya matendo ya babake, Dan alisema majirani zake wanaelewa kwamba hakuhusika na uhalifu huo.
Mwanawe Mackenzie asema ameridhishwa na hukumu
MWANA wa mhubiri tata Paul Nthenge Mackenzie, Dan Mackenzie, ameeleza kuridhika kwake na hukumu iliyotolewa dhidi ya baba yake ya kupatikana na hatia ya kuua watoto 190 katika msitu wa Shakahola kati ya Januari 2021 na Septemba 2023. Dan alisema hana sababu ya kuhuzunika kwa sababu ya mtu ambaye mafundisho yake yalimfanya aache shule akiwa Darasa la Saba na kujitafutia riziki kwa kuendesha bodaboda. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24, alisema hukumu hiyo imewaletea faraja familia zilizopoteza wapendwa wao katika mkasa huo, akisisitiza kwamba yeye mwenyewe alikuwa miongoni mwa walioathiriwa na mafundisho ya babake alipokuwa mtoto. “Ni faraja kwetu na kwa waathiriwa waliopoteza wapendwa wao Shakahola. Haki imetendeka. Ilikuwa kipindi kigumu kwetu na kwa waathiriwa. Sasa tumepata faraja na tunasubiri hukumu ya adhabu,” alisema. Dan, ambaye amejitenga na mafundisho ya kidini ya babake, alisema hakuhuzunishwa na uamuzi wa Jaji Diana Kavedza kwa sababu hakushiriki katika uhalifu huo. “Sihuzuniki kwamba babangu amepatikana na hatia. Niko sawa na nimetulia kwa sababu sikuhusika. Ana hatia,” alisema katika Mahakama Kuu ya Mombasa, ambako Mackenzie na washtakiwa wenzake 28 walipatikana na hatia katika mashtaka yote 191 ya mauaji. Hukumu hiyo ilimkumbusha Dan masaibu aliyopitia utotoni alipolazimishwa kufunga akiwa na umri wa miaka 12. Kukataa kwake kufunga kulizidisha uhasama kati yake na babake, na hatimaye akalazimika kuacha shule akiwa Darasa la Saba. Baadaye alianza kuendesha bodaboda mjini Malindi, kazi anayoendelea kufanya hadi sasa. “Tulianza kufunga nilipokuwa na umri wa miaka 12. Nilikataa. Babangu alinikatia tamaa na kuniambia nijitegemee. Hivyo ndivyo nilivyoishia kuendesha bodaboda mjini Malindi,” alisema. Dan pia alisimulia jinsi waumini wa kanisa hilo walivyompiga kwa karibu saa tatu kwa kukataa kuhudhuria ibada. Alimtaja Smart Mwakalama, naibu wa Mackenzie, kuwa miongoni mwa waliohusika. “Nimeathiriwa na mambo ambayo babangu amekuwa akifanya huko Shakahola. Ndiyo maana sikuishia msituni, kwa sababu nilikuwa nimechoshwa naye. Nililazimishwa kufunga kwa wiki moja nilipokuwa na umri wa miaka 12. Waumini hao, akiwemo Smart Mwakalama, walinipiga kwa karibu saa tatu ili tu nihudhurie ibada,” alisema. Mwakalama, mwanzilishi mwenza wa kanisa la Good News International Ministries (GNI), alielezwa kuwa mratibu muhimu wa usafirishaji wa wafuasi kutoka tawi la Furunzi mjini Malindi hadi msitu wa Shakahola. Dan alisema alitambua uzito wa yaliyokuwa yakitendeka Shakahola baada ya babake kukamatwa Aprili 2023 na kesi kuanza kusikilizwa mahakamani. “Hapo ndipo nilipogundua kwamba mambo aliyokuwa akitufanyia utotoni ndiyo aliyokuwa akifanya msituni,” alisema. Pia alifurahia kuokolewa kwa ndugu zake watano, dada watatu na wavulana wawili, waliokuwa wakiishi na nyanya yao katika nyumba ya familia eneo la Furunzi tangu Mackenzie alipokamatwa. Dan alisema aliripoti hali yao kwa polisi, hatua iliyosababisha msako na kuokolewa kwao. “Natumai sasa watakuwa na maisha mazuri,” alisema. Wakati wa ziara ya Mahakama Kuu nyumbani kwa Mackenzie mwezi Juni, Dan aliambia mahakama kwamba ndugu zake walikuwa wamezama katika mafundisho ya babake na kwamba misimamo mikali ya kidini ilikuwa imekita mizizi katika familia. Alitoa ushahidi huo katika kesi nyingine inayohusiana na mkasa huo, ambapo Mackenzie na wengine wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji kama uhalifu dhidi ya binadamu kuhusiana na vifo vya watu 53 katika kijiji cha Kwa Bi Nzaro. Licha ya matendo ya babake, Dan alisema majirani zake wanaelewa kwamba hakuhusika na uhalifu huo.

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…