USHIRIKIANO wa kisiasa alioanzisha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga na Rais William Ruto kabla ya kifo chake Oktoba 15 2025, sasa unaingia katika hatua muhimu huku vyama vya UDA na ODM vikijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa Agosti 10, 2027.
Kazi kubwa iliyobaki ni kutimiza ahadi za makubaliano yao, kuafikiana kuhusu ugavi wa mamlaka na kuunda muungano utakaoweza kustahimili ushindani wa kisiasa kuelekea uchaguzi ujao.
Vyama hivyo vimeunda timu ya wataalamu 10, watano kutoka kila upande, kuandaa manifesto ya pamoja itakayounganisha sera zao na kutathmini utekelezaji wa ahadi zilizotolewa mwaka 2022.
Timu hiyo inajumuisha wawakilishi wa UDA na ODM, huku wakurugenzi wakuu wa vyama hivyo, Nicodemus Bore na Oduor Ong’wen, wakishiriki kwa mujibu wa nyadhifa zao.
Bw Bore alisema lengo ni kuhakikisha ahadi za awali zinatimizwa na mahitaji ya maeneo yote nchini yanazingatiwa.
“Tunataka kuhakikisha kwamba ahadi tulizotoa mwaka 2022 zinatekelezwa kikamilifu,” alisema.
Hata hivyo, kuandaa manifesto ya pamoja ni sehemu moja tu ya kazi aliyobakisha Raila. Changamoto kubwa ni iwapo vyama hivyo vitaafikiana kuhusu jinsi vitakavyoshiriki uchaguzi na kugawana nafasi za uongozi katika serikali ijayo.
Ushirikiano huo ulianza kuimarika baada ya maandamano ya vijana wa Gen Z mwaka 2024, yaliyotoa presha kwa serikali ya Rais Ruto.
Rais aliwateua viongozi kadhaa wa ODM katika Baraza la Mawaziri mnamo Julai mwaka huo, kabla ya kutia saini makubaliano na Raila katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta (KICC) Machi 7, 2025.
Makubaliano hayo yalijumuisha ajenda ya vipengele 10, ikiwemo utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati ya Mdahalo wa Kitaifa (NADCO), kuimarisha ugatuzi, kuwawezesha vijana, kupambana na ufisadi, kupunguza matumizi mabaya ya fedha za umma na kulinda utawala wa sheria.
Baada ya kifo cha Raila, kiongozi wa ODM Oburu Oginga amesisitiza kuwa serikali inapaswa kutekeleza ahadi hizo ili kuonyesha kuwa ushirikiano huo una manufaa kwa Wakenya.
Bw Oginga amesema mazungumzo kuhusu uchaguzi wa 2027 yanapaswa kuzingatia ugavi wa mamlaka kwa uwiano wa asilimia 50 kwa 50.
Mnamo Julai, alitangaza kuwa ODM haitawasilisha mgombea wake wa urais, bali itaunga mkono kuchaguliwa tena kwa Rais Ruto. Viongozi wa ODM sasa wanataka chama hicho kiteue mgombea mwenza wa Rais, nafasi inayoshikiliwa na Naibu Rais Kithure Kindiki.
Pendekezo hilo limezua wasiwasi miongoni mwa washirika wa Rais wanaotaka Profesa Kindiki aendelee na wadhifa huo.
Pia kuna kazi ya kukamilisha mageuzi ya uchaguzi yaliyotokana na mapendekezo ya NADCO. IEBC imeonya kuwa kucheleweshwa kwa sheria muhimu kunaweza kuathiri maandalizi ya uchaguzi, ikiwemo mipango ya kiutendaji na ununuzi wa vifaa.
Miswada inayosubiriwa inahusu sheria za uchaguzi, makosa ya uchaguzi na vyama vya kisiasa, pamoja na mapendekezo kuhusu usajili wa wapigakura, teknolojia ya uchaguzi na ufadhili wa kampeni.
Hata hivyo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna anapinga dhana kwamba chama hicho kimeachana na azma ya kuwania urais.
Anasema ushirikiano huo ulilenga kudumisha utulivu wa kidemokrasia na kuwapa Wakenya nafasi ya kumuondoa Rais Ruto madarakani kupitia kura.
Anarejelea matamshi ya Raila wiki chache kabla ya kifo chake, alipouliza kwa nini watu walidhani ODM haitakuwa na mgombea urais mwaka 2027.
Hivyo basi, kazi aliyobakisha Raila si kuunganisha vyama viwili pekee, bali pia kuhakikisha ahadi za mageuzi zinatekelezwa na kwamba tofauti kuhusu mamlaka hazivunji ushirikiano huo kabla ya uchaguzi wa 2027.
Kazi aliyobakisha Raila kabla ya kifo chake

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…