ALIZETI ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikitumika kama malighafi ya utengenezaji mafuta ya kupikia na kuunda chakula cha mifugo, maua yake sasa yameanza kushabikiwa kurembesha mazingira.
Yamegeuka kuwa kivutio kipya na kuorodheshwa miongoni mwa maua ya mapambo yanayouzwa ng’ambo.
Kenya, ikijivunia kuwa miongoni mwa wazalishaji nguli wa maua duniani na kushikilia nafasi ya nne katika uuzaji wa maua hususan ya umaridadi, sasa inajumuisha alizeti kwenye orodha ya maua yenye ushindani mkuu sokoni.
Aghalabu, Kenya husafirisha asilimia 99 ya maua yake kwa zaidi ya nchi 80 ulimwenguni haswa aina ya waridi ‘rose’, carnation na alstroemeria. Alizeti sasa imejiunga rasmi na utandawazi huu wa maua ya kuvutia.
[caption id="attachment_173896" align="aligncenter" width="300"] Alizeti sasa inakumbatiwa kama maua ya urembesho. Picha|Sammy Waweru[/caption]
Ikiwa nyuma ya Colombia na Ecuador, katika nafasi ya tatu kimataifa kwa uzalishaji wa maua yaliyokatwa, Kenya inalenga kubadilisha sura ya maua yake kwa kuingiza maua ya kiangazi (summer flowers) yenye rangi ang’avu na matumizi mbalimbali, na alizeti inashirikishwa kwenye mageuzi haya.
Mbali na alizeti, maua mengine ya kiangazi ambayo yanaongeza upekee katika masoko ambayo Kenya inawahi ni pamoja na gypsophila, delphinium, limonium, snapdragons, matthiola incana, marigold, na lisianthus.
“Alizeti imekuwa ikijulikana kwa utengenezaji wa mafuta na chakula cha mifugo, lakini kutokana na utafiti tumezalisha aina mpya zinazoshabikiwa sokoni kama maua ya mapambo,” anasema Mildred Anyango, Mwakilishi wa Mauzo wa Ball SB ukanda wa Afrika Mashariki, kampuni ya kimataifa ya uzalishaji maua.
Ball SB, tawi la kampuni ya Ball Horticultural yenye makao yake makuu Chicago, Amerika, inashughulika na uzalishaji, upandikizaji na usambazaji wa miche kwa wakulima wa kitaalamu.
[caption id="attachment_173897" align="aligncenter" width="300"] Mildred Anyango, Mwakilishi wa Mauzo wa Ball SB ukanda wa Afrika Mashariki akikagua mashada ya maua ya alizeti wakati wa Makala ya 13 ya Maonyesho ya Kimataifa ya Maua (IFTEX) 2025, yaliyofanyika Jijini Nairobi. Picha|Sammy Waweru[/caption]
Anyango anaeleza kuwa ipatayo miaka mitano iliyopita, walitambua mwanya katika soko la maua ya mapambo, na wakajumuisha aina maalum za alizeti zilizobuniwa kwa ajili ya mashada na mapambo ya kifahari.
“Awali, mashada ya maua yalitawaliwa na waridi. Lakini sasa, maua ya alizeti yanachangia kuboresha rangi, haiba, na kuleta furaha ya kipekee,” anasema Anyango.
Tofauti na alizeti za kawaida zenye kichwa kikubwa kwa ajili ya mafuta, aina za mapambo zimezalishwa kwa minajili ya muonekano—zikiwa na rangi mbalimbali na muundo wa petali (petals) wa kuvutia.
Miongoni mwa aina maarufu ni Ziggy, yenye petali mbili zenye rangi mseto, Marley – yenye rangi mbili pia na mvuto wa kipekee, Carnival Sun yenye maua makubwa yenye petali nyingi, Pro-cut Red yenye petali nyekundu za kuvutia, na Vincent Fresh – aina isiyo ya kawaida yenye kitovu cha kijani.
[caption id="attachment_173898" align="aligncenter" width="300"] Alizeti maridadi ya rangi ya manjano. Picha|Sammy Waweru[/caption]
“Aina hizi si tu nzuri kwa macho, bali pia ni rahisi kusafirisha, hudumu kwa muda mrefu (ikilinganishwa na maua mengine) na hazichukui nafasi kubwa kwenye ndege (freight),” Anyango akaambia Akilimali kwenye mahojiano ya kipekee.
Ball SB ilikuwa miongoni mwa kampuni zinazozalisha maua, kujamiisha, za kupandikiza, kusafirisha ng’ambo, na wadauhusika wengine waliohudhuria Makala ya 13 ya Maonyesho ya Kimataifa ya Maua (IFTEX) 2025, yaliyofanyika Jijini Nairobi, kuanzia Juni 5.
Baadhi ya wazalishaji wa Kenya tayari wanasafirisha aina hizo mpya za alizeti kwa masoko ya ughaibuni kama vile Ulaya na na nchi za Uarabuni za Mashariki ya Kati, ambayo ni masoko ya jadi ya maua ya Kenya. Soko vilevile limepanuka hadi Asia Mashariki.
Kulingana na Clement Tulezi, Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza la Maua Kenya ‘Kenya Flower Council’, ongezeko la maua ya kiangazi kama vile alizeti linachangia ukuaji wa sekta hii.
