WANASIASA kutoka mirengo tofauti sasa wako katika kinyang’anyiro cha kutumia jina, ushawishi na urithi wa kisiasa wa aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Raila Odinga kuvutia ufuasi huku uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027 ukijongea.
Rais William Ruto, Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, Dkt Fred Matiang’i, Martha Karua, Eugene Wamalwa, Kalonzo Musyoka na hata Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa viongozi wanaotumia kumbukumbu ya Raila kujijenga kisiasa tangu kifo chake Oktoba 15, 2025.
Katika maeneo mengi nchini hasa Nyanza ambako Raila alikuwa na wafuasi waaminifu, jina lake limekuwa likitumika kusaka uungwaji mkono kisiasa.
Rais Ruto amekuwa akiwakumbusha wakazi wa eneo hilo kuhusu ushirikiano wake wa zamani na Raila, akitaja walivyokuwa pamoja katika kundi la ODM - Pentagon- mnamo 2007 na baadaye wakaunda serikali ya ‘Nusu-Mkate’ na marehemu Rais wa tatu Mwai Kibaki.
Wakati wa kufungua makavazi ya Raila katika maziara ya Kang’o ka Jaramogi, Bondo, mnamo Oktoba 7, Rais Ruto alisema muundo wa kaburi hilo la pande tano unaashiria umoja wa kundi la Pentagon.
“Nilikuwa na bahati ya kuketi kwenye meza hiyo pamoja naye. Nilijionea jinsi Jakom alivyokuwa akijenga mahusiano kati ya jamii na watu,” akasema.
Rais pia amehusisha miradi yake ya maendeleo na urithi wa Raila, akisema kila barabara inayojengwa katika maeneo yaliyosahaulika ni heshima kwa marehemu jagina huyo.
Kwa upande mwingine, Bw Sifuna, aliyekuwa katibu mkuu wa ODM kwa miaka minane, amekuwa akijitambulisha kama mwanafunzi wa kisiasa wa Raila kupitia mikutano ya Linda Mwananchi.
Wakati wa mazishi ya Raila mnamo Oktoba 19, 2025, alisema kumtumikia kama katibu mkuu kwa miaka minane ilikuwa heshima kubwa maishani mwake.
Katika mikutano ya kisiasa, Bw Sifuna amekuwa akisisitiza kuwa atatetea demokrasia, uhuru na utawala wa sheria, akisema hayo ndiyo maadili aliyoachiwa na Raila.
“Baba alituambia tuweke demokrasia, uhuru na kuheshimu utawala wa sheria mbele ya kila kitu,” akasema Bw Sifuna akiwahutubia wafuasi wake Nyandiwa, Sindo na mjini Homa Bay.
“Kwangu mimi kama Sifuna, kujenga barabara na viwanja vya michezo si jambo gumu , lakini ninachowaahidi ni kwamba nitaheshimu utawala wa sheria, nitalinda haki zenu na sitawahi kuua watoto wenu,” akaongeza.
Bw Musyoka naye amekuwa akiwakumbusha wapigakura kuhusu uhusiano wake wa zaidi ya miaka 15 na Raila, akisema alisimama naye licha ya changamoto za kisiasa na za mahakamani.
“Kwa zaidi ya miaka 15 niliyomuunga mkono Raila haiwezi kusahaulika. Ushindi wetu uliibwa na tulikumbana na changamoto mahakamani, lakini nilisimama naye,” akasema Bw Musyoka.
Kiongozi wa DAP-K Eugene Wamalwa naye amekuwa akisema ingawa Raila alifariki, maono na msingi aliosimamia havijapotea. Amekuwa akiwataka Wakenya kulinda uhuru, haki za raia na ugatuzi.
“Njia bora ya kumuenzi Baba ni kulinda kwa dhati uhuru ambao sasa uko hatarini, haki za raia na misingi ya demokrasia aliyopigania,” akasema Bw Wamalwa.
Dkt Matiang’i, anayejipanga kisiasa katika upinzani, amesisitiza umuhimu wa umoja wa viongozi wa Nyanza, akisema Raila aliwachukulia wanasiasa kutoka eneo hilo kama watoto wake.
Kiongozi wa PLP Martha Karua, ambaye amekuwa mshirika na mpinzani wa Raila kwa nyakati tofauti, alimkumbuka kama mtetezi jasiri wa wananchi na mpiganiaji wa demokrasia.
Hata Bw Gachagua, ambaye alikuwa katika upande tofauti wa kisiasa na Raila, alimtaja kama shujaa wa ukombozi wa pili na kusifu uwezo wake wa kujenga ODM kuwa chama imara.
Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino amekuwa akimwelezea Raila kama baba na mshauri wake wa kisiasa.
Pia amemtaka binti wa Raila, Winnie Odinga, kujiunga na Linda Mwananchi, akisema harakati hiyo ni nzuri kuliko mapambano ya makundi ndani ya ODM.
Bw Kenyatta naye amekuwa akitetea uamuzi wake wa kumuunga mkono Raila katika uchaguzi wa 2022, akisema alifanya kila alichoweza kumsaidia kushinda urais.
Hata hivyo, Mahakama ya Juu ilithibitisha ushindi wa Rais Ruto.
“Tulifanya handisheki na hata tukakubaliana kumuunga mkono Raila Odinga. Nilifanya kila nilichoweza kumsaidia Baba kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya,” akasema Bw Kenyatta.
Mchanganuzi wa siasa Geoffrey Mboya anasema kifo cha Raila kilimaliza safari yake binafsi ya kisiasa, lakini hakupunguza thamani ya jina lake.
Anasema wanasiasa wanajitahidi kujihusisha na sehemu tofauti za urithi wake, yakiwemo mapambano ya demokrasia, ugatuzi, ushirikiano wa kisiasa na uungwaji mkono aliokuwa nao Nyanza.
Ushindani huo unaonyesha kuwa jina la Raila limekuwa sehemu muhimu ya mikakati ya wanasiasa wanaotafuta uungwaji mkono kuelekea uchaguzi wa 2027.
‘2027 kwa jina la Baba Raila’

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…