WIZARA ya Afya imethibitisha kisa cha pili cha Ebola, virusi aina ya Bundibugyo, na kufikisha idadi ya jumla nchini kuwa visa viwili na kifo cha mtu mmoja.
Taarifa kutoka kwa Wizara ya Afya iliyofikia Taifa Leo jana ilisema kuwa kisa cha pili kinahusu mwanamume mwenye umri wa miaka 39 ambaye ni jamaa wa karibu wa mgonjwa wa kwanza aliyeaga dunia kutokana na gonjwa hilo wiki iliyopita.
Mwanamume huyo aliyekuwa katika karantini ya lazima kwa muda wa siku 21, alipatikana na virusi hivyo kupitia vipimo baada ya kukumbwa na maumivu ya viungo, uchovu na homa, ilisema taarifa hiyo.
“Kenya sasa imerekodi visa viwili vilivyothibitishwa na kifo kimoja,” alisema Mkurugenzi wa Afya Patrick Amoth.
Alisema kuwa mgonjwa huyo sasa amelazwa katika kituo maalum ambapo anahudumiwa na timu ya wahudumu wa afya waliopokea mafunzo chini ya masharti makali ya kuzuia virusi hivyo kusambaa.
Alisisitiza, hata hivyo, kuwa ingawa visa viwili vilivyothibitishwa vinahusiana, gonjwa la Ebola halijasambaa kwa sehemu kubwa ya wanajamii.
“Visa hivyo viwili vinahusiana na hakuna ushahidi wa kusambaa kwa jamii pana,” alisema Dkt Amoth.
Kulingana na Dkt Amoth, Wizara ya Afya imepata watu 113 miongoni mwa 128 waliotagusana na mgonjwa wa kwanza, ambapo 108 wamewekwa karantini ili kuangaziwa.
Kenya ilitangaza kisa chake cha kwanza kilichoripotiwa na Waziri wa Afya Aden Duale kilichohusu raia wa Kenya aliyeishi katika Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo (DRC) kwa miaka saba.
Alianza kuugua kwa karibu mwezi mmoja, akatibiwa katika vituo mbalimbali DRC, kabla ya kusafiri kupitia barabara hadi Kampala, Uganda na mwishowe kuwasili jijini Nairobi, Jumamosi Oktoba 3.
Aliaga dunia katika hospitali ya Nairobi Hospital ambapo vipimo katika maabara ya kitaifa na Kemri vilionyesha aliugua virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo.
Hofu kisa cha pili cha Ebola kikiripotiwa nchini

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…