VideoUpcoming
HABARI ZA SAA, SAA MBILI NA DAKIKA 55 - NOVEMBA 23, 2026
Channel: ITV Tanzania Watch on YouTube
About this video
Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : bit.ly/itvtanzania Facebook : bit.ly/2KeQNl3 Twitter : bit.ly/2XG7aii Instagram : bit.ly/34KItmg
Related stories
NewsSababu za Ruto kuenda Congo ghafla usiku
RAIS William Ruto na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Félix Tshisekedi, wamepata fursa mpya ya kurekebisha uhusiano wa kidiplomasia uliodorora kati ya nchi zao kwa karibu miaka mitatu. Viongozi hao walikutana Jumapili katika mkutano wa viongozi wanne uliofanyika Oyo, Jamhuri ya Congo, pamoja na Rais wa nchi hiyo Denis Sassou-N’Guesso na kiongozi wa Togo Faure Gnassingbé. Mkutano huo ulilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, ushirikiano wa kikanda, usalama na maendeleo ya kiuchumi. Dkt Ruto aliwasili Oyo Jumamosi usiku, Novemba 21, 2026, akikatiza ziara yake ya siku nane eneo la Magharibi mwa Kenya. Katika ujumbe wake, Rais alisema viongozi hao walikuwa na nia ya kuimarisha ushirikiano na kutafuta suluhu ya changamoto zinazoikumba Afrika. “Majadiliano yetu yanalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kukuza ushirikiano wa kikanda, kuendeleza amani na usalama na kupanua ushirikiano kwa ajili ya ustawi wa pamoja wa mataifa yetu,” akasema Dkt Ruto. Kwa upande wake, Rais Tshisekedi alisema mkutano huo ni fursa muhimu ya kujenga upya imani kati ya viongozi wa Afrika na kutafuta suluhu ya kudumu kwa mzozo wa usalama mashariki mwa DRC. “Tunajitolea kuimarisha mazungumzo na imani kati ya viongozi wa Afrika na kufanya kazi pamoja kutafuta suluhu za kudumu kwa mzozo wa usalama mashariki mwa DRC. Amani na utulivu katika eneo la Maziwa Makuu zinahitaji kujitolea kwa pamoja na suluhu zinazoongozwa na Waafrika,” akasema. Uhusiano kati ya Nairobi na Kinshasa ulianza kuzorota Disemba 2023 baada ya kuzinduliwa kwa muungano wa Alliance Fleuve Congo (AFC), unaohusishwa na waasi wa M23, jijini Nairobi. Serikali ya DRC iliishutumu Kenya kwa kuruhusu watu wanaohusishwa na waasi kutumia ardhi yake kuendesha shughuli za kisiasa zinazolenga kuipindua serikali ya Rais Tshisekedi. Kenya ilikanusha madai hayo na kusisitiza kuwa haijihusishi na masuala ya ndani ya nchi jirani. Kinara wa Mawaziri Musalia Mudavadi alisema wakati huo kuwa Kenya ni taifa la kidemokrasia lina
NewsKenyan newspapers review, Nov 23: Why Ruto abruptly cut short Western tour for secretive Congo talks
Kenyan newspapers spotlight Ruto’s Congo mission, mounting debt, Sifuna’s US campaign outreach, county hiring concerns and a widening gender wealth gap.
NewsBayelsa boat mishap: Tinubu donates N250m to victims’ families, as Shettima visits survivors
By Johnbosco AgbakwuruABUJA — PRESIDENT Bola Tinubu has called for stricter enforcement of safety standards on Nigeria’s inland waterways following the tragic boat mishap in Bayelsa State, announcing a N250 million Federal Government donation to support the bereaved families.He also demanded a thorough investigation into the circumstances surrounding the accident, vowing that the Federal Government […]
NewsNatembeya: Babu hana imani kwamba Sifuna atashinda, ndio maana anapanga kuwania 2032
GAVANA wa Trans Nzoia George Natembeya sasa anadai kuwa Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino haamini kuwa Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna anaweza kushinda urais 2027 na hana nia ya kuunga azma yake. Bw Natembeya, ambaye ni mshirika wa karibu wa kisiasa wa Sifuna, anadai kuwa Bw Owino anajipanga kuwania urais 2032 badala ya kumuunga mkono seneta huyo katika azma yake ya kumng'oa Rais William Ruto mamlakani. Alidokeza kuwa Bw Owino ameahirisha azma yake ya urais hadi 2032 kwa sababu hataki kukabiliana na rais aliye mamlakani katika uchaguzi wa 2027. Bw Owino, ambaye anaongoza chama cha The Mwananchi Party (TMP), alitangaza Aprili kuwa atawania ugavana wa Nairobi kisha 2027 kwa muhula mmoja kabla ya kuwania urais. “Nitawania ugavana 2027 kwa muhula mmoja, kisha nitakuwa kwenye kinyang'anyiro cha urais mnamo 2032,” alisema mnamo Aprili 26. Akizungumza Jumapili, Bw Natembeya alitilia shaka kujitolea kwa Bw Owino kuunga azma ya Bw Sifuna. “Babu Owino yuko katika upinzani lakini hayuko Linda Mwananchi,” akasema Bw Natembeya. Alipoulizwa iwapo Bw Owino anaamini Bw Sifuna anaweza kushinda urais 2027, gavana huyo alisema hesabu za kisiasa za mbunge huyo ndizo zimemfanya kulenga uchaguzi wa 2032. “Kwa hesabu zake, sisi ni watu wenye akili. Hataki kukabiliana na Rais aliye mamlakani, ndiyo maana anasukuma azma yake hadi 2032,” akasema. Hata hivyo, Bw Natembeya alionyesha imani kuwa Bw Sifuna hatimaye ataingia Ikulu, akisema huenda akawa rais aliye mamlakani kufikia 2032 iwapo upinzani utamshinda Bw Ruto 2027. “Kwangu mimi, naamini kuwa kufikia 2032 tutakuwa na Sifuna kama rais aliye mamlakani kwa sababu Ruto atashindwa mnamo 2027. Kwa hiyo, hesabu zake hazina maana kwa sababu anakwepa kukabiliana na Ruto 2027 lakini atakutana na Sifuna 2032 katika mazingira hayo hayo,” akasema.