SERIKALI imepunguza bei ya petroli na mafuta taa kwa kima cha Sh1 pekee huku bei ya dizeli ikasalia ilivyokuwa kuanzia Julai 15, 2025, hatua ambayo haitoi afueni yoyote kwa raia.
Kwa hivyo, kulingana na bei hiyo mpya iliyotangazwa Alhamisi, Agosti 14, 2025, na Mamlaka ya Kusimamia Sekta ya Kawi na Mafuta (EPRA), petroli, dizeli na mafuta taa zitauzwa kwa bei ya rejareja ya Sh185.31, Sh171.58 na Sh155.58 kwa lita, mtawalia, jijini Nairobi kuanzia Agosti 15 hadi Septemba 14, 2025.
Kuanzia Julai 15 hadi Agosti 14, 2025, wateja jijini Nairobi wamekuwa wakiuziwa petroli, dizeli na mafuta taa kwa Sh184.31, 171.58 na 155.58, mtawalia.
Hii ni baada ya Epra, mnamo Julai 14, 2025, kuongeza bei ya kwa kiwango cha juu cha Sh8.99 kwa petroli, Sh8.67 kwa dizeli na Sh9.65 kwa lita kwa mafuta taa.
Mamlaka hiyo ilisema kuwa ongezeko hilo la bei ya mafuta lilichangiwa na kuongezeka kwa bei ya mafuta katika masoko ya kimataifa kutokana na vita kati ya Iran na Israel.
Kulingana na Epra, ilipunguza bei ya petroli Alhamisi kufuatia kushuka kwa bei ya bidhaa hii inayoingizwa kutoka ng’ambo kwa kima cha asilimia 1.06 “kutoka dola 716.03 (Sh93,083.9) kwa lita 1000 mnamo Juni 2025 hadi dola 708.47 (Sh92,101.1) mnamo Julai 2025 kwa lita 1000."
“Kwa upande mwingine, bei ya dizeli ilipanda kwa kima cha asilimia 1.52 kutoka dola 682.73 (Sh88,754.9) hadi dola 693.82 (Sh90,196.6) kwa lita 1000 huku bei ya mafuta taa ikipanda kwa kima cha asilimia 1.87 kutoka dola 692.80 (Sh90,064) hadi dola 705.74 (Sh91,746.2) kwa lita 1000,” ikaeleza Epra.
Bei ya mafuta huathiri hali ya uchumi pakubwa husasan gharama ya uchukuzi na uzalishaji bidhaa viwandani. Sababu ni kwamba magari na mashine hutumia ama petroli au dizeli.
Aidha, mitambo ya uzalishaji wa kawi ya stima hutumia dizeli.
Hamna afueni ya maana Epra ikipunguza bei ya petroli kwa Sh1 tu
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
BusinessHofu ya wagonjwa wa saratani kukosa matibabu kufuatia mabadiliko ya SHA
WAGONJWA wa saratani nchini wameibua wasiwasi kuhusu kucheleweshwa kwa matibabu, kukataliwa kwa maombi ya dawa na kupunguzwa kwa kiwango cha fedha wanacholipiwa na Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA). Wanasema mfumo mpya wa kuidhinisha matibabu umewalazimu kulipa fedha za ziada ili kupata huduma ambazo awali ziligharamiwa kikamilifu na bima ya afya. Katika Hospitali ya Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga (JOOTRH), kati ya maombi 30 ya matibabu yaliyowasilishwa kwa SHA Jumatatu, ni 12 pekee yaliidhinishwa. Daktari mmoja mtaalamu wa saratani alisema hata wagonjwa walioidhinishwa walitakiwa kuongeza fedha kutoka mifukoni mwao. Alitaja mgonjwa wa saratani ya utumbo aliyelazimika kulipa Sh20,000 kwa vipimo, licha ya kuwa awali gharama hizo zililipwa na SHA. Daktari alisema hali hiyo imacha wagonjwa wasiojiweza kifedha wakisimamisha matibabu kwa kukosa pesa za kuongeza. Mgonjwa mmoja wa saratani ya matiti alisema kiwango chake cha fedha za kununua dawa ya Letrozole kimepunguzwa hadi Sh5,400, ilhali anahitaji zaidi ya Sh20,000 kwa dawa hiyo inayosaidia kudhibiti ukuaji wa saratani inayochochewa na homoni. “Ninahitaji zaidi ya Sh20,000 kununua dawa zangu. Kiasi hicho kinapopunguzwa nalazimika kuongeza fedha za ziada. Bila dawa hizo huenda nishindwe kudhibiti homoni,” akaeleza. Mfumo huo mpya pia umeongeza muda wa kusubiri dawa hospitalini. Maombi ya matibabu sasa yanahitaji kupitishwa na muuguzi, daktari mtaalamu na mfamasia kabla ya kuidhinishwa. Muuguzi katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta alisema foleni katika kliniki za saratani zinaongezeka huku wagonjwa wakingoja vibali. Mgonjwa Mary Adhiambo pia alisema kituo cha saratani cha Texas kimeacha kuuza dawa kwa wagonjwa wanaopokea matibabu katika hospitali zingine, na badala yake kuwataka wahamie huko. Mabadiliko hayo yameathiri wagonjwa wanaotibiwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta na Hospitali ya Mafunzo, Rufaa na Utafiti ya Chuo Kikuu cha Kenyatta (KUTRRH), ambao awali walinunua baadhi ya dawa katika vituo vingine. Mkur
BusinessAnthropic sets IPO price at $83 per share, targets $1.5trn valuation
–Claude maker raises $81.3bn in world’s largest IPO, overtakes SpaceX as investors rush for AI, despite $104bn lossBy Vera Anyagafu, with agency report The artificial intelligence race just produced the biggest stock market debut in history. Anthropic, the United States artificial intelligence company behind the Claude chatbot, on Wednesday priced its initial public offering at […]
BusinessOyedele urges banks to prioritise agricultural lending
…Commissions Moniepoint Abuja branch By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The Minister of Finance and Coordinating Minister of the Economy, Taiwo Oyedele, has urged banks and other financial institutions to make loans more affordable and accessible to businesses, particularly those operating in the agricultural sector, to stimulate productivity and economic growth. Oyedele made the call […]
BusinessNasarawa attracts $2.3bn investments in seven years — Abdullahi
Records 21 reforms, 11 PPP projects worth ₦93bn By John Alechenu ABUJA — Nasarawa State has attracted more than $2.3 billion in investments over the past seven years following reforms and institutional development aimed at making the state more competitive and investor-friendly. The Managing Director and Chief Executive Officer of the Nasarawa Investment and Development […]