WAKAZI wa Kisumu wameheshimu wosia wa marehemu Raila Odinga wa kuhimiza mazungumzo kati ya vijana na wazee kuhusu changamoto za kijamii, kisiasa na kiuchumi zinazokabili jamii.
Hafla hiyo iliyoleta pamoja wazee na vijana. ilifanyika katika Ukumbi wa Ofafa Memorial, kama sehemu ya shughuli za siku tatu za kuadhimisha maisha na urithi wa Raila kabla ya mwaka mmoja tangu kifo chake Alhamisi, Oktoba 15, 2026.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadhimisho ya Raila, Prof Adams Oloo, alisema ilikuwa muhimu kuanzisha shughuli hizo kwa kuwakutanisha wazee waliomfahamu Raila na vijana waliovutiwa na ujasiri na uzalendo wake.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Luo, Ker Odungi Randa, aliwahimiza vijana kujifunza mila na desturi za jamii yao, akisema kuporomoka kwa mifumo ya jadi kumevuruga malezi na ushauri kwa vijana.
Alitaja mifumo kama Siwindhe, iliyotumiwa kuwaandaa wasichana kuhusu ndoa, na Duol, ambako wavulana walifundishwa majukumu yao katika familia na jamii.
Randa pia aliwataka vijana kudumisha amani na kuepuka kutumia simu kutukana viongozi, akionya kuwa tabia hiyo inaweza kuwaweka hatarini.
Mwakilishi wa vijana, Victoria Adwet, alisema mitandao ya kijamii imechangia pengo kati ya vizazi kwa sababu vijana hawapati nafasi za kutosha kujifunza tamaduni zao.
Aliomba wazee na vijana washirikiane, huku akitaka mitandao ya kijamii itumiwe kuwafikia vijana na kuwahamasisha kushiriki shughuli za kitamaduni.
Vijana pia walipendekeza kuanzishwa kwa Baraza la Vijana wa Luo ili kuwawezesha kushirikiana na wazee na kushiriki masuala ya jamii.
Askofu Joseph Ouko wa Evangelical Youth Alliance, Nyanza, alisema vijana watahitaji uwazi, vita dhidi ya ufisadi na uteuzi huru na wa haki wa wagombea wa vyama.
Mjane wa aliyekuwa Ker wa Luo, Willis Otondi, Lillian Otondi, aliwataka kina mama kurejea katika malezi ya jadi na kuwafundisha wasichana kuhusu familia, ndoa na malezi ya watoto.
Shughuli hizo zitahitimishwa Alhamisi, Oktoba 15, katika uwanja wa Migwena, Bondo, ambako Rais William Ruto na viongozi wengine wanatarajiwa kuhudhuria.
Kabla ya hapo, Jumatano, Oktoba 14, kutakuwa na hafla ya kimataifa ya kuwasha mishumaa Kang’o ka Jaramogi kuanzia saa kumi na mbili jioni, ikiongozwa na Mama Ida Odinga. Wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za ufundi pia watashiriki zoezi la kutoa damu mjini Kisumu.
Maadhimisho ya Raila – Vijana na wazee wakumbuka wosia wake

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…