VideoUpcoming
CHADEMA WALIAMSHA/NI KUHUSU MARIDHIANO/WATOA MASHARTI MAWILI/DIRA YA TAIFA VIPI INAFUATWA?
Channel: Global TV Online Watch on YouTube
About this video
🔴#LIVE:CHADEMA WALIAMSHA/NI KUHUSU MARIDHIANO/WATOA MASHARTI MAWILI/DIRA YA TAIFA VIPI INAFUATWA? TANGAZA NA FRONTPAGE SASA TUPIGIE. 0687 531 251 ============================================================ ⚫️ JE, UNA HABARI? ⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 760 403894 or 255 719 401968) ⚫️ Email: [email protected]
Related stories
NewsSerikali yachunguza madai ya udukuzi wa jukwaa la eCitizen
SERIKALI imeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya shambulizi kubwa la kimtandao dhidi ya mfumo wa eCitizen, huku kukiwa na hofu kuwa taarifa binafsi za Wakenya na data za serikali huenda ziliibwa. Kundi la wahalifu wa kimtandao linalojiita ByteToBreach linadai kuwa lilidukua mfumo huo na kuiba gigabaiti 600 za stakabadhi za taarifa za wateja, gigabaiti 100 za data na gigabaiti 40 za misimbo ya programu za kompyuta. Taarifa hizo ziliibuliwa Jumatatu na kampuni ya Amerika inayohusika na usalama wa kimtandao, Vecert. Kundi hilo pia linadai kuwa liliweza kuingilia mifumo inayowaunganisha Wakenya na huduma mbalimbali za serikali. Hata hivyo, Wizara ya Usalama wa Ndani ilisema kikosi chake cha kiufundi na usalama kinafanya uchunguzi kubaini ukubwa wa tukio hilo. Katika taarifa iliyotolewa Jumanne, wizara hiyo ilihakikishia umma kuwa huduma za eCitizen zinaendelea kupatikana kama kawaida. “Tunashirikiana na mashirika husika ya serikali kukabiliana na tukio hili. Huduma za eCitizen zinaendelea kupatikana na umma unaweza kuendelea kuzitumia kama kawaida," ilisema wizara. Kampuni ya Webmasters Kenya Ltd, inayosimamia jukwaa la eCitizen, iliambia ‘Taifa Leo’ kuwa suala hilo linashughulikiwa na mashirika husika ya serikali. eCitizen ni jukwaa kuu linalowawezesha Wakenya na wakazi wengine kupata huduma za serikali kupitia akaunti moja. Jukwaa hilo linaunganisha zaidi ya huduma 22,000, zikiwemo maombi ya pasipoti, leseni za udereva, vitambulisho, vyeti vya kuzaliwa na ndoa, vyeti vya tabia njema na usajili wa biashara. Wataalamu wanaonya kuwa iwapo madai ya udukuzi yatathibitishwa, mifumo mingine inayotumia teknolojia ya eCitizen inaweza pia kuwa hatarini. Mtafiti wa usalama wa kimtandao na mkuu wa Cyber Guard Africa, Dkt Bright Gameli, alisema kuingiliwa kwa mfumo mkuu wa habari kama eCitizen kunaweza kuwapa wahalifu njia ya kufikia huduma nyingine zilizounganishwa nao. Kundi hilo limetaja Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA), Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI), Safaricom na Huduma ya Kita
NewsALIYEDUKUA GTA VI AHUKUMIWA MIAKA SABA JELA, AACHILIWA SIKU HIYOHIYO
NewsDelta Killings: Police summon Omo-Agege, Egbo, others for questioning
The competing accounts bring the number of fatalities to seven, although the governor and police put the toll at six, pending investigations
NewsSifuna ataka aondolewe kwenye kesi ya kubadilisha jina la chama
SENETA wa Nairobi Edwin Sifuna ameomba Jopo la Kutatua Migogoro ya Vyama vya Kisiasa kumuondoa katika kesi inayopinga kubadilisha jina la chama cha The Equitable Party (TEP) kuwa Linda Mwananchi Movement. Katika pingamizi lake, Sifuna anasema hahusiki moja kwa moja na maamuzi yanayopingwa na mwanachama Emmanuel Willyngtone Khamala, wala mlalamishi hajaomba amri yoyote dhidi yake. Anataka mahakama kutupilia mbali malalamishi hayo dhidi yake pamoja na gharama za kesi. Khamala anapinga hatua za viongozi wa chama kubadilishwa bila kuwashirikisha wanachama ipasavyo. TEP ilizinduliwa katika Hoteli ya Serena jijini Nairobi Oktoba 4, 2026, huku Sifuna akitangazwa kuwa kiongozi wake. Siku nne baadaye, Kamati Kuu ya Kitaifa ya chama hicho iliidhinisha azimio la kubadilisha jina kuwa Linda Mwananchi Movement. Khamala anasema uamuzi huo ulifanywa bila kuwashirikisha wanachama waliosajiliwa, licha ya kuwaathiri moja kwa moja. Pia, anapinga kutangazwa kwa kikosi kipya cha uongozi Oktoba 30, akisema wanachama hawakushauriwa wala kupewa taarifa.