SERIKALI ya Amerika imekumbusha raia wake nchini Kenya kuwa waangalifu ikisema kunaweza kutokea mashambulizi ya kigaidi.
Mwezi wa Septemba, unasema Ubalozi wa Amerika nchini Kenya, ni mwezi wa kumbukumbu za mashambulizi makubwa ya kigaidi, ikiwa ni pamoja na shambulio la 9/11 nchini Amerika na shambulio la Septemba 21, 2013 katika jumba la kibiashara la Westgate jijini Nairobi.
Watu 2,977 walikufa katika shambulio la Amerika, huku 67 wakipoteza maisha katika shambulio la Westgate, Nairobi.
"Ingawa mashambulizi yanaweza kutokea wakati wowote, wasiwasi unaongezeka karibu na tarehe za kumbukumbu za mashambulizi ya awali ya kigaidi, kama vile Septemba 11, shambulio la Septemba 21 la Westgate," ubalozi ulisema katika ushauri uliotoa Septemba 13, 2024.
Vile vile, ubalozi unasema, kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa shambulio la Hamas nchini Israeli (Oktoba 7, 2023) inakaribia.
“Ubalozi wa Amerika mjini Nairobi unawakumbusha raia wa Amerika nchini Kenya kwamba wanapaswa kuwa waangalifu zaidi kutokana na hatari za ugaidi na utekaji nyara. Maeneo yanayotembelewa na raia wa Amerika na watalii jijini Nairobi na kwingineko nchini Kenya yanaweza kulengwa na magaidi,” ulisema ushauri wa ubalozi.
Ubalozi huo unashauri raia wa Amerika kuendelea kuwa macho katika maeneo yanayotembelewa na watalii, kutathmini mipango yao ya kibinafsi ya usalama, kufuatilia vyombo vya habari vya humu nchini, kuepuka maeneo ambayo maandamano yanafanyika na kuepuka mikusanyiko ya watu.
Ubalozi wa Uingereza nchini Kenya ulisisitiza ushauri wa Ubalozi wa Amerika.
Amerika yakumbusha raia wake Kenya Septemba ni mwezi wa mikosi ya mashambulizi
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
Travel
TravelTANAPA calls for active investment to promote tourism in Lake Zone
GEITA: THE Tanzania National Parks Authority (TANAPA) has called on development stakeholders in the Lake Zone, including mineral miners, to seize investment opportunities in the tourism sector. TANAPA Head of Business Development Unit, Ms Jully Bede Lyimo, made the call recently during a special meeting between TANAPA and development stakeholders held in Geita Municipality. She…
TravelShivo Tanzania’s Richard Ashby elected to ZATI board of directors
ZANZIBAR: Richard Ashby of Shivo Tanzania has been elected to the Board of Directors of the Zanzibar Association of Tourism Investors (ZATI), following the association’s Annual General Meeting (AGM) and board elections held in Zanzibar on Wednesday. Ashby secured 47 votes in a competitive contest involving 10 candidates, earning one of four positions on the…
TravelUnited Nigeria Airlines begins Jos flights to Lagos, Kano, Owerri
United Nigeria Airlines will commence scheduled flight operations from Jos to Lagos, Kano and Owerri on November 24 and 29, 2026, providing residents of Plateau State with additional air connections to other parts of the country. The airline said tickets for the new routes were already available for purchase. The Lagos–Jos–Lagos route will operate four […]