Video
MTENDAJI UYUI AREJESHA MILIONI NANE ZA WANANCHI
Channel: ITV Tanzania Watch on YouTube
About this video
#HABARI: Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Malongwe wilayani Uyui mkoani Tabora, Wiston Cyprian Hizza, anayelalamikiwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kuweka watu vizuizini na kuwapora mali, amelazimika kurejesha shilingi milioni nane kwa mfanyabiashara Masanja Mwandu baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuingilia kati. Hatua hiyo imefuatia sakata ambapo mtendaji huyo alimweka kizuizini mfugaji James Lugaila na kumtaka kulipa faini ya shilingi milioni nane, na alipokosa fedha hizo alimpigia simu Mwandu alipe faini hiyo huku Lugaila akilazimika kumkabidhi mfanyabiashara huyo ng'ombe wake 14 kama malipo, ambao sasa wamerejeshwa kwake. Akizungumza wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha Aprili hadi Septemba mwaka huu, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tabora, Azza Mtaita, ameeleza hatua zinazoendelea kuchukuliwa dhidi ya vitendo kandamizi kwa wananchi, pamoja na kushughulikia ubadhirifu wa fedha za vyama vya ushirika, fedha za umma na miradi ya serikali. Kwa upande wake, mfugaji James Lugaila ameelezea namna alivyowekwa kizuizini na kupokwa mifugo yake kabla ya taasisi hiyo kumsaidia kupata haki yake. RADIO ZETU KWENYE VING’AMUZI: Radio One: Azam 061, Digitek 110, Capital Radio: Azam 383, Digitek 112, Powered by #MCHEZOSUPA JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA: - Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Mix by Yas, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV. #ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania Follow @itvtz @radioonetanzania @itv2tanzania
Related stories
GeneralElectoral Act not responsible for rising campaign violence — Adegbonmire
By Cynthia Alo & Kafayat Kokumo Chairman of the Senate Ad Hoc Committee on Electoral Reforms, Adeniyi Adegbonmire, has said the Electoral Act is not responsible for rising cases of campaign violence across the country, insisting that the problem lies in the failure of relevant institutions to enforce its provisions. Adegbonmire, who is also the […]
General"UCHAWI WALETE KWANGU, HAPA HAKUNA SHAMBA LA MTU!" - MGOGORO WA ARDHI WAVUMA
"UCHAWI WALETE KWANGU, HAPA HAKUNA SHAMBA LA MTU!" - MGOGORO WA ARDHI WAVUMA "Uchawi mlete kwangu, hapa hakuna shamba la mtu!" - Kauli nzito yatolewa hadharani kuhusu mgogoro wa ardhi na mashamba ya…
GeneralNigeria records 94% HIV viral suppression – NACA
The NACA director-general, however, identified gaps in HIV diagnosis, stressing the need to ensure more Nigerians know their status and access uninterrupted treatment. She said Early Infant Diagnosis coverage among HIV-exposed infants increased from 15 per cent in 2022 to 66 per cent in 2025. “While this is significant progress, we must do more to […]
General