Mahakama ya Watoto imempata mhubiri tata Paul Mackenzie na hatia katika mashtaka sita ya kuwashambulia na kuwafanyia watoto ukatili.

Hata hivyo, washitakiwa wenzake 21 wameachiliwa huru dhidi ya mashtaka yote 17 yaliyokuwa yakiwakabili. Uamuzi huo ni wa kwanza wa kuwaachilia huru baadhi ya washitakiwa katika msururu wa kesi zinazotokana na mauaji ya halaiki ya Shakahola. Mackenzie anatumikia kifungo cha miaka 200 jela kwa mauaji ya watu msituni Shakahola.


HABARI ZAIDI KUFUATA..