WAKENYA wengi wamegeukia kula matumbo kama kitoweo kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha.
Hii ni kinaya kwani kwa muda mrefu nyama hiyo imekuwa ikichukuliwa kuwa ya watu wa kipato cha chini.
Kulingana na Shirika la Kitaifa la Takwimu Kenya (KNBS), bei ya matumbo imepanda kwa karibu asilimia 34 katika kipindi cha miaka minne iliyopita, kutoka Sh260.46 kwa kilo mwaka wa 2020 hadi Sh344.92 mwaka wa 2024 kuashiria ongezeko kubwa la mahitaji.
Kile ambacho hapo awali kilionekana kama bidhaa ya ziada isiyo na thamani sasa kimekuwa mbadala wa nyama kwa familia nyingi zinazopambana kumudu gharama ya maisha.
“Nilipoanza, matumbo hayakuwa maarufu hivi,' anasema.
"Sasa, nauza matumbo zaidi kuliko nyama ya kawaida. Watu hawawezi tena kumudu nyama ya ng’ombe," asema Bw Charles Wamugunda, muuzji bucha jijini Nairobi ambaye amekuwa kwenye biashara hiyo kwa zaidi ya miaka 10.
Bw Wamugunda hupata matumbo kutoka vichinjio vya Kiserian na Dagoretti na anakiri kuwa hata bei ya jumla imepanda.
“Bei inapopanda kule vichinjioni, sisi pia tunalazimika kuongeza. Kisha kuna ushuru ambao zamani hatukuwa tunalipa. Hii inaathiri faida,” anasema.
Anaongeza, “Mazingira ya biashara pia yamebadilika, na ushuru wa ziada unapunguza kiwango cha faida. Kuna ushuru ambao siku hizi tunalazimika kulipa, tofauti na zamani.”
Anasema wanaopendelea matumbo wameongezeka tofauti na zamani ambapo yalikuwa ya kawaida katika familia maskini.
Katikati mwa jiji la Nairobi, Bw Dancan Kamau pia anashikilia maoni sawa na hayo.
'Miaka kumi iliyopita, nilikuwa ninauza matumbo kwa Sh150 kwa kilo. Leo hii, bei imeongezeka mara mbili,' anasema. 'Wateja wamehama kutoka nyama ya ng’ombe hadi matumbo. Ni nafuu na rahisi kupika.'
Ingawa Bw Kamau hupata matumbo kutoka kwa mifugo wake mwenyewe, anasema faida imekuwa ndogo.
“Gharama zimepanda kote, malisho hadi mishahara ya wafanyakazi. Hakuna faida kama zamani.” Hata hivyo, mahitaji ni makubwa. Katika siku nzuri, Bw Kamau huuza kati ya kilo 80 hadi 100 za matumbo.
“Kwa mfano, kama baba alikuwa akinunua nyama ya ng’ombe kwa familia yake na sasa anapitia hali ngumu kifedha, atapendelea kubeba matumbo akirudi nyumbani kuliko kufika mikono mitupu. Wale waliokuwa wananunua nyama sasa wamehamia matumbo. Wakati wa hali ngumu, watu hubadilisha mambo,' aliongeza.
Katika Kampuni Kenya Meat Commission (KMC), Meneja wa Mauzo na Masoko, Bi Lydia Mandila, alithibitisha kuhusu ongezeko la mahitaji.
'Tumeona ongezeko kubwa la mauzo ya matumbo, hasa katika maeneo ya watu wa kipato cha chini na cha kati,' anasema.
"Ni nafuu na yana virutubisho."
Bi Mandila anasema kuwa ingawa nyama ya ng’ombe bado ni bidhaa kuu ya KMC, matumbo yamekuwa bidhaa ya pili yenye faida ijapokuwa upatikanaji wake unategemea idadi ya ng’ombe wanaochinjwa.
'Katika kila kilo 130 za nyama ya ng’ombe, unapata takriban kilo 13 za matumbo,' anasema. 'Kwa hiyo kadri tunavyoongeza uchinjaji, ndivyo tunavyoweza kutoa matumbo zaidi.'
Hata hivyo, anasema kuna msimu ambapo mauzo ya matumbo hupungua, hasa wakati wa sherehe ambapo watu hupendelea vipande bora vya nyama.
