KATIKA Kiswahili, upatanisho wa kisarufi ni muhimu tunapotaja idadi.
Mojawapo ya makosa yaliyozoeleka ni kuhesabu miezi bila kutumia kiambishi cha nomino ambacho ni mi-.
Ni kawaida kukutana na sentensi kama vile:
*Msimu huo mvua ilinyesha kwa mwezi tatu. Sentensi hii si sahihi. Nomino mwezi inamaanisha kipindi cha siku ishirini na nane hadi thelathini na moja.
Kwa hivyo katika wingi itakuwa miezi. Vilevile, kivumishi cha idadi tatu kinafaa kichukue kiambishi mi-. Ili kuisahihisha tutasema: Msimu huo mvua ilinyesha kwa miezi mitatu.
Makosa mengine yaliyozoeleka katika kuhesabu nomino ni kuvipa vivumishi tasa viambishi vya idadi: sita, saba, tisa na kumi.
Kila mara utakumbana na sentensi kama vile: Nilipofika darasani niliwapata wanafunzi *wasita. Vikombe *visaba vimeoshwa na mpishi.
Magari *matisa yameegeshwa. Miti *mikumi ilipandwa jana. Sentensi hizi si sahihi kwani zimetumia viambishi vya nomino mwanzoni mwa vivumishi sita, saba, tisa na kumi.
Tunafaa kuzisahihisha kwa kusema: Nilipofika darasani niliwapata wanafunzi sita. Vikombe saba vimeoshwa na mpishi. Magari tisa yameegeshwa. Miti kumi ilipandwa jana.
Kosa jingine la kawaida tunapohesabu nomino ni kukosa kutumia viambishi vya nomino tunapotaja vivumishi vya idadi vinavyobadilika katika wingi.
Aghalabu utakumbana na sentensi kama: *Nilinunua vitabu kumi na moja. *Wageni tano wamewasili kwetu.
Tunafaa kusema: Nilinunua vitabu kumi na kimoja. Wageni watano wamewasili kwetu.
Mwanafunzi mwenye changamoto ya kuhesabu nomino kwa usahihi, afanye mazoezi ya kuhesabu nomino ainati katika umoja na wingi.
Makosa ya kudondosha viambishi vya idadi ya nomino katika wingi

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
TravelMiss World Kufungua Milango ya Utalii
ZANZIBAR imeendelea kujitokeza kama moja ya vivutio muhimu vya utalii nchini, safari hii ikipokea ugeni wa Miss World 2026, Joheirry Molla aliyewasili visiwani humo Novemba 19, 2026, akiwa ameambatana na warembo kutoka mabara sita.
TravelAskari Tanapa, TFS mbaroni mauaji ya wabeba mkaa
KAGERA; Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia askari 13, wakiwemo wa wanyamapori wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), askari wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na askari mgambo, kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne yaliyotokea Kijiji cha Kanyamika, Kata ya Karambi, Tarafa ya Kimwani, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Taarifa…
TravelNgorongoro scoops continental gong
ACCRA: THE Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) has won the Excellence in Sustainable Tourism and Conservation Management Award at the Africa Business Forum & Awards 2026. The award recognises Ngorongoro’s contribution to biodiversity conservation, sustainable tourism development and the protection of its outstanding natural and cultural heritage. The awards ceremony was held in Accra, Ghana,…
TravelDk Kijaji: Mashindano makubwa gofu Afrika kufanyika Serengeti
MARA; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, amesema Uwanja wa Gofu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti utawezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya gofu ya Afrika na kimataifa, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii, mapato na kuitangaza nchi kupitia utalii wa michezo. Akizungumza leo Oktoba 18, 2026, wakati wa uzinduzi wa…