KINYUA Nkanata amekuwa kwenye uzalishaji wa avokado kwa zaidi ya miaka 16, akiwa aliingilia kilimo chake kama njia ya kujipa pato la ziada.
Hata ingawa tayari ameshastaafu, alikuwa akihudumu katika mashirika mbalimbali kitengo cha mauzo, ikiwemo shirika moja la habari nchini.
Avokado, pia maparachichi, anaendeleza kilimo chake eneo la Meru.
Matunda hayo yameanza kupata umaarufu mkubwa Meru, na yanaepelekana sako kwa bako na chai—zao linalokuzwa kwa wingi katika kaunti hiyo.
[caption id="attachment_175901" align="aligncenter" width="300"] Kinyua Nkanata, mkulima wa maparachichi Meru. Picha|Sammy Waweru[/caption]
Nkanata hulima maparachichi kwa ajili ya soko la nje ya nchi.
Hata hivyo, kwa miaka mitatu hadi minne iliyopita, uzalishaji wake umekumbwa na changamoto si haba kutokana na mdudu anayefahamika kama False Codling Moth (FCM).
FCM ni mdudu hatari sana anayeshambulia matunda kama vile avokado, na hushinikiza wakulima kutumia dawa zenye kemikali kuua wadudu, ambazo pia huhatarisha afya ya binadamu.
[caption id="attachment_175902" align="aligncenter" width="300"] Wadudu aina ya FCM walionaswa kupitia mtego wa sola. Picha|Sammy Waweru[/caption]
Kenya ikiwa mzalishaji mkuu wa maparachichi Barani Afrika na kuorodheshwa sita bora duniani, uwepo wa FCM unatishia nafasi yake ya kipekee katika soko la kimataifa.
Soko la Ulaya, linaloongoza kwa uagizaji wa avokado kutoka Kenya, lina masharti makali kuhusu viwango vya mabaki ya dawa kwenye mazao. Nkanata anaeleza kuwa FCM ilianza kushambulia shamba lake 2022, na kusababisha hasara na upotevu mkubwa wa mazao.
Awali, mazao yaliyoishia kukataliwa sokoni yalikuwa yakichezea kilo 200 hadi 500 kwa msimu.
Lakini kuanzia 2022, kiwango hicho kiliongezeka hadi tani 2.2 (sawa na kilo 2,200).
[caption id="attachment_175903" align="aligncenter" width="300"] Mdudu hatari aina ya FCM akishambulia avokado kiwango chake cha mazao kinashuka. Ila kwa kutumia solar traps, mkulima anapata afueni. Picha|Sammy Waweru[/caption]
“Maparachichi ya kuuza nje huuzwa kwa kati ya Sh100 hadi Sh140 kwa kilo, lakini yakishambuliwa, bei hushuka hadi Sh30 kwa kilo katika soko la ndani,” anasema mkulima huyo.
FCM ni mdudu ambaye ni karantini; akigunduliwa kwenye kontena, bidhaa hiyo hurudishwa nchi ilikotoka.
Katika harakati za kukabiliana na changamoto hiyo, barobaro mbunifu amebuni mtego unaotegemea nguvu za kawi, yaani miale ya jua unaosaidia kudhibiti FCM.
“Kutumia mitego ya wadudu ya sola ni njia ya kiasili kudhibiti wadudu,” anasema Nkanata, ambaye pia ni mwenyekiti wa muungano wa wakulima wa maparachichi Abogeta West, Meru.
[caption id="attachment_175904" align="aligncenter" width="300"] Kinyua Nkanata akielezea jinis mtego wa FCM unavyofanya kazi usiku. Picha|Sammy Waweru[/caption]
Mbunifu huyo ni Mutuma Muriuki, ambaye ni mwanzilishi wa Eco Bristo Ltd, kampuni inayounda na kusambaza mitego maalum hasa kukabiliana na mdudu hatari aina ya FCM. “Sikutaka tu kutengeneza teknolojia maarufu, nilitaka sana kuangazia mahangaiko ya wakulima kutokana na wadudu ili chakula kinachotufikia kiwe salama—ambacho hakijakuzwa kwa kutumia dawa zenye kemikali,” Mutuma akaambia Akilimali kwenye mahojiano ya kipekee.
