Benki ya Standard Chartered imefungua kituo kipya cha huduma za kifedha cha Priority Centre katika eneo la Nyali, Mombasa, hatua inayolenga kuwahudumia wateja wenye uwezo mkubwa wa kifedha katika eneo la Pwani.
Kituo hicho kitatoa huduma maalumu za ushauri kuhusu uwekezaji, upangaji wa mali, ufadhili, uhifadhi wa utajiri na mipango ya kurithisha mali vizazi vijavyo. Benki hiyo imesema hatua hiyo inalenga kuwaleta karibu wananchi wa Pwani na fursa za uwekezaji wa kimataifa kupitia mtandao wake mkubwa duniani.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Birju Sanghrajka, Mkurugenzi Mkuu wa Standard Chartered Kenya, alisema Mombasa imeendelea kuwa kitovu muhimu cha shughuli za kiuchumi nchini kutokana na ukuaji wa biashara, utalii, usafirishaji na viwanda. Alibainisha kuwa uchumi wa kaunti hiyo una thamani ya zaidi ya Sh700 bilioni, jambo linaloongeza mahitaji ya huduma za kifedha za hali ya juu.
Kwa upande wake, Edith Chumba, Mkuu wa Huduma za Utajiri wa Standard Chartered Kenya na Afrika Mashariki, alisema wateja wengi wanahitaji ushauri unaovuka mipaka ya uwekezaji wa kawaida ili kuwasaidia kujenga, kuhifadhi na kuhamisha utajiri wao kwa vizazi vijavyo.
Kauli hiyo pia ilionyesha kuwa Mombasa inaendelea kuimarika kama kitovu cha biashara na uwekezaji. Katika nusu ya kwanza ya mwaka 2026, Bandari ya Mombasa ilihudumia tani milioni 22.3 za mizigo, huku tani 566,400 zikisafirishwa kwa reli. Aidha, zaidi ya wageni wa kimataifa 96,700 waliwasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mombasa katika miezi minne ya kwanza ya mwaka huo.
Kituo kipya cha Nyali kinaongeza uwepo wa huduma za Priority Banking za Standard Chartered nchini Kenya, huku benki hiyo ikilenga kupanua huduma zake kwa wateja wenye utajiri mkubwa nje ya Nairobi na kuwapa fursa za kifedha kutoka shirika la kimataifa
Kituo kipya cha huduma za uwekezaji Nyali kufaidi Pwani

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
BusinessAnthropic sets IPO price at $83 per share, targets $1.5trn valuation
–Claude maker raises $81.3bn in world’s largest IPO, overtakes SpaceX as investors rush for AI, despite $104bn lossBy Vera Anyagafu, with agency report The artificial intelligence race just produced the biggest stock market debut in history. Anthropic, the United States artificial intelligence company behind the Claude chatbot, on Wednesday priced its initial public offering at […]
BusinessOyedele urges banks to prioritise agricultural lending
…Commissions Moniepoint Abuja branch By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The Minister of Finance and Coordinating Minister of the Economy, Taiwo Oyedele, has urged banks and other financial institutions to make loans more affordable and accessible to businesses, particularly those operating in the agricultural sector, to stimulate productivity and economic growth. Oyedele made the call […]
BusinessNasarawa attracts $2.3bn investments in seven years — Abdullahi
Records 21 reforms, 11 PPP projects worth ₦93bn By John Alechenu ABUJA — Nasarawa State has attracted more than $2.3 billion in investments over the past seven years following reforms and institutional development aimed at making the state more competitive and investor-friendly. The Managing Director and Chief Executive Officer of the Nasarawa Investment and Development […]
BusinessObi pledges massive investment in education, healthcare
By Chimaobi Nwaiwu NNEWI — Presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, has pledged massive investment in education and healthcare, improved electricity supply and an end to kidnapping if elected president in 2027. Obi, who made the pledge on Friday during a visit to Onitsha, Anambra State, also said his proposed administration, […]