MAHAKAMA Kuu imempa mwanablogu na mtumiaji wa mitandao ya kijamii, Ndiang’ui Kinyagia, fidia ya Sh5 milioni baada ya kubaini kwamba maafisa wa polisi walikiuka haki zake walipovamia nyumba yake, kuipekua, kutwaa mali yake na kumzuia kusafiri kwa uhuru.
Katika uamuzi uliotolewa na Jaji Patricia Nyaundi wa Kitengo cha Katiba na Haki za Kibinadamu jijini Nairobi, mahakama ilisema polisi waliingia nyumbani kwa Kinyagia mnamo Juni 21, 2025, bila kibali cha mahakama na bila kuthibitisha kuwa walitimiza masharti ya kufanya upekuzi bila kibali hicho.
Jaji Nyaundi alisema maafisa hao walishindwa kuwasilisha sababu zilizoonyesha kwamba kupata kibali cha mahakama kungeathiri au kuchelewesha uchunguzi wao.
“Sehemu ya 60 ya Sheria ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi si tu tamko la kawaida. Ni kinga ya kikatiba iliyowekwa kisheria ili kulinda haki za wananchi,” alisema jaji huyo.
Kinyagia, ambaye ni mjasiriamali wa teknolojia na mchangiaji wa masuala ya umma mtandaoni, alipata umaarufu mnamo Juni 2025 baada ya kujificha alipogundua kwamba maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) walikuwa wakimtafuta kufuatia chapisho la mtandaoni lililohusishwa na maandamano yaliyokuwa yakipangwa dhidi ya serikali.
Polisi walikuwa wameanzisha uchunguzi kuhusu ujumbe uliowekwa katika mtandao wa X waliodai ulikuwa wa uchochezi na wenye maudhui ya uasi. Baada ya kufuatilia akaunti hiyo hadi kwa Kinyagia na kupata usaidizi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya, maafisa walielekea nyumbani kwake.
Mahakama ilielezwa kwamba polisi walipiga kambi katika makazi hayo kwa muda mrefu kabla ya kuvunja mlango na kuingia ndani waliposhindwa kumpata. Walipekua nyumba hiyo na kuondoka na vifaa mbalimbali huku wakiacha orodha ya vitu vilivyochukuliwa kwa msimamizi wa eneo hilo.
Jaji Nyaundi aliamua kuwa hatua hiyo ilikiuka haki za Kinyagia za faragha, mali, utu, usalama wa kibinafsi na uhuru wa kutembea.
Mahakama pia ilizuia Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) pamoja na polisi kuendelea kumshtaki Kinyagia kuhusiana na uchunguzi huo, ikisema mchakato mzima ulianza kwa vitendo visivyozingatia Katiba.
Mwanablogu kulipwa Sh5 milioni kwa kuvamiwa na polisi

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]