MAENDELEO ya afya ya msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya na mbunge wa zamani wa Mikumi, Joseph Haule ‘Professor Jay’, yameimarika kwa kiasi kikubwa, huku ikitabiriwa kuwa atarejea rasmi katika majukumu yake ifikapo mwaka 2026.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya kutimiza umri wa miaka 50 wa Professor Jay,Mama Lisa amesema kuimarika kwa afya ya msanii huyo ni matokeo ya rehema za Mwenyezi Mungu na ustahimilivu mkubwa katika kipindi cha matibabu.
“Tunapomshukuru Mungu kwa mume wangu kutimiza miaka 50, tunaziona rehema zake kwa namna afya yake ilivyotengemaa. Kulikuwa na nyakati ngumu zilizojaa maumivu na majaribu, lakini leo hii ni mzima, imara na ana afya njema,” alisema. SOMA: Prof Jay: DM yangu ina maombi mengi mno
Aidha, alibainisha kuwa kutokana na hatua hiyo kubwa ya kurejea kwa afya yake, kuna matumaini ya kumuona msanii huyo akirejea kulitumikia taifa kupitia sanaa na shughuli za kijamii kuanzia mwaka 2026, akiwa na ari mpya.
Professor Jay, ambaye mchango wake katika tasnia ya muziki na uongozi wa umma unatambulika kitaifa, amekuwa nje ya majukumu yake ya kawaida kwa muda mrefu kutokana na matibabu, hali iliyowahusisha viongozi wa kitaifa na wadau mbalimbali wa sanaa kumuombea na kumuunga mkono.The post Prof. Jay atimiza miaka 50 first appeared on HabariLeo.
Prof. Jay atimiza miaka 50

This story was originally published by Habari Leo.
Read the full story at Habari LeoRelated stories
TravelMiss World Kufungua Milango ya Utalii
ZANZIBAR imeendelea kujitokeza kama moja ya vivutio muhimu vya utalii nchini, safari hii ikipokea ugeni wa Miss World 2026, Joheirry Molla aliyewasili visiwani humo Novemba 19, 2026, akiwa ameambatana na warembo kutoka mabara sita.
TravelAskari Tanapa, TFS mbaroni mauaji ya wabeba mkaa
KAGERA; Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia askari 13, wakiwemo wa wanyamapori wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), askari wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na askari mgambo, kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne yaliyotokea Kijiji cha Kanyamika, Kata ya Karambi, Tarafa ya Kimwani, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Taarifa…
TravelNgorongoro scoops continental gong
ACCRA: THE Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) has won the Excellence in Sustainable Tourism and Conservation Management Award at the Africa Business Forum & Awards 2026. The award recognises Ngorongoro’s contribution to biodiversity conservation, sustainable tourism development and the protection of its outstanding natural and cultural heritage. The awards ceremony was held in Accra, Ghana,…
TravelDk Kijaji: Mashindano makubwa gofu Afrika kufanyika Serengeti
MARA; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, amesema Uwanja wa Gofu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti utawezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya gofu ya Afrika na kimataifa, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii, mapato na kuitangaza nchi kupitia utalii wa michezo. Akizungumza leo Oktoba 18, 2026, wakati wa uzinduzi wa…