MAMLAKA ya Kudhibiti Kawi na Petroli (EPRA) imeongeza bei ya bidhaa za mafuta katika hatua ambayo imeamsha hisia mseto na kuashiria siku ngumu zijazo kwa Wakenya.
Kutokana na hatua hiyo, bei mpya mafuta ya Super Petroli sasa ni Sh226.96 kwa lita, Sh227.85 kwa dizeli na Sh219.87 kwa mafuta ya taa jijini Nairobi.
Bei ya mafuta ya taa imeongezeka kwa Sh28.49 huku petroli ikipanda kwa Sh12.93 na dizeli kwa Sh9.90 kwa kila lita.
Ongezeko hilo la bei ya bidhaa za mafuta limechangiwa na sababu mbalimbali, ikiwemo machafuko yanayoendelea Mashariki ya Kati kuhusiana na vita vya Israel na Amerika dhidi ya Iran, kulingana na Mkurugenzi wa EPRA, Edward Mwirigi.
Aidha, uamuzi wa serikali kusitisha ruzuku ya mafuta umechangia ongezeko la bei.
“Septemba imekuwa mwezi mbaya zaidi tangu vita vilipozuka,” alisema Bw Mwirigi akihutubia vyombo vya habari.
Alifafanua kuwa hatua ya kupunguza ushuru wa ongezeko la thamani (VAT) kwa bidhaa za mafuta kutoka asilimia 16 hadi nane itaendelea kutekelezwa hadi Januari 14 ili kuwalinda Wakenya dhidi ya gharama kubwa za mafuta.
Hata hivyo, hatua hiyo huenda isitoshe kuzuia athari za kupanda kwa bei ya mafuta duniani, ambazo tayari zinatishia kuongeza gharama ya maisha nchini.
Bei ya mafuta ghafi ya Brent ilipanda na kuvuka Dola 100 kwa pipa mwezi uliopita, huku ikiuzwa kwa Dola 105.98 Jumatano, kutokana na misukosuko iliyotokana na vita Mashariki ya Kati.
Mapigano hayo yamevuruga usambazaji wa mafuta baada ya Iran kushambulia miundomsingi muhimu katika eneo la Ghuba, ikiwemo mitambo ya kusafisha mafuta na mabomba ya kusafirisha mafuta.
Mafuta ghali yanatarajiwa kuongeza gharama za usafiri, kilimo na uzalishaji viwandani, huku wafanyabiashara na watoa huduma wakitarajiwa kuhamishia gharama hizo kwa wateja. Dizeli ni muhimu katika kuendesha uchumi wa Kenya kwa kuwa hutumika katika magari ya uchukuzi wa umma, mitambo ya kilimo na viwanda.
Wakati huo huo, mfumuko wa bei ulifikia asilimia 6.8 mwezi uliopita, kiwango cha juu zaidi tangu Januari 2024, wakati ulipokuwa asilimia 6.9.
Serikali pia imeonya kuwa hazina ya ruzuku ya mafuta imekuwa ikipungua kwa kasi kutokana na gharama kubwa ya kudhibiti bei.
Ruzuku hiyo hugharimiwa kupitia Ushuru wa Ustawi wa Petroli, unaotozwa kwa bidhaa za mafuta.
Hali hii inazua wasiwasi kuwa Wakenya huenda wakakabiliwa na ongezeko zaidi la bei za bidhaa muhimu na huduma katika siku zijazo
Kazeni mshipi: Bei za mafuta zaongezeka tena

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…