[caption id="attachment_173899" align="aligncenter" width="300"] Kulingana na Mildred Anyango kutoka Ball SB alizeti inatumika kupiga jeki maua mengine kwenye mashada. Picha|Sammy Waweru[/caption]
“Tunaendelea kushuhudia ongezeko la masoko mapya Barani Asia na maeneo mengine ya Ulaya,” Tulezi anasema.
Isitoshe, kuna mabadiliko jinsi maua yanavyosafirishwa—wazalishaji sasa wakiandaa mashada tayari kwa matumizi ya moja kwa moja sokoni badala ya kusafirisha yakiwa maua ghafi.
Tulezi anasema hatua hiyo inaongeza thamani kwenye maua, na kuvutia soko la ndani kwa ndani Kenya ambalo kwa muda mrefu halijakuwa la kuridhisha.
“Ingawa kiwango cha matumizi ya maua humu nchini bado ni cha chini, baadhi ya wapenzi wa maua wameonyesha kuvutiwa na yale ya alizeti,” Anyango anakiri.
Anahimiza haja ya Wakenya kufurahia mashada ya maua, kama inavyoshuhudiwa Ulaya. Alizeti za mapambo pia ni rahisi kulima, na zinakomaa kwa muda mfupi – karibu miezi miwili. Kwa wenye chanzo cha maji, wanakuza mfululizo hivyo basi kudumisha wanunuzi.
[caption id="attachment_173900" align="aligncenter" width="300"] Maua maridadi, yakiwemo ya alizeti ambayo Ball SB huzalisha mbegu na miche yake kwa minajili ya ukuzaji kuwahi masoko ya ng'ambo. Picha|Sammy Waweru[/caption]
Maua ya alizeti yavutia masoko ng’ambo
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
BusinessHofu ya wagonjwa wa saratani kukosa matibabu kufuatia mabadiliko ya SHA
WAGONJWA wa saratani nchini wameibua wasiwasi kuhusu kucheleweshwa kwa matibabu, kukataliwa kwa maombi ya dawa na kupunguzwa kwa kiwango cha fedha wanacholipiwa na Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA). Wanasema mfumo mpya wa kuidhinisha matibabu umewalazimu kulipa fedha za ziada ili kupata huduma ambazo awali ziligharamiwa kikamilifu na bima ya afya. Katika Hospitali ya Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga (JOOTRH), kati ya maombi 30 ya matibabu yaliyowasilishwa kwa SHA Jumatatu, ni 12 pekee yaliidhinishwa. Daktari mmoja mtaalamu wa saratani alisema hata wagonjwa walioidhinishwa walitakiwa kuongeza fedha kutoka mifukoni mwao. Alitaja mgonjwa wa saratani ya utumbo aliyelazimika kulipa Sh20,000 kwa vipimo, licha ya kuwa awali gharama hizo zililipwa na SHA. Daktari alisema hali hiyo imacha wagonjwa wasiojiweza kifedha wakisimamisha matibabu kwa kukosa pesa za kuongeza. Mgonjwa mmoja wa saratani ya matiti alisema kiwango chake cha fedha za kununua dawa ya Letrozole kimepunguzwa hadi Sh5,400, ilhali anahitaji zaidi ya Sh20,000 kwa dawa hiyo inayosaidia kudhibiti ukuaji wa saratani inayochochewa na homoni. “Ninahitaji zaidi ya Sh20,000 kununua dawa zangu. Kiasi hicho kinapopunguzwa nalazimika kuongeza fedha za ziada. Bila dawa hizo huenda nishindwe kudhibiti homoni,” akaeleza. Mfumo huo mpya pia umeongeza muda wa kusubiri dawa hospitalini. Maombi ya matibabu sasa yanahitaji kupitishwa na muuguzi, daktari mtaalamu na mfamasia kabla ya kuidhinishwa. Muuguzi katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta alisema foleni katika kliniki za saratani zinaongezeka huku wagonjwa wakingoja vibali. Mgonjwa Mary Adhiambo pia alisema kituo cha saratani cha Texas kimeacha kuuza dawa kwa wagonjwa wanaopokea matibabu katika hospitali zingine, na badala yake kuwataka wahamie huko. Mabadiliko hayo yameathiri wagonjwa wanaotibiwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta na Hospitali ya Mafunzo, Rufaa na Utafiti ya Chuo Kikuu cha Kenyatta (KUTRRH), ambao awali walinunua baadhi ya dawa katika vituo vingine. Mkur
BusinessAnthropic sets IPO price at $83 per share, targets $1.5trn valuation
–Claude maker raises $81.3bn in world’s largest IPO, overtakes SpaceX as investors rush for AI, despite $104bn lossBy Vera Anyagafu, with agency report The artificial intelligence race just produced the biggest stock market debut in history. Anthropic, the United States artificial intelligence company behind the Claude chatbot, on Wednesday priced its initial public offering at […]
BusinessOyedele urges banks to prioritise agricultural lending
…Commissions Moniepoint Abuja branch By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The Minister of Finance and Coordinating Minister of the Economy, Taiwo Oyedele, has urged banks and other financial institutions to make loans more affordable and accessible to businesses, particularly those operating in the agricultural sector, to stimulate productivity and economic growth. Oyedele made the call […]
BusinessNasarawa attracts $2.3bn investments in seven years — Abdullahi
Records 21 reforms, 11 PPP projects worth ₦93bn By John Alechenu ABUJA — Nasarawa State has attracted more than $2.3 billion in investments over the past seven years following reforms and institutional development aimed at making the state more competitive and investor-friendly. The Managing Director and Chief Executive Officer of the Nasarawa Investment and Development […]