FATAKI
MPAKA kati ya mapenzi na chuki ni finyu sana. Mtu anayempenda mwingine sana na kuwa radhi kumfanyia lolote hata ‘kumpa maisha yake,’ ndiye yuleyule anayeweza kumchukia mwenzake kwa ari na hamasa sawia kiasi cha kumfanyia maovu yasiyoelezeka.
Matukio yanayoshuhudiwa katika miaka ya karibuni kuhusu wanandoa na wapenzi waliopendana na kuendana kama pacha wa toke nitoke kabla ya kuchukiana, kutendeana uhayawani zaidi ya wanyama wenyewe, ni ithbati tosha.
Uhalisia huu unasisitiza haja ya kuhakikisha kuwa, iwapo ni lazima uwe na mpenzi au kufunga ndoa, unafanya hivyo na mtu mkarimu, mwenye maadili na utu!
Iwe ni mwanamke au mwanamme, umuhimu wa kuwa na uhusiano wa kimapenzi au kufunga ndoa na mtu anayekuthamini kwanza kama binadamu mwenye fikra zake razini na hisia, mwenye moyo wa huruma na msingi wa kimaadili au imani inayojikita kwenye kumwogopa Rabuka, hauwezi ukasisitizwa vya kutosha.
Sifa hizi zitakufaa mno wewe binafsi pamoja na mwenzako baadaye wakati kwa bahati mbaya, au nzuri, msisimko wa mapenzi utadidimia, ashiki kufifia na macho kufunguka na kukabiliana ana kwa ana na uhalisia wa mtu unayeishi au kuchumbiana naye.
Hakuna anayeingia kwenye mahusiano ya kimapenzi au kwenye ndoa akiwa na matumaini kwamba haitadumu. Wengi huwa na taswira ya jinsi watakavyoishi pamoja kwa furaha hadi uzeeni wao bila kutarajia kwamba mahusiano yao yatasambaratika.
Si ajabu kuwa ndoa huitwa kufunga pingu za maisha baada ya kulishana kiapo cha kuwa pamoja hadi wote au mmoja wao atakapomuaga mwenzake buriani.
Hata hivyo, mambo ni kangaja huenda yakaja na wakati mwingine, uchumba au ndoa husambaratika na wapenzi au wanandoa walioshibana wakakinaiana na kuchukiana vibaya.
Hapo ndipo baadhi ya wahasiriwa, katika juhudi za kulipiza kisasi au kuponza machungu kwa usaliti, kutemwa, huanza kumwaga mtama kuhusu mambo yao ya siri huku umma ukilazimishwa kutazama kwa mshangao sinema wasiofahamu ndewe wala sikio.
Ni katika kipindi hiki ambapo sifa za utu, huruma, na maadili huchangia pakubwa kumwezesha mtu binafsi kujizuia kumdhalilisha mwenzake baada ya mahusiano kuvunjika.
Ni fumbo jinsi penzi hugeuka shubiri, wengine wakiishia kuangamizana!
FATAKI MPAKA kati ya mapenzi na chuki ni finyu sana. Mtu anayempenda mwingine sana na kuwa radhi kumfanyia lolote hata ‘kumpa maisha yake,’ ndiye yuleyule anayeweza kumchukia mwenzake kwa ari na hamasa sawia kiasi cha kumfanyia maovu yasiyoelezeka. Matukio yanayoshuhudiwa katika miaka ya karibuni kuhusu wanandoa na wapenzi waliopendana na kuendana kama pacha wa toke nitoke kabla ya kuchukiana, kutendeana uhayawani zaidi ya wanyama wenyewe, ni ithbati tosha. Uhalisia huu unasisitiza haja ya kuhakikisha kuwa, iwapo ni lazima uwe na mpenzi au kufunga ndoa, unafanya hivyo na mtu mkarimu, mwenye maadili na utu! Iwe ni mwanamke au mwanamme, umuhimu wa kuwa na uhusiano wa kimapenzi au kufunga ndoa na mtu anayekuthamini kwanza kama binadamu mwenye fikra zake razini na hisia, mwenye moyo wa huruma na msingi wa kimaadili au imani inayojikita kwenye kumwogopa Rabuka, hauwezi ukasisitizwa vya kutosha. Sifa hizi zitakufaa mno wewe binafsi pamoja na mwenzako baadaye wakati kwa bahati mbaya, au nzuri, msisimko wa mapenzi utadidimia, ashiki kufifia na macho kufunguka na kukabiliana ana kwa ana na uhalisia wa mtu unayeishi au kuchumbiana naye. Hakuna anayeingia kwenye mahusiano ya kimapenzi au kwenye ndoa akiwa na matumaini kwamba haitadumu. Wengi huwa na taswira ya jinsi watakavyoishi pamoja kwa furaha hadi uzeeni wao bila kutarajia kwamba mahusiano yao yatasambaratika. Si ajabu kuwa ndoa huitwa kufunga pingu za maisha baada ya kulishana kiapo cha kuwa pamoja hadi wote au mmoja wao atakapomuaga mwenzake buriani. Hata hivyo, mambo ni kangaja huenda yakaja na wakati mwingine, uchumba au ndoa husambaratika na wapenzi au wanandoa walioshibana wakakinaiana na kuchukiana vibaya. Hapo ndipo baadhi ya wahasiriwa, katika juhudi za kulipiza kisasi au kuponza machungu kwa usaliti, kutemwa, huanza kumwaga mtama kuhusu mambo yao ya siri huku umma ukilazimishwa kutazama kwa mshangao sinema wasiofahamu ndewe wala sikio. Ni katika kipindi hiki ambapo sifa za utu, huruma, na maadili huchangia pakubwa kumwezesha mtu binafsi kujizuia kumdhalilisha mwenzake baada ya mahusiano kuvunjika.

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
GeneralT- Touch ampa onyo Marioo bifu yake na Ibraah, Atoa mazito "Usiingilie bifu yangu na S2Kizzy"
FOLLOW KURASA ZETU ZA MITANDAO YA KIJAMII: Instagram
GeneralLagos renews campaign against open defecation
…Calls for improved sanitation, gender-sensitive toilet facilities By Olasunkanmi Akoni The Lagos State Government has renewed its campaign for improved sanitation, proper hygiene practices and access to safe toilet facilities as part of efforts to eliminate open defecation and promote public health. The Special Adviser to the Governor on Environment, Olakunle Akodu, and the Permanent […]
GeneralWaste crisis: LAWMA acting MD unveils 60-day action plan
…Warns staff against laxity, promises operational overhaul By Olasunkanmi Akoni The newly appointed Acting Managing Director of the Lagos Waste Management Authority (LAWMA), Olajuwon Akinyemi, has unveiled a 60-day emergency action plan to tackle waste management challenges across Lagos State, warning staff against indiscipline and poor performance. Akinyemi, who has assumed office amid growing concerns […]
GeneralWedding guests mocked my thrift-store dress — Then the groom’s mom spoke up
A thrift-store wedding dress draws cruel judgment, until the bride’s mother-in-law reveals its family history and brings the ceremony to a shocking standstill.