WITO umetolewa kwa mataifa mbalimbali kuingilia kati ili kuisaidia nchi ya Nepal baada ya idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko makubwa yaliyokumba maeneo ya milimani ikiwa zaidi ya 470 huku zaidi ya watu 1,000 wakiendelea kutafutwa.
Waokoaji wanaendelea kukagua mabonde na vijiji vilivyofunikwa na matope, mawe na vifusi baada ya mafuriko makubwa yaliyotokea Jumatano.
Janga hilo lilitokea baada ya sehemu ya barafu katika Milima ya Himalaya kuyeyuka na kusababisha mkondo mkubwa wa maji, matope na mawe kuingia kwenye mito ya milimani.
Awali kulikuwa na dhana kwamba tetemeko la ardhi ndilo lililosababisha maafa hayo, lakini uchunguzi wa baadaye ulionyesha kuwa kuyeyuka kwa barafu na miamba ndiko kulikosababisha mafuriko hayo.
Mafuriko hayo yameathiri vibaya eneo la Rasuwa na maeneo mengine kaskazini mwa Nepal, karibu na mpaka wa China.
Vijiji, barabara, madaraja na miundombinu mingine vimeharibiwa, hali inayofanya shughuli za uokoaji kuwa ngumu.
Taarifa za mamlaka ya utalii Nepal zinaonyesha kuwa watalii 667 hawajulikani waliko, wakiwemo raia wa nchi 31.
Takribani wageni 540 kati yao ni raia wa kigeni. India imeorodhesha raia wake 288 waliopotea, huku Amerika ikiwa na angalau 65, Malaysia 55, Ukraine 53, Uingereza 33, Australia 25 na Canada 25.
Mafuriko pia yameathiri upande wa Tibet unaodhibitiwa na China.
Katika jimbo la Gyirong, watu 558, wakiwemo raia 260 wa kigeni, wameripotiwa kupotea, huku China ikithibitisha vifo vitatu.
Serikali za Nepal na China zimepeleka helikopta na vikosi vya uokoaji katika maeneo yaliyoathirika.
Hata hivyo, barabara zilizokatika na mawasiliano kuvurugika vimeathiri juhudi za kuwafikia manusura.
Wakati huo huo, mamlaka zimeonya kuhusu hatari nyingine ya mafuriko baada ya maji kuziba sehemu ya Mto Bhotekoshi na kuunda ziwa linaloweza kuvunja kingo na kusababisha mafuriko zaidi.
Wakazi katika maeneo yaliyo hatarini wameonywa kuwa tayari kwa uokoaji.
Nepal hupokea mvua nyingi wakati wa msimu wa monsoon, lakini wataalamu wameonya kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanaongeza hatari ya kuyeyuka kwa barafu na kutokea kwa mafuriko makubwa.
Shughuli za uokoaji zinaendelea huku familia zikisubiri taarifa kuhusu ndugu zao waliopotea.
Idadi ya walioangamia nchini Nepal yafika 470

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
TravelMiss World Kufungua Milango ya Utalii
ZANZIBAR imeendelea kujitokeza kama moja ya vivutio muhimu vya utalii nchini, safari hii ikipokea ugeni wa Miss World 2026, Joheirry Molla aliyewasili visiwani humo Novemba 19, 2026, akiwa ameambatana na warembo kutoka mabara sita.
TravelAskari Tanapa, TFS mbaroni mauaji ya wabeba mkaa
KAGERA; Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia askari 13, wakiwemo wa wanyamapori wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), askari wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na askari mgambo, kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne yaliyotokea Kijiji cha Kanyamika, Kata ya Karambi, Tarafa ya Kimwani, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Taarifa…
TravelNgorongoro scoops continental gong
ACCRA: THE Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) has won the Excellence in Sustainable Tourism and Conservation Management Award at the Africa Business Forum & Awards 2026. The award recognises Ngorongoro’s contribution to biodiversity conservation, sustainable tourism development and the protection of its outstanding natural and cultural heritage. The awards ceremony was held in Accra, Ghana,…
TravelDk Kijaji: Mashindano makubwa gofu Afrika kufanyika Serengeti
MARA; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, amesema Uwanja wa Gofu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti utawezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya gofu ya Afrika na kimataifa, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii, mapato na kuitangaza nchi kupitia utalii wa michezo. Akizungumza leo Oktoba 18, 2026, wakati wa uzinduzi wa…