MUDA mrefu kabla ya Migwena kuwa kitovu cha mikutano mikubwa ya kisiasa na kitamaduni nchini, uwanja huo uliokuwa ukitumiwa na vijana kutafuta wachumba na jamii jirani kusuluhisha tofauti zao kupitia michezo, ulikuwa na nafasi ya pekee katika historia ya familia ya Odinga.
Ni hapa, katika uwanja huo ulioko Bondo, Kaunti ya Siaya, ambapo Jaramogi Oginga Odinga, Makamu wa Rais wa kwanza wa Kenya, anasemekana kumwona kwa mara ya kwanza Mary Odima, mwanamichezo chipukizi aliyekuja kuwa mkewe na mama wa watoto wake, akiwemo Raila Odinga na Dkt Oburu Oginga.
Zaidi ya miaka 80 baadaye, Migwena inajiandaa kupokea maelfu ya wageni, viongozi wa kisiasa na wapenzi wa utamaduni watakaohudhuria maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, leo.
Uteuzi wa uwanja huo haukuwa wa bahati nasibu. Kwa familia ya Odinga na wakazi wa Sakwa, Migwena ni mahali ambapo kumbukumbu za familia, historia ya jamii na utamaduni vinaingiliana.
Uwanja huo wenye ukubwa wa takriban ekari 32, ulioko Wadi ya South Sakwa, Bondo, ulianza kutumiwa miaka ya 1930 kwa mashindano ya mieleka na mchezo wa bao, kabla ya kuwa kitovu cha shughuli za kitamaduni miaka ya 1960.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo, Akelo Gwela, Jaramogi alivutiwa na Mary alipomwona akishinda mbio za mita 100 wakati wa mashindano ya jamii.
Wawili hao walioana Januari 23, 1943, katika Shule ya Maseno, kisha wakafanya sherehe za kimila Sakwa. Miezi tisa baadaye, Mary alijifungua Oburu, ambaye baadaye alifuatwa na Raila.
Kwa miaka mingi, Migwena iliwaleta pamoja watu kutoka maeneo mbalimbali ya Nyanza, ikikuza mshikamano na amani kupitia michezo na sherehe za kitamaduni.
Ingawa shughuli zake za kila mwaka zilianza kupungua baada ya serikali za kaunti kuanzishwa mwaka 2013, uwanja huo unaendelea kuwa muhimu kihistoria.
Kwa familia ya Odinga, kurejea Migwena kuadhimisha Raila ni kurejea mahali ambapo simulizi la familia yao lilipoanzia.
Migwena: Uwanja wa mapenzi na historia ya familia ya Odinga

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…