MASHIRIKA ya kutetea haki za binadamu yamekosa ruhusa ya kukagua eneo la Ikulu ya Nairobi, kufuatia madai kuwa ujenzi wa kanisa lenye thamani ya Sh1.8 bilioni unakaribia kukamilika licha ya agizo la korti la kusimamisha mradi huo.
Jaji David Mburu alitupilia mbali ombi hilo, akisema mashirika hayo hayakuwasilisha ushahidi wowote wa kuhalalisha ukaguzi wa eneo hilo.
Alisema mahakama haiwezi kutumiwa kufanya uchunguzi kwa niaba ya walalamishi.
Mashirika hayo ni Transparency International Kenya, Tume ya Kutetea Haki za Kibinadamu, Inuka Kenya Ni Sisi na Taasisi ya Uwajibikaji wa Kijamii.
Mashirika hayo yaliiambia mahakama kuwa yalipokea taarifa za ndani kwamba ujenzi wa kanisa hilo ulikuwa karibu kukamilika, hatua ambayo huenda ilikiuka agizo la mahakama la Agosti 26, 2025.
Kesi hiyo iliwasilishwa Agosti 2025, mashirika hayo yakipinga mpango wa kujenga kanisa la kudumu katika Ikulu.
Yalisema mradi huo unakiuka Katiba kuhusu kutengwa kwa masuala ya dini na utawala, matumizi ya ardhi na rasilimali za umma, usawa, uhuru wa kuabudu na ushirikishaji wa wananchi.
Wakili wa walalamishi alisema duru za kuaminika ziliwaarifu kuwa kanisa hilo lilikuwa karibu kukamilika.
Aliomba mahakama iruhusu ukaguzi kubaini iwapo ujenzi ulikuwa umeendelea licha ya amri iliyopo.
Alisema walalamishi wangeondoa kesi hiyo iwapo kanisa lilikuwa limekamilika, lakini hawakuweza kupata ushahidi kwa kuwa Ikulu inalindwa na haifikiki kwa urahisi.
Afisi ya Mwanasheria Mkuu ilipinga ombi hilo, ikisema lilitegemea uvumi usioambatana na hati ya kiapo au ushahidi wa barua.
Hata hivyo, Taasisi ya Katiba iliunga mkono ukaguzi huo.
Katika uamuzi wake, Jaji Mburu alisema wahusika wana wajibu wa kuwasilisha ushahidi wao.
“Mahakama haiwezi kutumiwa kama chombo cha kukusanya ushahidi,” akasema akiongeza kuwa ukaguzi unapaswa kufafanua ushahidi uliowasilishwa, wala si kuziba mapengo katika kesi ya mlalamishi.
Rais William Ruto alisema Julai 2025 kuwa alitaka kujenga kanisa la kudumu baada ya kupata sehemu ya kuabudia iliyoezekwa kwa mabati Ikulu.
Alisema michango ya kibinafsi ingefadhili mradi huo, akitaja gharama ya Sh350 milioni badala ya Sh1.2 bilioni zilizoripotiwa.
Mahakama bado haijaamua iwapo mradi huo unakiuka Katiba.
Ombi la kukagua ujenzi wa kanisa ikuluni lakataliwa

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsSenate committee hails Air Peace over ₦80,000 military fare
By Henry Umoru ABUJA — The Senate Committee on Army has commended Air Peace and its Chairman, Dr Allen Onyema, for introducing a discounted one-way domestic air fare of ₦80,000 for serving and retired personnel of the Nigerian Armed Forces. The committee also urged other airlines and corporate organisations in the country to emulate the […]
NewsTroops rescue 18 abducted children, hunt for four others in Kaduna
By Kingsley Omonobi Troops of the Nigerian Army under Operation Fansan Yamma have rescued 18 children abducted by suspected terrorists in Kaduna State, while intensifying efforts to secure the release of four others still held by the fleeing kidnappers. The children, members of the Boys’ and Girls’ Brigade, were reportedly abducted early Sunday, November 22, […]
NewsGovt tightens grip on sirens, flashing lights
KILIMANJARO: THE government has ordered the Police Force to tighten controls on unauthorised vehicle sirens and flashing lights, warning that rampant misuse of the devices undermines public safety and offers cover for criminals. Minister for Home Affairs Patrobas Katambi is- s u e d the directive yest e r d a y w h e…
NewsNairobi: Police launch probe as missing former MP is found dumped along Ngong Road
Former North Horr MP Francis Chachu Ganya was found alive, drugged along Ngong Road after vanishing for 24 hours, as investigators probe an alleged abduction.