Video
DC TANGA AZINDUA MRADI WA KUPINGA UKATILI NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA
Channel: Millard Ayo Watch on YouTube
Related stories
NewsMpango wa TSC kutoa vyeti kwa walimu vya kuendelea kufundisha wazua hisia mseto
PENDEKEZO la Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) kuanza kutoa vyeti maalumu kuruhusu walimu kuendelea kufundisha limezua mjadala mkali, huku wadau wa elimu wakitofautiana kuhusu mamlaka ya tume hiyo kusimamia ajira na pia kudhibiti taaluma ya ualimu. Pendekezo hilo limo katika Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya TSC wa 2026, unaolenga kufanya mafunzo ya mara kwa mara ya kuwaongezea walimu ujuzi kuwa ya lazima. Walimu watakaokosa kushiriki mafunzo hayo wanaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Hata hivyo, wadau wanatofautiana kuhusu mpango huo. Baadhi wanataka kuundwa kwa chombo huru kitakachosimamia mafunzo na utoaji wa vyeti vya kitaaluma, huku wengine wakitaka serikali ihakikishe walimu hawalazimishwi kulipia mafunzo hayo. Kifungu cha 28 cha mswada huo kinapendekeza kubadilishwa kwa Kifungu cha 35 cha Sheria ya TSC ili kuipa tume jukumu la kuhakikisha walimu wote wanazingatia viwango vya taaluma ya ualimu.Mswada huo unapendekeza tume iwalazimishe walimu wote waliosajiliwa kushiriki mafunzo ya kuendeleza ujuzi wao na kisha kuwapa vyeti vya kuwaruhusu kuendelea kufundisha. Mwalimu atakayekosa kutimiza masharti hayo atakabiliwa na hatua za kiutawala zitakazofafanuliwa katika kanuni.Pendekezo hilo lina maana kwamba hata walimu ambao wamesajiliwa na TSC na wamehudumu kwa miaka mingi watalazimika kutimiza masharti mapya ili kupata vyeti hivyo.Ingawa usajili wa TSC unatambua mwalimu kuwa amekidhi masharti ya kujiunga na taaluma, cheti kipya kitategemea ushiriki wake katika mafunzo ya mara kwa mara. Hata hivyo, mswada haujaeleza vyeti hivyo vitakuwa halali kwa muda gani, vitafanywa upya baada ya kipindi gani, au kama walimu watalazimika kuvilipia. Pia haujaweka wazi muda wa mafunzo hayo wala atakayeyagharamia. Chama cha Wadau wa Elimu nchini kimepinga pendekezo hilo, kikisema TSC haipaswi kuwa mwajiri na wakati huo huo kuwa msimamizi wa leseni za taaluma.Katibu Mkuu wa kitaifa wa chama hicho, Ndung’u Wangenye, alisema Bunge linapaswa kupitisha sheria ya kuunda chombo huru kitakach
NewsZimbabwean president surprised Kenya's Defence minister is female: "Defence?"
Zimbabwe's Emmerson Mnangagwa appeared surprised after Ruto introduced him to Kenya's female Defence CS Soipan Tuya during a State House meeting.
NewsIEBC yahitaji Sh10bn kununua vifaa vipya vya uchaguzi 2027
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) huenda ikalazimika kununua vifaa vipya vya teknolojia ya uchaguzi kila baada ya miaka mitano, hali inayoweza kuongeza mzigo wa matumizi kwa walipa ushuru. Naibu mwenyekiti wa IEBC Fahima Abdalla aliambia Kamati ya Haki na Masuala ya Sheria ya Bunge la Kitaifa kuwa ukaguzi wa kiufundi uliofanywa na Mamlaka ya ICT (ICTA) ulibaini kuwa vifaa vya usimamizi za uchaguzi Kenya (Kiems) vilivyonunuliwa mwaka 2021 kwa uchaguzi wa 2022 vimefikia mwisho wa muda wake wa matumizi. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, vifaa 15,000 vilivyonunuliwa wakati huo haviwezi kutegemewa katika uchaguzi mkuu wa 2027. Hali hii ina maana kuwa IEBC italazimika kutafuta angalau Sh10 bilioni kununua vifaa vipya 60,000 ili kuendesha uchaguzi ujao. “Wataalamu wa Mamlaka ya ICT walikuja kukagua vifaa vya Kiems na kutuambia kuwa teknolojia hiyo ina muda wa matumizi wa miaka mitano. Walitueleza kuwa vifaa hivyo havitafanya kazi ipasavyo katika uchaguzi mkuu wa 2027,” alisema Bi Abdalla. Kauli yake ilijiri baada ya Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo kutaka kujua ni vifaa vingapi vilivyonunuliwa kwa uchaguzi wa 2022 ambavyo vinaweza kutumika tena mwaka 2027. Hata hivyo, uamuzi huo unazua wasiwasi kuhusu matumizi ya mabilioni ya fedha za umma kila baada ya miaka mitano, huku serikali ikikabiliwa na mahitaji mengine kama afya, miundombinu na malimbikizo ya madeni. IEBC pia inakabiliwa na changamoto ya jinsi ya kutupa vifaa vya zamani. Hapo awali, tume hiyo ilipendekeza kuvifuta taarifa na kuvitoa kwa shule au taasisi nyingine za serikali. Hata hivyo, vifaa hivyo vina teknolojia maalumu za utambuzi wa wapigakura na baadhi ya taarifa zake huhitajika kuhifadhiwa kama ushahidi iwapo kutakuwa na kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi. Mtaalamu wa utawala bora Barasa Nyukuri alisema kununua vifaa vipya kila baada ya miaka mitano kunaweza kuilazimisha IEBC kufanya ununuzi kwa haraka, hali inayoweza kuongeza gharama na kuzua migogoro ya zabuni. Mwanasheria na mtaalamu wa uchaguzi David Och
NewsMuthama Martin Njenga: Kenyan Man in US Shoots Wife Dead, Surrenders to the Police
A Kenyan man surrendered after allegedly killing his wife in Oakley on Thanksgiving; his wounded 16-year-old stepdaughter rescued two young children from the home.