KIWANDA kipya cha kuzalisha kemikali ya kuunda saruji kinachojengwa Matuga, Kaunti ya Kwale, kinatarajiwa kuongeza uwezo wa Bamburi Cement kuzalisha kemikali ya Clinker kutoka tani milioni moja hadi milioni 2.6 kwa mwaka.
Mradi huo wa Sh250 milioni pia utaongeza uwezo wa kampuni hiyo kuzalisha saruji kutoka tani milioni 1.8 hadi milioni nne kila mwaka, hatua inayolenga kuimarisha sekta ya ujenzi nchini na kupunguza utegemezi wa uagizaji wa bidhaa hiyo.
Rais William Ruto aliweka jiwe la msingi la mradi huo, uliohudhuriwa na viongozi wa serikali, wawekezaji na viongozi wa eneo hilo.
Miongoni mwa waliohudhuria ni Mawaziri Hassan Joho na Salim Mvurya, Mkurugenzi Mkuu wa Amsons Group Edha Nahdi, Gavana wa Kwale Fatuma Achani, Spika wa Seneti Amason Kingi na Mwenyekiti wa Bodi ya Bamburi Cement Dkt John Simba.
Akizungumza katika hafla hiyo, Nahdi alisema uwekezaji huo unaonyesha dhamira ya muda mrefu ya Amsons Group katika kukuza uchumi wa Kenya na kuimarisha uzalishaji wa bidhaa nchini.
Kwa upande wake, Dkt Simba alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha jamii zinazoishi karibu na mradi zinanufaika na uwekezaji huo.
Alitaja mpango wa kuhamisha wakazi wa Kijiji cha Mwachome, ambao ulihusisha pia mafunzo ya usimamizi wa fedha ili kuwasaidia wakazi walioathiriwa kutumia vizuri rasilimali walizopokea.
Gavana Achani alitoa wito kwa wakazi wa Matuga na wafanyabiashara wa eneo hilo kushirikishwa kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huo ili wanufaike na fursa za kiuchumi.
Kiwanda hicho kinatarajiwa kuunda zaidi ya nafasi 10,000 za ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, hususan katika sekta za usafirishaji, uchimbaji wa mawe.
Mkurugenzi Mkuu wa Wave 360 Africa, Zedd Mukoya, alisema mradi huo ni fursa kwa vijana wa Kwale kushiriki katika maendeleo ya viwanda katika kaunti yao.
“Matumaini yangu ni kwamba siku moja kijana kutoka Kwale ataweza kuutazama kiwanda hicho na kusema, ‘Nilisaidia kukijenga na kimenipa mustakabali mzuri katika eneo langu,’” alisema Mukoya
Kampuni ya Wave 360 Africa ilihusika na maandalizi na uratibu wa hafla hiyo, ikisimamia miundombinu, uwekaji chapa, itifaki na shughuli za uwanjani.
Mamia kunufaika na mradi wa kiwanda cha Bamburi

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
Jobs and Career₦1.45trn Lagos ports upgrade targets 20,000 jobs
…As FG flags off Apapa, Tin Can modernisation By Efe Onodjae The Federal Government on Wednesday flagged off a £746 million (about ₦1.45 trillion) modernisation of Apapa and Tin Can Island ports in Lagos, targeting 48-hour cargo clearance and the creation of 20,000 direct and indirect jobs. The project is expected to reduce cargo delays, […]
Jobs and CareerEast African Community announces 68 job vacancies: How Kenyans can apply
EAC opens 68 jobs across East Africa, from senior to support roles. Eligibility, age limit and online application rules for citizens of its eight partner states.
Jobs and CareerKenya, Canada province sign new deal to open more job opportunities for skilled workers
Kenya and New Brunswick signed a labour mobility MoU linking skilled workers and eligible refugees with employers through training and migration support pact.
Jobs and CareerEquity Bank posts top job vacancies for Kenyan professionals
Equity Bank Kenya has advertised 15 full-time jobs across commercial, risk, credit and foundation roles, with deadlines from November 26 to December 17, 2026.