DAR ES SALAAM: Wanafunzi wanaosomea fani ya ukarimu katika Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) sasa watapata mafunzo ya ziada ya miezi mitatu kutoka kwa watalaamu wa Serengeti Breweries Limited (SBL) huku kampuni hii ikilenga kusaidia kujenga kizazi kipya cha wataalamu wa sekta ya utalii na ukarimu inayokua kwa kasi nchini Tanzania.
Kupitia makubaliano yaliyosainiwa Septemba baina NCT na SBL, kundi la kwanza la wanafunzi zaidi ya 100 tayari wamejiunga na mpango huu kama sehemu ya mpango wa mafunzo ya ujuzi wa maisha uitwao “Skills for Life”.
Wanafunzi hawa watajifunza miongoni mwa mambo mengine, viwango vya kimataifa vya utoaji wa vinywaji vya pombe ikiwa ni pamoja na ustadi wa kutengeneza mchanganyiko wa vinywaji vilivyo (cocktails) na visivyo na kilevi (mocktails), pamoja na kuboresha viwango vya huduma za baa na vinywaji.
“Haya ni mafunzo ya kipekee yanayoenda mbali na ujuzi wa kiufundi na kutoa mafunzo ya ujuzi wa maisha kama vile kutengeneza chapa binafsi, usimamizi wa muda, uongozi, na ufanisi katika mawasiliano,” alisema Rispa Hatibu wakati wa hafla ya ufunguzi wa kundi hilo la kwanza la wanafunzi.
Hatibu, ambaye ni Meneja Mawasiliano na Uendelevu wa SBL, alisisitiza dhamira ya kampuni katika maendeleo ya vijana akisema, “Mpango huu ni zaidi ya ujuzi tu—ni kuhusu kuwawezesha vijana na zana za kubadilisha maisha yao na kusaidia ukuaji wa sekta ya utalii na ukarimu nchini.”
Kwa upande wake, Mary Maduhu ambaye ni Meneja wa Taaluma kutoka NCT alielezea programu hii kama ishara ya maono ya ushirikiano kati ya SBL na NCT.
SOMA: PMAYA 2024: SBL yatwaa tuzo ya Rais kwa wazalishaji bora
“Mafunzo haya siyo tu yanahusu ujuzi wa kiufundi; ni kuhusu kufungua uwezo na kuhamasisha vipaji kwa wanafunzi. Pia ni mwanzo wa safari kuelekea ukuaji wa kitaaluma na kibinafsi,” alisema Maduhu.
Aliongeza kuwa sekta ya utalii ya Tanzania inakua kwa kasi na hivyo kuongeza mahitaji ya nguvu kazi yenye ujuzi wa sekta hiyo, pengo ambalo alisema ushirikiano kati ya SBL na NCT utasaidia kulijaza kwa kutengeneza nguvu kazi inayokidhi viwango vya kimataifa vya ukarimu.
“Zaidi ya athari yake ya moja kwa moja kwa wanafunzi, programu hii pia inaashiria dhamira pana kwa maendeleo endelevu. Kwa kukuza talanta na kuongeza ajira, SBL na NCT wanachangia katika ukuaji wa kijamii na kiuchumi wa taifa la Tanzania,” aliongeza Mkuu huyo wa Taaluma.
The post SBL yapaisha viwango vya sekta ya ukarimu kimataifa appeared first on HabariLeo.
SBL yapaisha viwango vya sekta ya ukarimu kimataifa

This story was originally published by Habari Leo.
Read the full story at Habari LeoRelated stories
TravelMiss World Kufungua Milango ya Utalii
ZANZIBAR imeendelea kujitokeza kama moja ya vivutio muhimu vya utalii nchini, safari hii ikipokea ugeni wa Miss World 2026, Joheirry Molla aliyewasili visiwani humo Novemba 19, 2026, akiwa ameambatana na warembo kutoka mabara sita.
TravelAskari Tanapa, TFS mbaroni mauaji ya wabeba mkaa
KAGERA; Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia askari 13, wakiwemo wa wanyamapori wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), askari wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na askari mgambo, kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne yaliyotokea Kijiji cha Kanyamika, Kata ya Karambi, Tarafa ya Kimwani, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Taarifa…
TravelNgorongoro scoops continental gong
ACCRA: THE Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) has won the Excellence in Sustainable Tourism and Conservation Management Award at the Africa Business Forum & Awards 2026. The award recognises Ngorongoro’s contribution to biodiversity conservation, sustainable tourism development and the protection of its outstanding natural and cultural heritage. The awards ceremony was held in Accra, Ghana,…
TravelDk Kijaji: Mashindano makubwa gofu Afrika kufanyika Serengeti
MARA; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, amesema Uwanja wa Gofu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti utawezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya gofu ya Afrika na kimataifa, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii, mapato na kuitangaza nchi kupitia utalii wa michezo. Akizungumza leo Oktoba 18, 2026, wakati wa uzinduzi wa…