WAZIRI wa Fedha John Mbadi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dorcas Oduor wameamriwa kufika katika Mahakama Kuu Novemba 27, 2026, kusikilizwa kabla ya kupewa adhabu kwa kupuuza amri za mahakama kuhusu ufichuzi wa mikataba ya mikopo ya kimataifa.
Jaji Patricia Nyaundi aliwapata wawili hao na hatia ya kudharau mahakama baada ya serikali kukosa kutoa maelezo kuhusu mikopo ya kimataifa na jinsi fedha hizo zilivyotumika.
Jaji alisema wawili hao watawasilisha sababu za kupunguziwa adhabu kabla ya hukumu kutolewa.
Kesi hiyo inatokana na uamuzi wa Desemba 2024 ambapo Mahakama Kuu iliamua kuwa serikali ilikiuka haki ya wananchi kupata habari kwa kukataa kutoa maelezo kuhusu mikopo kwa kipindi cha miaka tisa.
Jaji Lawrence Mugambi aliamuru serikali kutoa stakabadhi hizo ndani ya siku 45 kufuatia ombi la Tume ya Haki za Kibinadamu Kenya na Wanjiru Gikonyo.
Jaji Nyaundi alisema ushahidi ulionyesha kuwa amri ya mahakama ilifikishwa kwa maafisa hao, lakini hawakuwasilisha majibu kupinga ombi la kuwatangaza kuwa walidharau mahakama.
Alionya kuwa amri za mahakama ni lazima ziheshimiwe na kwamba kuziacha kukiukwa bila hatua kunadhoofisha utawala wa sheria.
Mbadi, Mwanasheria Mkuu hatarini kuadhibiwa kwa kukosa kufichua mikataba ya mikopo ya Serikali

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]