Watu wawili wamethibitishwa kufariki dunia huku wengine sita wakijeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuhusika katika ajali ya barabarani katika eneo la Mghalani kwenye barabara kuu ya Mombasa-Nairobi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Tarafa Ndogo ya Samburu, Lydia Mambo, basi la Dreamline lililokuwa likisafiri kutoka Nairobi kuelekea Mombasa liligonga lori lililokuwa limeegeshwa kando ya barabara kati ya Mackinnon na Taru, Kaunti ya Kwale. Bi Mambo alithibitisha kuwa mmoja wa waliofariki alikuwa abiria aliyekwama ndani ya basi hilo.
"Lori hilo lilikuwa limeharibika barabarani na dereva wake hakuwa ameweka alama zozote za tahadhari, jambo ambalo huenda lilichangia ajali hiyo kulingana na matokeo yetu ya awali ya uchunguzi," alisema.
Maafisa wa polisi walifika haraka eneo la tukio na kuwaokoa abiria, huku majeruhi wakipelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi.
Kwa mujibu wa Bi Mambo, eneo la tukio tayari limeshughulikiwa na magari hayo mawili kuvutwa hadi Kituo cha Polisi cha Taru huku uchunguzi ukianza.
Afisa wa Utekelezaji wa Sheria za Trafiki katika Ukanda wa Pwani, Asha Wario, amewatahadharisha madereva wanaotumia barabara kuu yenye shughuli nyingi ya Mombasa-Nairobi kuwa waangalifu na kuzingatia kikamilifu sheria na kanuni za trafiki.
"Ningependa kuwasihi madereva wawe waangalifu kwa sababu nyingi ya ajali hizi hutokea asubuhi. Hii ina maana kuwa hutokea kutokana na mwonekano hafifu unaosababishwa na manyunyu ya mvua za asubuhi," alisema Bi Wario.
Alisisitiza kuwa madereva watakaopatikana wakikiuka sheria za trafiki watafikishwa mahakamani, akiongeza kuwa juhudi pia zinaendelea za kuelimisha madereva wa mabasi na malori kuhusu usalama barabarani.
Wawili wafariki, sita wajeruhiwa basi likigonga lori Kwale

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]