NAIBU Rais Kithure Kindiki amesema amefanya mkutano mtandaoni na Rais William Ruto ambapo wamejadili suala la mgomo wa wahudumu wa uchukuzi ambao umesababisha shughuli za usafiri kukwama kote nchini.
Prof Kindiki amesema haya wakati wa mkutano na viongozi wa Tharaka uliofanyika nyumbani kwake, Irunduni, Kaunti ya Tharaka Nithi. Rais Ruto naye yumo ziarani nchini Azerbaijan.
Mgomo wa wahudumu wa uchukuzi ulioanza kutekelezwa saa sita usiku wa kuamkia Jumatatu umelemaza huduma na biashara katika miji mingi huku Nairobi, Kitengela, Meru, Murang’a, Machakos, Kitale ikiwa miongoni mwa iliyoathirika zaidi.
Kufikia saa kumi jioni, usafiri bado ulikuwa nadra katika maeneo mengi huku magari machache yaliyoonekana barabarani yakipigwa mawe na vijana au kushurutishwa kuondoka.
Katika miji ya Ruiru, Kasarani na Juja, Nairobi, polisi walikuwa na wakati mgumu kukabiliana na makundi ya wakazi walioanza kuimba nyimbo za kukashifu serikali. Polisi walilazimika kurusha vitoa machozi kutawanya waandamanaji huku hali ikiendelea kuwa ya taharuki.
Kindiki: Ruto ameitisha mkutano saa kumi jioni kuangalia vile tutapunguza bei ya mafuta
Taifa Leo 1 min read

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsMAGAZETI NOV 21, 2026: SAMIA KATIBA MPYA ITAPATIKANA 2028/29
Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania
ITV Tanzania Video
NewsTinubu’s re-election campaign backed by visible evidence, not just promises — Oshiomhole
"The real campaign is not about promising what we will do. It is about showing what President Tinubu is already doing"
Vanguard News 1 min read
NewsTAARIFA YA HABARI YA ASUBUHI: NOV 21, 2026
Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania
ITV Tanzania Video
News