JAMII ya Ilimanyang katika Kaunti ya Turkana inataka itambuliwe rasmi kama watu wenye ulemavu kutokana na hali adimu ya kiafya inayowafanya washindwe kutoa jasho, jambo linalohatarisha maisha yao katika joto kali la eneo hilo.
Jamii hiyo inayokadiriwa kuwa na watu 600, wengi wao wakiishi katika kijiji cha Kapua, Turkana ya Kati, hulazimika kunyunyiziwa maji mara kwa mara ili kupunguza joto na kuzuia miili yao kupata joto kupita kiasi.
Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Jinsia na Usawa (NGEC), Rehema Jaldesa, amesema tume hiyo itashirikiana na wataalamu wa afya kufanya uchunguzi kubaini hali hiyo na hatua zinazofaa kuchukuliwa.
Afisa mkuu wa huduma za afya Turkana, Gilchrist Lokoel, alisema dalili zilizoripotiwa zinafanana na ugonjwa adimu wa kurithi unaojulikana kama hypohidrotic ectodermal dysplasia (HED), unaoweza kuathiri tezi za jasho, nywele na meno.
Hata hivyo, alisema uchunguzi wa kina unahitajika kuthibitisha iwapo jamii hiyo ina ugonjwa huo.
Nancy Ebolon, ambaye amekuwa akipigania haki za watu wa Ilimanyang, alisema waathiriwa hulazimika kula mara kwa mara na kunyunyiziwa maji ili kuendelea kuishi katika mazingira yenye joto kali.
“Mtu hapa Ilimanyang huzimia asipokula ndani ya saa moja au asipopata maji ya kunyunyiziwa mwilini baada ya nusu saa. Hali ikizidi kuwa mbaya, hufariki,” alisema.
Alisema watoto wanaozaliwa na hali hiyo wako katika hatari kubwa zaidi, kwani huhitaji uangalizi wa karibu na kupozwa mara kwa mara ili kuzuia miili yao kupata joto kupita kiasi.
Mbali na changamoto za kiafya, jamii hiyo inakabiliwa na unyanyapaa na imani potofu. Baadhi ya watoto wanaozaliwa na hali hiyo hukataliwa na baba zao, hali inayozidisha mateso ya familia zinazowalea.
Elimu pia imeathirika kutokana na mazingira magumu wanayoishi. Jaldesa alisema baadhi ya wanafunzi hulazimika kusafiri kilomita 120 kwenda na kurudi ili kufanya mitihani ya kitaifa.
“Mtoto anawezaje kusafiri kilomita 120 katika joto kali kwa siku moja ili kufanya mtihani?” aliuliza, akitaka mipango maalumu ya kuwasaidia wanafunzi hao.
Jaldesa alisema NGEC itaratibu kambi ya matibabu na kushirikisha Baraza la Kitaifa la Watu Wenye Ulemavu ili kubaini uwezekano wa jamii hiyo kusajiliwa na kupata msaada wa serikali.
Kutambuliwa kama walemavu kunaweza kuwawezesha watu wa jamii hiyo kupata huduma maalumu za afya, elimu na ulinzi wa kijamii.
Hata hivyo, jamii hiyo pia inakabiliwa na uhaba wa maji, umaskini na changamoto za kupata vitambulisho vya taifa na vyeti vya kuzaliwa, hali inayoweza kuwazuia kupata huduma muhimu.
Wanatumai kuwa kutambuliwa rasmi kutasaidia kupunguza ubaguzi na kufungua njia ya kupata huduma zinazozingatia mahitaji yao ya kipekee.
Kukosa kutoka jasho ni ulemavu? Jamii yataka kutambuliwa rasmi

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…