Akiwa na taaluma ya kilimohai (Agroecology), Mutuma ametumia tajriba yake kutoa huduma za kilimo Bara Afrika, India, Colombia na Mexico kusaidia wakulima wa mashamba madogo. Mwaka 2021, kwa kutumia Sh150, 000, akiba, alianza kutengeneza mitego hiyo akiwa Meru.
Mtego wa sola unavyofanya kazi
Teknolojia hiyo hutumia mwanga wa buluu wa LED kuvutia wadudu. Baada ya kuvutiwa, wadudu huanguka kwenye chombo chenye maji na sabuni au huangamizwa kwa umeme—kulingana na aina ya mtego.
[caption id="attachment_175906" align="aligncenter" width="300"] Mutuma Muriuki, ambaye ni mwanzilishi wa Eco Bristo Ltd, kampuni inayotoa huduma za mitego ya wadudu. Picha|Sammy Waweru[/caption]
Miundo ya mitego hiyo ni Kifaru—ya mashamba madogo, Ndovu, mashamba makubwa, na Chui iliyotengenezwa kuhudumu kwenye ekari moja.
Bei, inalingana na saizi na muundo.
Eco Bristo pia hutengeneza bidhaa ya kuongeza rutuba kwenye udongo kwa kutumia biochar—makaa ya Kaboni.
Licha ya changamoto za kifedha kuboresha ubunifu wake, 2023 Mutuma alipata granti ya Sh1 milioni kutoka kwa Shirika lisilo la Kiserikali la Heifer International, ambalo lina mpango maalum kusaidia wakulima.
[caption id="attachment_175907" align="aligncenter" width="300"] Mutuma Muriuki akielezea jinsi mitego anayounda inavyofanya kazi kunasa wadudu. Picha|Sammy Waweru[/caption]
Aidha, granti hiyo ambayo pia ni tuzo hutolewa kupitia shindano la AYuTe linalolenga vijana wanaoshiriki mtandao wa kilimo na uzalishaji chakula, wenye bunifu kuangazia changamoto zinazozingira wakulima.
Lengo la Mutuma ni moja tu; kuhakikisha Kenya na Bara Afrika inazalisha chakula salama, bila dawa.
Mkulima wa avokado anavyokabili wadudu kupitia mtego wa sola
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
BusinessAnthropic sets IPO price at $83 per share, targets $1.5trn valuation
–Claude maker raises $81.3bn in world’s largest IPO, overtakes SpaceX as investors rush for AI, despite $104bn lossBy Vera Anyagafu, with agency report The artificial intelligence race just produced the biggest stock market debut in history. Anthropic, the United States artificial intelligence company behind the Claude chatbot, on Wednesday priced its initial public offering at […]
BusinessOyedele urges banks to prioritise agricultural lending
…Commissions Moniepoint Abuja branch By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The Minister of Finance and Coordinating Minister of the Economy, Taiwo Oyedele, has urged banks and other financial institutions to make loans more affordable and accessible to businesses, particularly those operating in the agricultural sector, to stimulate productivity and economic growth. Oyedele made the call […]
BusinessNasarawa attracts $2.3bn investments in seven years — Abdullahi
Records 21 reforms, 11 PPP projects worth ₦93bn By John Alechenu ABUJA — Nasarawa State has attracted more than $2.3 billion in investments over the past seven years following reforms and institutional development aimed at making the state more competitive and investor-friendly. The Managing Director and Chief Executive Officer of the Nasarawa Investment and Development […]
BusinessObi pledges massive investment in education, healthcare
By Chimaobi Nwaiwu NNEWI — Presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, has pledged massive investment in education and healthcare, improved electricity supply and an end to kidnapping if elected president in 2027. Obi, who made the pledge on Friday during a visit to Onitsha, Anambra State, also said his proposed administration, […]