UONGEZAJI thamani maziwa ni shughuli ambayo inaweza kumletea mkulima mapato zaidi.
Hii ni kwa sababu bidhaa zilizoongezewa thamani huuzwa kwa bei za juu, ikilinganishwa na kuyauza maziwa ya kawaida.
Mmojawapo wa wale wanaochuma kutokana na uongezaji thamani kwa maziwa ni Margaret Njoki, ambaye alijitosa katika shughuli ya hiyo miaka saba iliyopita, wakati huo, akihudumu katika kampuni moja mjini Naivasha.
Hata hivyo, alikuwa akiyauza maziwa tu mnamo mwaka 2015.
Baada ya kugundua kuwa wateja wengi walikuwa wakihitaji maziwa gururu (yoghurt), akaamua kuzitengeneza pamoja na bidhaa nyinginezo za maziwa; mathalani jibini, siagi na kadhalika.
Kwa sasa, Njoki huongeza thamani maziwa na kupakia katika plastiki na kusambaza kwa wateja wake.
Aidha, huuza kwa dukakuu moja.
“Kandarasi yangu kazini ilipoisha 2016, nilikuwa na uhakika kuwa sitaki kuajiriwa tena. Nikahama ili kuendeleza uzalishaji katika eneo la Kabati. Mnamo 2017, nikapoteza gururu kutokana na uharibifu,” asema Njoki.
[caption id="attachment_181981" align="alignnone" width="1920"] Margaret Njoki aonyesha bidhaa zake katika eneo la Ngara, Nairobi. PICHA|PETER CHANGTOEK[/caption]
Kuharibika kwa bidhaa zake kulimshurutisha kufunga shughuli ya utengenezaji, baada ya kupoteza bidhaa zilizokuwa na thamani ya Sh400,000.
Kilichoonekana kama kutia chumvi kwenye kidonda, wafanyakazi wake wakamwibia bidhaa zilizokuwa zimebaki.
Kabla ya hasara hiyo, alikuwa akizitengeneza bidhaa kutoka kwa maziwa lita 700 kila siku na alikuwa akiziuza kwa muda wa siku mbili.
Hata hivyo, alifungua upya tena 2018. Mambo yakaenda segemnege tena mwaka 2021, baada ya bidhaa zake kuharibika na kupata hasara ya takribani Sh600,000 na kulazimika kufunga biashara tena.
Licha ya changamoto, mwaka uliopita akaanza kuzitengeneza bidhaa kutoka kwa maziwa tena.
Njoki anafichua kuwa, amekuwa akiyanunua maziwa kutoka kwa mkulima mmoja tangu 2016.
Huchakata maziwa lita 200 kila siku, anayoyanunua kwa Sh55 kwa lita.
“Nina wafanyakazi saba; watatu hapa na wanne kule Kabati,” asema Njoki, ambaye hutengeneza bidhaa nyingine katika eneo la Kabati, Kaunti ya Murang’a, na kadhaa katika eneo la Ngara, aliko na duka analouzia bidhaa zake.
Hutumia brandi ya Tahraji kwa bidhaa zake, na kampuni yake hujulikana kama Crystal Creamery Limited.
Hutengeneza bidhaa kuanzia 150ml hadi lita 5.
“Bidhaa yetu kuu ni gururu; tuna Tarahji Cultured Yoghurt. Tuna gururu ilyotiwa ladha ya matunda, aiskrimu, jibini/chizi, siagi na salmi,” afichua, akiongeza kwamba, hutumia stroberi, vanila, karakara, mananasi pamoja na matunda mengine kutengeneza bidhaa zake.
Njoki hununua stroberi kilo moja kwa Sh300 kutoka kwa mkulima mmoja kutoka Nyahururu.
Pia, hununua kilo tano za matunda aina ya ‘blueberry’ kwa Sh1,500, karakara kwa Sh80 kwa kilo na mananasi kwa Sh50-Sh180 kila moja.
[caption id="attachment_181980" align="alignnone" width="1920"] Margaret Njoki aonyesha bidhaa zake katika eneo la Ngara, Nairobi. PICHA|PETER CHANGTOEK[/caption]
“Hupakia gururu kwa 150ml, 250ml, 500ml, lita 1, lita 2, lita 3 na lita 5. Pia, huwa tunauza kwa wingi, kuanzia lita 10 hadi lita 20, kwa wale wanaotaka za kuuza. Huuza gururu 12 za 150ml kwa Sh400, 12 za 250ml kwa Sh600, 6 za 500ml kwa Sh600,” afichua Njoki, anayejulikana kwa jina Mama Milky katika eneo la Ngara.
Yeye pia huwapa mafunzo watu wanaonuia kuanzisha biashara ya kutengeneza bidhaa kutoka kwa maziwa. “Mimi hutoza Sh5,000 kwa kila bidhaa. Pia, huwa na mafunzo mtandaoni ambapo hutoza Sh3,500. Huchukua muda wa saa 2 hadi 3,” aongeza.
Anasema kwamba, mipango yake ya siku za usoni ni kulijenga jina lake katika shughuli ya kuongezea thamani maziwa. Huuza bidhaa zake katika sehemu mbalimbali na huuza kwa dukakuu la Topmart na ameanza kuziuza kwa Jumia.
Uongezaji thamani maziwa unavyompa hela

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
BusinessAnthropic sets IPO price at $83 per share, targets $1.5trn valuation
–Claude maker raises $81.3bn in world’s largest IPO, overtakes SpaceX as investors rush for AI, despite $104bn lossBy Vera Anyagafu, with agency report The artificial intelligence race just produced the biggest stock market debut in history. Anthropic, the United States artificial intelligence company behind the Claude chatbot, on Wednesday priced its initial public offering at […]
BusinessOyedele urges banks to prioritise agricultural lending
…Commissions Moniepoint Abuja branch By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The Minister of Finance and Coordinating Minister of the Economy, Taiwo Oyedele, has urged banks and other financial institutions to make loans more affordable and accessible to businesses, particularly those operating in the agricultural sector, to stimulate productivity and economic growth. Oyedele made the call […]
BusinessNasarawa attracts $2.3bn investments in seven years — Abdullahi
Records 21 reforms, 11 PPP projects worth ₦93bn By John Alechenu ABUJA — Nasarawa State has attracted more than $2.3 billion in investments over the past seven years following reforms and institutional development aimed at making the state more competitive and investor-friendly. The Managing Director and Chief Executive Officer of the Nasarawa Investment and Development […]
BusinessObi pledges massive investment in education, healthcare
By Chimaobi Nwaiwu NNEWI — Presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, has pledged massive investment in education and healthcare, improved electricity supply and an end to kidnapping if elected president in 2027. Obi, who made the pledge on Friday during a visit to Onitsha, Anambra State, also said his proposed administration, […]