ALIYEKUWA gavana wa Nairobi, Mike Sonko amepoteza kesi Sh385 milioni za ushuru kwenye mvutano unaohusu Sh1.4 bilioni zilizowekwa katika akaunti zake 11 za benki kati ya 2013 na 2019, alipohudumu kama seneta na gavana wa Nairobi.
Korti ya kutatua mizozo kuhusu ushuru ilibaini kuwa Sonko hakutoa ushahidi wa kutosha kuondoa tathmini ya Mamlaka ya Kukusanya Ushuru (KRA), kulingana na uchunguzi kuhusu pesa zilizowekwa akaunti hiyo.
“Amefeli kutekeleza mzigo wa ushahidi aliotwikwa chini ya Sheria kuhusu Korti ya Rufaa kuhusu Ushuru. Mlalamishi hajatoa ushahidi ya kuridhisha na ya kuthibitisha kwamba aliwapa washtakiwa stakabadhi na ushahidi wa kutosha kuwafanya kubadilisha uamuzi wake,” ilisema korti.
Kamishina wa KRA kuhusu Ushuru Nchini alichunguza masuala ya Sonko ya ushuru katika kipindi cha miaka saba na mnamo Juni 24, 2022, akatoa kiasi cha ziada cha mapato ya ushuru Sh407.4 milioni, kilichohitaji kuchunguzwa.
Bw Sonko baadaye aliruhusiwa kuwasilisha ombi akiwa amechelewa kupinga hatua hiyo. Disemba 13, 2024, KRA ilitoa uamuzi wa kupinga ikithibitisha uchunguzi wa Sh385 milioni.
Sonko alikata rufaa Januari 2025, akipinga namna ambavyo KRA ilishughulikia ununuzi na matumizi ya biashara yake.
Alihoji kuwa KRA ilikataza kwa njia isiyofaa ununuzi na matumizi ya biashara, ikapuuza stakabadhi za kuthibitisha, vyeti vya wauzaji bidhaa, na kukosa kutoa gharama halal zilizotokea wakati wa kuzalisha mapato yame.
KRA ilieleza korti kwamba Sonko aliendesha akaunti 11 za benki katika kipindi hicho kutoka benki za Equity, KCB, Diamond Trust na Co-operative Bank.
Pigo Sonko akipoteza kesi ya Sh385m za ushuru kwenye akaunti zake 11

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
BusinessAnthropic sets IPO price at $83 per share, targets $1.5trn valuation
–Claude maker raises $81.3bn in world’s largest IPO, overtakes SpaceX as investors rush for AI, despite $104bn lossBy Vera Anyagafu, with agency report The artificial intelligence race just produced the biggest stock market debut in history. Anthropic, the United States artificial intelligence company behind the Claude chatbot, on Wednesday priced its initial public offering at […]
BusinessOyedele urges banks to prioritise agricultural lending
…Commissions Moniepoint Abuja branch By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The Minister of Finance and Coordinating Minister of the Economy, Taiwo Oyedele, has urged banks and other financial institutions to make loans more affordable and accessible to businesses, particularly those operating in the agricultural sector, to stimulate productivity and economic growth. Oyedele made the call […]
BusinessNasarawa attracts $2.3bn investments in seven years — Abdullahi
Records 21 reforms, 11 PPP projects worth ₦93bn By John Alechenu ABUJA — Nasarawa State has attracted more than $2.3 billion in investments over the past seven years following reforms and institutional development aimed at making the state more competitive and investor-friendly. The Managing Director and Chief Executive Officer of the Nasarawa Investment and Development […]
BusinessObi pledges massive investment in education, healthcare
By Chimaobi Nwaiwu NNEWI — Presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, has pledged massive investment in education and healthcare, improved electricity supply and an end to kidnapping if elected president in 2027. Obi, who made the pledge on Friday during a visit to Onitsha, Anambra State, also said his proposed administration, […]