VIONGOZI ambao wametawala siasa za Kenya kwa miongo kadhaa wanakabiliwa na swali gumu huku uchaguzi mkuu wa Agosti 2027 ukikaribia: Je, wako tayari kukabidhi hatamu kwa kizazi kipya au wataendelea kupigania nafasi zao katika uongozi?
Miongoni mwa wanasiasa wanaokabiliwa na mjadala huo ni Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi, Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, Waziri wa Ushirika Wycliffe Oparanya, Martha Karua, kiongozi wa ODM Oburu Oginga, Gavana wa Siaya James Orengo na Seneta wa Kakamega Boni Khalwale.
Wachanganuzi wanasema ingawa viongozi hao bado wana mitandao mikubwa ya kisiasa, uzoefu na ushawishi katika maeneo yao, wanakabiliwa na shinikizo kutoka kwa vijana wanaotaka mabadiliko ya kizazi katika uongozi.“Mjadala si kwamba viongozi hawa wameishiwa na ushawishi wa kisiasa.
Wengi bado wana mitandao, uzoefu serikalini na uwezo wa kujadiliana kuhusu miungano.
Swali ni iwapo mifumo iliyowadumisha madarakani kwa miaka mingi inaweza kustahimili kiu ya mabadiliko ya kizazi,” anasema mchambuzi Geoffrey Mboya.
Mabadiliko hayo yanajitokeza wazi katika eneo la Magharibi mwa Kenya, ambako baadhi ya wanasiasa wakongwe wameunga mkono azma ya Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kuwania urais.
Waliokuwa mawaziri Musikari Kombo, Fred Gumo, Noah Wekesa na Philip Masinde, pamoja na wabunge wa zamani Joash Wamang’oli na Bifwoli Wakoli, wamejitokeza kuunga mkono Sifuna, wakisema eneo hilo linahitaji kuandaa kizazi kipya cha viongozi wa kitaifa.
Hatua hiyo ni ya kipekee kwa sababu ni wanasiasa waliokuwa na ushawishi mkubwa katika maamuzi ya kisiasa ya eneo hilo wanaopendekeza kijana achukue hatamu.
Mzozo kuhusu kizazi pia ulijitokeza katika mkutano wa Sifuna Magharibi, ambapo Naibu Kiongozi wa chama cha Democracy for the Citizens Cleophas Malala alimtaka Seneta Khalwale astaafu pamoja na wenzake na kuachia vijana nafasi.
Kauli hiyo ilizua mzozo mkali.
Hata upinzani unakabiliwa na changamoto hiyo, huku viongozi wakongwe wakijaribu kuafikiana kuhusu atakayepata tiketi ya urais mwaka 2027.
Kalonzo, mwenye umri wa miaka 72, ameongeza shughuli za kisiasa akilenga kupata nafasi nyingine ya kuwania urais.
Alianza safari yake bungeni mwaka 1985 na kuhudumu kama Makamu wa Rais chini ya marehemu Mwai Kibaki.
Hata hivyo, anashinikizwa na baadhi ya wanasiasa vijana wanaosema Kenya inahitaji sura mpya katika kinyang’anyiro cha urais.
Umri wa baadhi ya viongozi hao pia umeongeza uzito wa mjadala. Oburu atakuwa na miaka 83 wakati wa uchaguzi wa 2027 na 88 mwaka 2032.
Orengo atakuwa na miaka 76 na 81 mtawalia, huku Kalonzo akiwa na miaka 73 na 78.
Mudavadi atakuwa na miaka 66 mwaka 2027 na 71 mwaka 2032, huku Wetang’ula akiwa na miaka 70 na 75 mtawalia.
Wakili Chris Omore anasema takwimu hizo hazimaanishi kuwa viongozi hao hawawezi kuendelea na siasa, lakini zinaonyesha muda unaobaki kwa baadhi yao kutimiza malengo makubwa ya kisiasa.
Rais William Ruto pia alichochea mjadala huo aliposema wakati wa ziara yake Gusii Novemba 10 kuwa anatarajia kuondoka katika siasa za moja kwa moja mwaka 2032 pamoja na baadhi ya viongozi wa upinzani, wakiwemo Kalonzo na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua.
Hata hivyo, viongozi hao hawajaonyesha nia ya kuachana na malengo yao.
Orengo tayari ametwaa chama cha Liberal Democratic Party (LDP) ambacho anakitumia kupanga upya mikakati yake ya kisiasa.
Kwa upande mwingine, kizazi kipya kinazidi kujitokeza.
Miongoni mwao ni Sifuna, Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro, Babu Owino wa Embakasi Mashariki, Seneta wa Nyandarua John Methu, Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi na Malala.
Sifuna, mwenye miaka 45 mwaka 2027, amekuwa sura muhimu katika mjadala huo kupitia vuguvugu la Linda Mwananchi.
Nyoro, mwenye miaka 40, amejijengea jina katika masuala ya uchumi, huku Owino akiwa na wafuasi wengi hasa mijini.
Ripoti ya Centre for Multiparty Democracy ya mwaka 2026 inaonyesha vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 wanaunda takriban asilimia 57 ya wapiga kura wanaostahili kupiga kura.
Hata hivyo, Omore anaonya kuwa idadi hiyo haimaanishi moja kwa moja kuwa vijana watawachagua wagombea vijana.
Anasema masuala kama ukosefu wa ajira, ushuru, gharama ya maisha na ufisadi yanaweza kuwa na uzito zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Centre for Multiparty Democracy Frankline Mukwanja anasema wanasiasa vijana wanaozingatia sera na maendeleo wana nafasi nzuri, lakini lazima wajenge miundo yao ya kisiasa na kuonyesha uwezo wa kuhamasisha wananchi bila kutegemea mitandao ya wakongwe.
Wazee katika siasa pabaya kura za 2027 wimbi la vijana likitishia kuwafunika

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsOando’s rising fortunes: How Wale Tinubu is rewriting growth story
By Adebayo Adeoye Jubril Adewale Tinubu, CON, is not one to be easily satisfied with yesterday’s accomplishments. For the Oando Group Chief Executive, every milestone appears to present another opportunity to raise the bar, test new possibilities and push the boundaries of what an indigenous energy company can achieve. That restless ambition is once again […]
News2027: Imperative of Peter Mbah’s second term in Enugu
By Willy Eya Politics apart, Enugu State Governor, Dr Peter Mbah deserves a second term in office. That is not contestable. Certainly, the governor’s achievements since assumption of office in 2023 will campaign for him ahead of the 2027 general elections. One good turn, they say, deserves another. Mbah came in as an accomplished technocrat […]
NewsMakinde’s image on campaign balloon stirs controversy at Tinubu’s Ibadan rally
By Adeola Badru The image of Oyo State Governor, Seyi Makinde, displayed alongside those of President Bola Tinubu and other political figures on a campaign balloon at the All Progressives Congress (APC) rally in Ibadan on Saturday has stirred controversy, raising questions about the governor’s political alignment ahead of the 2027 general elections. The balloon, […]
NewsNigerian politicians preparing for war, not election, by Dele Sobowale
“War is nothing more than the continuation of politics by other means” – Karl von Clausewitz, 1780-1831 The Prussian General and military theorist could not have had Nigeria in mind when he wrote several books on politics and war because Nigeria did not exist then. But, some of his theories, which are still required reading […]