Video
'SITAKI NGONJERA' MWIGULU ACHARUKA WANANCHI MALINYI KUCHELEWESHEWA KIVUKO
Channel: ITV Tanzania Watch on YouTube
About this video
Waziri Mkuu Dkt Mwigulu Nchemba amesema haridhishwi na sababu zinazotolewa na viongozi kuhusu ucheleweshaji wa kivuko cha Kikove hadi Mlimba na akataka apewe majibu ya papohapo ni lini kivuko hicho kitafikishwa wilayani humo ili kianze kutoa huduma kwa wananchi. Akizungumza na wananchi wa Malinyi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Toboatobo, wilayani Malinyi, mkoani Morogoro Dkt. Mwigulu amesema haikubaliki wananchi kuendelea kupata shida ya usafiri wakati fedha za Serikali zimeshalipwa kwa ajili ya kivuko hicho. Waziri Mkuu amesema mradi wa kivuko cha Kikove umedumu kwa karibu miaka tisa, na akataka majibu ya uhakika kuhusu lini kivuko hicho kitafikishwa Mlimba. “Mheshimiwa Naibu Waziri sijaridhika na maelezo yako kuhusu hiki kivuko. Hebu mpigie simu mtendaji wa TEMESA na umuweke kwenye kipazasauti ili wananchi wasikie ni lini hasa kivuko hiki kitafika hapa Malinyi.” “Mmesema kivuko kimekamilika. Na sasa kama kimekamilika kinafanya nini huko? Nataka kujua kinakuja lini. Mimi sitaki ngonjera ngonjera. Miaka tisa hatuwezi tukaelezea jambo kwa wiki moja tena. Fedha ilishalipwa. Kivuko kimekaa muda mrefu. Wananchi hawa wanapata shida,” amesema. Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : bit.ly/itvtanzania Facebook : bit.ly/2KeQNl3 Twitter : bit.ly/2XG7aii Instagram : bit.ly/34KItmg
Related stories
GeneralKUMEKUCHA: NOVEMBA 25, 2026
Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania
GeneralPAMBULA WA CHADEMA AENDELEA KUSOTA KAMA LISSU
PAMBULA WA CHADEMA AENDELEA KUSOTA KAMA LISSU😳 #breaking #shorts #chadema
GeneralDIAMOND AKOSHWA NA SAA YA BABA LEVO
GeneralOsun man tortures 21-yr-old son to death over N75,000, phone
“During the interrogation, the man said his son stole N75,000 and absconded with one android phone he bought for him on 'easy-buy'"