RAIS William Ruto ameahidi kutumia Sh15 bilioni kujenga kilomita 150 za barabara katika Kaunti ya Busia, huku akizindua miradi ya miundombinu na kutangaza mipango ya kuimarisha usalama na usambazaji wa umeme katika eneo hilo.
Dkt Ruto, aliyeanza ziara ya siku nne katika eneo la Magharibi mwa Kenya Alhamisi, pia aliahidi kuunganisha familia 16,000 na umeme katika Busia ndani ya miezi sita ijayo.
Katika ziara hiyo, aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa kambi ya Kikosi cha kukabiliana na fujo (GSU) eneo la Akichelesit, Teso Kaskazini, na kutangaza kuwa serikali itatenga Sh100 milioni kujenga nyumba za maafisa watakaohudumu hapo.
Alisema mradi huo utaimarisha usalama katika eneo hilo na kuhakikisha maafisa wa polisi wanapata mazingira bora ya kuishi wanapotekeleza wajibu wao wa kulinda wananchi na mali yao.
Rais pia alifungua Kituo cha Utamaduni cha Kakapel Iteso, kinacholenga kuhifadhi na kukuza urithi wa jamii ya Iteso.
Katika Kaunti ya Bungoma, alizindua Barabara ya Matisi-Bokoli-Milani-Teremi, akaweka jiwe la msingi la soko la Bokoli na kufungua Barabara ya Mfupi-Mukuyuni-Naitiri pamoja na soko la Naitiri.
Baada ya kutangaza miradi hiyo, Dkt Ruto alitumia ziara hiyo kuwataka wapinzani wake kukubali kupimwa na wapigakura kwa rekodi zao za maendeleo badala ya kutumia idadi ya watu wa jamii zao kujipatia nafasi za kisiasa.
Akiwahutubia wakazi wa Teso Kaskazini, alisema uchaguzi unapaswa kuwa kipimo cha kile viongozi wamefanyia wananchi, wala si mashindano ya kikabila au kauli mbiu za kisiasa.
Alisema kila eneo nchini lina haki sawa ya kupata maendeleo na kwamba serikali yake haitaacha nyuma jamii yoyote katika mipango yake ya kubadilisha maisha ya wananchi.
Alikosoa wanasiasa ambao, kulingana naye, hutumia idadi ya watu na nguvu za kura za jamii zao kudai mgao wa mamlaka.
“Je, Mnataka kuambiwa kwamba unatoka katika jamii ndogo au kwamba ninyi ni wachache? Kila kiongozi anapaswa kupimwa na wapigakura na kuhukumiwa kwa rekodi yake ya kazi,” alisema.
Rais aliwauliza wapinzani wake ajenda yao ni ipi zaidi ya kauli za kutaka serikali iondoke madarakani, akisema yake inalenga miundombinu, kilimo, elimu na huduma za afya.
Kauli hizo zinaonekana kulenga pia msimamo wa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, anayeongoza chama cha Democracy for the Citizens (DCP), ambaye amekuwa akisisitiza umuhimu wa idadi ya kura za jamii mbalimbali katika mazungumzo ya kuunda serikali.
Dkt Ruto alipuuza madai kwamba jamii zinaweza kutumia idadi ya kura wanazodai kuwa nazo kama silaha ya kujadiliana kuhusu mamlaka.
“Hakuna mtu anayebeba mamilioni ya kura anayodai kuwa nayo na kwenda nayo hotelini kujadiliana kuhusu mamlaka. Nitawaonyesha vumbi,” alisema.
Aliwataka wakazi wa Busia kutathmini rekodi yake ya maendeleo na kumpa muhula wa pili ili aendeleze miradi inayoendelea.
Pia alitetea serikali jumuishi, akisema ndiyo njia ya kuimarisha umoja wa kitaifa na kuhakikisha kila eneo linanufaika na maendeleo.
Alisema serikali haitakubali siasa za ukabila na chuki, akiwataka wananchi kuungana chini ya falsafa ya “Usawa ni Sawa”.
Ruto apeleka injili ya ‘Usawa’ magharibi akiahidi miradi ya mabilioni ya pesa

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]