KAMPUNI ya stima Kenya (KPLC) imekanusha madai kuwa iliondoa transfoma 15 kutoka maeneo mbalimbali katika eneo bunge la Mbeere North, Kaunti ya Embu, kwa sababu za kisiasa, ikisema vifaa hivyo vilichukuliwa kwa ukarabati wa kawaida.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Meneja wa KPLC Kaunti ya Embu, Bw Vincent Okello, alisema transfoma zinapopata hitilafu kama kuingia maji au kasoro nyingine ambazo haziwezi kurekebishwa zikiwa eneo la matumizi, hupelekwa kwenye karakana maalumu kwa ukarabati, majaribio na kukaushwa kwa teknolojia maalumu ili kurejesha ubora wake.
Alisema kati ya Mei na Juni mwaka huu, transfoma 15 ziliondolewa Mbeere North kutengenezwa.
Kati ya hizo, 14 tayari zimerejeshwa na kufungwa upya, huku moja iliyoharibiwa na wahuni wiki iliyopita ikibadilishwa Ijumaa.
"Kazi hizi ni za kiufundi pekee na zinalenga kuhakikisha wananchi wanapata umeme salama, wa kutegemewa na ulio thabiti," alisema Bw Okello.
Hata hivyo, wakazi walipinga madai kwamba walihusishwa kabla ya transfoma hizo kuondolewa. Walisema walishtushwa na hatua hiyo na kudai baadhi ya transfoma zilirejeshwa usiku baada ya vyombo vya habari kuripoti kuhusu kero hiyo.
KPLC yakanusha madai ya kuhamishia transfoma Mbeere North kwa sababu ya kisiasa
Taifa Leo 1 min read

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsTinubu’s re-election campaign backed by visible evidence, not just promises — Oshiomhole
"The real campaign is not about promising what we will do. It is about showing what President Tinubu is already doing"
Vanguard News 1 min read
NewsTAARIFA YA HABARI YA ASUBUHI: NOV 21, 2026
Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania
ITV Tanzania Video
News
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
Vanguard News 1 min read