Video
WANANCHI 350 TABORA WABOMOA MAJENGO KWA HIARI
Channel: ITV Tanzania Watch on YouTube
About this video
#HABARI: Idadi ya nyumba, vibanda vya biashara na majengo ya uwekezaji yanayopaswa kubomolewa bila fidia kutokana na kujengwa ndani ya hifadhi za barabara mkoani Tabora imeongezeka kutoka 567 hadi kufikia 1,136, ambapo wananchi zaidi ya 350 tayari wamevunja majengo yao kwa hiari kabla ya kuanza kwa zoezi la ubomoaji wa lazima. Hata hivyo, baadhi ya wamiliki wakiwemo wakazi wa pembezoni mwa Barabara ya Sikonge katika eneo la Tabora Mjini kama Mzee Hussein Hissa na Bahati Hussein wameendelea kupinga hatua hiyo wakidai kuwa makazi yao yalikuwepo kabla na yamekutwa na barabara. Kwa upande wao, wamiliki waliotii sheria akiwemo Abdallah Chota wameshaanza kuvunja nyumba zao huku maeneo mengine yakisubiri hatua za kisheria. Wakala ya Barabara Kuu Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Tabora ikiongozwa na Meneja wa Mkoa Mhandisi Raphael Mlimaji pamoja na Fundi Sanifu Advera Sinzya wamekagua maeneo hayo na kutoa taarifa ya hali ya sasa ya zoezi la ubomoaji pamoja na msimamo wa serikali. RADIO ZETU KWENYE VING’AMUZI: Radio One: Azam 061, Digitek 110, Capital Radio: Azam 383, Digitek 112, Powered by #MCHEZOSUPA JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA: - Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Mix by Yas, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV. #ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania Follow @itvtz @radioonetanzania @itv2tanzania
Related stories
General10 countries where visa overstay can attract severe penalties
Travellers who remain in a foreign country after their authorised period of stay has expired risk facing serious immigration consequences, including heavy fines, detention, deportation and restrictions on returning.
GeneralUganda: Wife unmoved after husband falls from chair until children come to his rescue
A doorbell camera captured a man falling from a swivel chair as his wife continued sweeping unbothered, until his children came over to help him get up.
GeneralKAPOMBE ATIA NENO KABLA YA KUIVAA ORLANDO PIRATES
General