KAUNTI za Mandera na Marsabit ndizo zinakabiliwa na hatari kuu zaidi ya kudhuriwa na ukame, hali inayohatarisha maisha ya wakazi na mifugo kutokana na ukosefu wa maji na malisho kote katika eneo hilo.
Ardhi imekauka na kupasukapasuka, maji yameadimika, huku joto kali likisababisha vichaka kudidimia na mifugo kufa.
Kamishina wa Mandera James Chacha anasema hali inazidi kuzorota kote katika kaunti hiyo huku maeneo yaliyoathirika zaidi yakijumuisha Mandera Kaskazini, Kati, Lafey na Mandera Magharibi.
Watu wapatao 300,000 wameathiriwa na idadi inazidi kupanda huku mvua ikikosa kunyesha na malisho kutoweka.
“Kiangazi kinatisha. Kuna haja ya mikakati endelevu ili kuokoa maisha ya binadamu na mifugo,” akasema Bw Chacha.
Serikali ya kaunti hiyo inavisambazia maji takriban vituo 299 lakini mahitaji yanazidi kwa mbali rasilimali zinazopatikana, na kuacha familia zikizidi kuathirika kwa sababu mifugo ikitembea mwendo mrefu, viwango vya maziwa vinadorora na familia zinakosa uwezo wa ununuzi.
Ili kupata maji, wanakijiji ni sharti wachange Sh25,000 kukodisha lori la lita 10,000, kiasi ambacho ni muhali kwa familia nyingi ambazo tayari zimepokonywa utajiri wazo wa mifugo.
Vijiji kadhaa vimeathirika ikiwemo vituo vya mpakani vilivyoonekana awali kama mikondo ya kujifaidi ambavyo sasa vimegeuka njia za kukatisha tamaa.
Katika kijiji cha Awara, makali ya kiangazi yamesababisha mimea na malisho kukauka.
Juhudi za kuweka mifugo hai zimekuwa ghali huku baadhi ya wakazi wakilazimika kusafiri mara moja kwa wiki mjini Rhamu, karibu kilomita 10, kununua malisho ya mifugo kwa sababu mimea haikui tena Awara.
Hali hiyo ya kusikitisha imegeuza masoko kuwa mahali pa ukandamizaji.
Njaa: Maelfu Mandera, Marsabit wachungulia kaburi

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
BusinessAnthropic sets IPO price at $83 per share, targets $1.5trn valuation
–Claude maker raises $81.3bn in world’s largest IPO, overtakes SpaceX as investors rush for AI, despite $104bn lossBy Vera Anyagafu, with agency report The artificial intelligence race just produced the biggest stock market debut in history. Anthropic, the United States artificial intelligence company behind the Claude chatbot, on Wednesday priced its initial public offering at […]
BusinessOyedele urges banks to prioritise agricultural lending
…Commissions Moniepoint Abuja branch By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The Minister of Finance and Coordinating Minister of the Economy, Taiwo Oyedele, has urged banks and other financial institutions to make loans more affordable and accessible to businesses, particularly those operating in the agricultural sector, to stimulate productivity and economic growth. Oyedele made the call […]
BusinessNasarawa attracts $2.3bn investments in seven years — Abdullahi
Records 21 reforms, 11 PPP projects worth ₦93bn By John Alechenu ABUJA — Nasarawa State has attracted more than $2.3 billion in investments over the past seven years following reforms and institutional development aimed at making the state more competitive and investor-friendly. The Managing Director and Chief Executive Officer of the Nasarawa Investment and Development […]
BusinessObi pledges massive investment in education, healthcare
By Chimaobi Nwaiwu NNEWI — Presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, has pledged massive investment in education and healthcare, improved electricity supply and an end to kidnapping if elected president in 2027. Obi, who made the pledge on Friday during a visit to Onitsha, Anambra State, also said his proposed administration, […]