AFISA Mkuu Msimamizi wa kituo cha polisi (OCS) cha Lamu Central anauguza majeraha aliyopata kwenye makabiliano na mshukiwa wa uhalifu.
Kamanda wa Polisi wa Lamu, Bw Shadrack Ruto, alisema OCS Hassan Noor alikuwa akiongoza kundi la maafisa sita Jumanne mchana kumkabili na kumkamata mshukiwa Ahmed Yusuf Bwanamadi aliyeripotiwa kubeba silaha hatari (panga) huku akihangaisha umma.
Licha ya polisi kumwamuru kuweka silaha chini na kujisalimisha mbele yao, mshukiwa alikataa na akamsongea OCS na kumkata sehemu ya mbele ya kichwa.
Ni hali iliyowalazimu polisi wengine kutumia bunduki zao ambapo walimpiga risasi mbili za mguu wa kushoto na kumlemaza.
Mshukiwa kwa sasa amelazwa kwenye hospitali kuu ya rufaa ya King Fahd kwa matibabu, naye OCS pia anapokea matibabu kwenye hospitali ambayo haikutajwa.
Bw Ruto alionya vikali raia wanaoendeleza uvamizi wa mara kwa mara na kuumiza polisi kukoma kwani hatua hiyo ni kinyume cha sheria.
Alisema maafisa wake hawatamvumilia yeyote anayewajia kwa lengo la kuwadhuru, akisema wako tayari kutumia bunduki kuyaokoa maisha yao.
OCS ashambuliwa na mshukiwa wa uhalifu

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]