'Lakini kwa ujumla, tumerekodi mauzo na faida kubwa katika kipengele hicho. Hata tunafanya usambazaji unaolengwa, wakati mwingine hadi mitaa na maeneo ya kipato cha chini ili kufikia mahitaji,' aliambia Taifa Leo.
"Kila mtu anakimbilia huko kwa sababu soko la Burma si kama zamani,' anasema.
Hali ngumu ya uchumi yalazimu Wakenya zaidi kula matumbo badala ya nyama
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
BusinessHofu ya wagonjwa wa saratani kukosa matibabu kufuatia mabadiliko ya SHA
WAGONJWA wa saratani nchini wameibua wasiwasi kuhusu kucheleweshwa kwa matibabu, kukataliwa kwa maombi ya dawa na kupunguzwa kwa kiwango cha fedha wanacholipiwa na Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA). Wanasema mfumo mpya wa kuidhinisha matibabu umewalazimu kulipa fedha za ziada ili kupata huduma ambazo awali ziligharamiwa kikamilifu na bima ya afya. Katika Hospitali ya Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga (JOOTRH), kati ya maombi 30 ya matibabu yaliyowasilishwa kwa SHA Jumatatu, ni 12 pekee yaliidhinishwa. Daktari mmoja mtaalamu wa saratani alisema hata wagonjwa walioidhinishwa walitakiwa kuongeza fedha kutoka mifukoni mwao. Alitaja mgonjwa wa saratani ya utumbo aliyelazimika kulipa Sh20,000 kwa vipimo, licha ya kuwa awali gharama hizo zililipwa na SHA. Daktari alisema hali hiyo imacha wagonjwa wasiojiweza kifedha wakisimamisha matibabu kwa kukosa pesa za kuongeza. Mgonjwa mmoja wa saratani ya matiti alisema kiwango chake cha fedha za kununua dawa ya Letrozole kimepunguzwa hadi Sh5,400, ilhali anahitaji zaidi ya Sh20,000 kwa dawa hiyo inayosaidia kudhibiti ukuaji wa saratani inayochochewa na homoni. “Ninahitaji zaidi ya Sh20,000 kununua dawa zangu. Kiasi hicho kinapopunguzwa nalazimika kuongeza fedha za ziada. Bila dawa hizo huenda nishindwe kudhibiti homoni,” akaeleza. Mfumo huo mpya pia umeongeza muda wa kusubiri dawa hospitalini. Maombi ya matibabu sasa yanahitaji kupitishwa na muuguzi, daktari mtaalamu na mfamasia kabla ya kuidhinishwa. Muuguzi katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta alisema foleni katika kliniki za saratani zinaongezeka huku wagonjwa wakingoja vibali. Mgonjwa Mary Adhiambo pia alisema kituo cha saratani cha Texas kimeacha kuuza dawa kwa wagonjwa wanaopokea matibabu katika hospitali zingine, na badala yake kuwataka wahamie huko. Mabadiliko hayo yameathiri wagonjwa wanaotibiwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta na Hospitali ya Mafunzo, Rufaa na Utafiti ya Chuo Kikuu cha Kenyatta (KUTRRH), ambao awali walinunua baadhi ya dawa katika vituo vingine. Mkur
BusinessAnthropic sets IPO price at $83 per share, targets $1.5trn valuation
–Claude maker raises $81.3bn in world’s largest IPO, overtakes SpaceX as investors rush for AI, despite $104bn lossBy Vera Anyagafu, with agency report The artificial intelligence race just produced the biggest stock market debut in history. Anthropic, the United States artificial intelligence company behind the Claude chatbot, on Wednesday priced its initial public offering at […]
BusinessOyedele urges banks to prioritise agricultural lending
…Commissions Moniepoint Abuja branch By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The Minister of Finance and Coordinating Minister of the Economy, Taiwo Oyedele, has urged banks and other financial institutions to make loans more affordable and accessible to businesses, particularly those operating in the agricultural sector, to stimulate productivity and economic growth. Oyedele made the call […]
BusinessNasarawa attracts $2.3bn investments in seven years — Abdullahi
Records 21 reforms, 11 PPP projects worth ₦93bn By John Alechenu ABUJA — Nasarawa State has attracted more than $2.3 billion in investments over the past seven years following reforms and institutional development aimed at making the state more competitive and investor-friendly. The Managing Director and Chief Executive Officer of the Nasarawa Investment and Development […]