KUFUATIA kifo cha kutatanisha cha binti wa Seneta wa Nakuru Tabitha Karanja, mahakama Ijumaa iliamuru ashtakiwe kwa mauaji.
Hakimu mwandamizi Mahakama ya Kibera, Bi Zainab Abdul aliamuru Omari Lali ashtakiwe kwa mauaji ya Tecra Mungai.
Tecra aliyetazamiwa kuwa mrithi wa kiwanda cha kutengeneza mfinyo cha Keroche Breweries (KBL) kilichoko Naivasha alikufa katika mazingira tata katika hoteli moja ya kitalii eneo la Pwani.
Bi Abdul aliyechunguza kifo hicho alifikia uamuzi kwamba “Omari Lali ashtakiwe kwa mauaji.”
Akitoa uamuzi hakimu alisema “baada ya kutathmini ushahidi niliopokea ni bayana kwamba lawama za mauaji ya Tecra zinamuota mpenziwe Omari Lali.”
Hakimu aliendelea kusema kwamba ushahidi wote uliowasilishwa umebaini ni yeye (Omari Lali) aliyehusika na kifo cha Tecra.
Familia ya Karanja iliwakilishwa katika uchunguzi huo na wakili mwenye tajriba ya juu James Orengo na wakili Profesa Elisha Ongoya.
Baada ya kupokea taarifa za mashahidi zaidi ya 20 hakimu alisema “Lali alihusika na mauaji ya Tecra.”
Kufuatia uamuzi Bi Abdul aliamuru faili ya kesi hiyo ipelekewe Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Renson Ingonga ndipo amfungulie mashtaka ya mauaji Omari Lali.
Awali Lali alikuwa ameshtakiwa kwa mauaji lakini DPP wa zamani Noordin Haji alisitisha mashtaka na kuamuru uchunguzi ufanywe na idara ya mahakama kubaini kilicho sababisha kifo cha Tecra.
"Nimefikia uamuzi kwamba Lali alihusika na kifo cha Tecra. Hivyo basi hii imepata kwamba Lali alihusika na mauaji ya Tecra,” alisema Bi Abdul Ijumaa katika uamuzi aliosoma kupitia video mtandaoni.
Alimpendekezea DPP Lali ashtakiwe kwa mauaji kinyume cha Sheria Nambari 203 na 204 za Uhalifu.
Hakimu alisema kwamba fuvu la kichwa cha Tecra lilikuwa limepasuka mbali na majeraha mengine aliyokuwa nayo binti huyo wa mmiliki wa kampuni ya pombe ya Keroche Breweries.
Mahakama ilisema Tecra na Lali walikuwa wawili tu alipokufa.
Hakimu alisema ijapokuwa Lali alijitetea kwamba Tecra alianguka na kujeruhiwa ni bayana majeraha aliyopata hayaambatani na mtu aliyeanguka.
Hakimu alisema ubongo wa Tecra ulikuwa na majeraha mabaya.
Pia alisema Lali alijikanganya katika ushahidi wake. Kabla ya kifo chake Tecra watu wa familia yake walikuwa wamemshinikiza avunje urafiki wake na Lali.
Sasa DPP atapata samanzi siku ile Lali atafika kortini kufunguliwa mashtaka ya mauaji yaliyotokea Aprili 2020
Mashahidi zaidi ya 20 walivyomhusisha Lali na kifo cha binti wa Keroche
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
Travel
TravelTANAPA calls for active investment to promote tourism in Lake Zone
GEITA: THE Tanzania National Parks Authority (TANAPA) has called on development stakeholders in the Lake Zone, including mineral miners, to seize investment opportunities in the tourism sector. TANAPA Head of Business Development Unit, Ms Jully Bede Lyimo, made the call recently during a special meeting between TANAPA and development stakeholders held in Geita Municipality. She…
TravelShivo Tanzania’s Richard Ashby elected to ZATI board of directors
ZANZIBAR: Richard Ashby of Shivo Tanzania has been elected to the Board of Directors of the Zanzibar Association of Tourism Investors (ZATI), following the association’s Annual General Meeting (AGM) and board elections held in Zanzibar on Wednesday. Ashby secured 47 votes in a competitive contest involving 10 candidates, earning one of four positions on the…
TravelUnited Nigeria Airlines begins Jos flights to Lagos, Kano, Owerri
United Nigeria Airlines will commence scheduled flight operations from Jos to Lagos, Kano and Owerri on November 24 and 29, 2026, providing residents of Plateau State with additional air connections to other parts of the country. The airline said tickets for the new routes were already available for purchase. The Lagos–Jos–Lagos route will operate four […]