Filamu ya kutangaza vivutio vya utalii vya nchini Tanzania ijulikanayo kama “Tantalizing Tanzania” inayomhusisha mwanamuziki wa India Shakti Mohan aliyepiga picha mjongeo katika hifadhi za Serengeti, Ngorongoro na Zanzibar imezinduliwa nchini India.
Filamu hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Swahili iliyopo Mumbai nchini India imezinduliwa rasmi na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga.
Uzinduzi huo uliofanyika usiku wa Desemba 13,2024 jijini Mumbai nchini India uliratibiwa na Kampuni inayohudumia watalii nchini India na Tanzania ya Swahili Safari kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini India .
“Mafanikio ya jitihada zetu yanaakisiwa katika takwimu za Barometer ya Utalii ya Umoja wa Mataifa, iliyochapishwa Januari 2024 inaonyesha kuwa, mwaka 2023, Tanzania ilikaribisha watalii milioni 1.8 waliovunja rekodi, ikiwa ni ongezeko kubwa la asilimia 24.3% ukilinganisha na mwaka 2022 sambamba na ongezeko la mapato yatokanayo na utalii takribani dola za Kimarekani bilioni 3.4, jambo linaloonyesha uthabiti na ukuaji wa sekta ya utalii nchini Tanzania” Mhe. Chana amefafanua.
Amesema kupitia filamu ya “Tantalizing Tanzania” inawakilisha maendeleo makubwa katika kuongeza ufahamu wa Tanzania kama kivutio cha utalii nchini India, na kwamba filamu hiyo itaongeza idadi ya watalii kutoka nchini India, jumla ya 44,438 mwaka 2023.
Mhe. Chana ametumia fursa hiyo kunadi vivutio vya utalii huku akisisitiza Tanzania imejaliwa kuwa na maliasili, vivutio vya kuvutia vya kiutamaduni, na fukwe za bahari za bara na Zanzibar zinazotoa fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya utalii ikiwa ni pamoja na kuendeleza huduma za malazi katika maeneo ya hifadhi na maeneo ya mijini, kuimarisha utalii wa fukwe kwa kuanzisha hoteli za fukwe na kupanua huduma za burudani na burudani.
Kwa upande wake Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amepongeza waandaaji wa Filamu hiyo kwa kuwa imeakisi uhalisia wa vivutio vilivyoko Tanzania Bara na Zanzibar na kusema kuwa huo ni mwendelezo wa mikakati ya kuvutia watalii nchini Tanzania.
Naye, Mkurugenzi wa Swahili Safaris India, Rajiv Jagat Desai, alisema kuwa filamu hiyo imelenga kuonyesha Tanzania kama nchi ya kipekee yenye Utalii wa wanyamapori katika Hifadhi za Taifa pamoja na fukwe na mwaka 2024 imefanikiwa kupeleka watalii 100 nchini Tanzania.
“Tumeamua kama tunataka kuitangaza Tanzania ni lazima kumtumia msanii kuja nchini tanzania ili avutie watalii wa India hivyo watu wa India wataijua vizuri zaidi Tanzania” amesisitiza.
Uzinduzi huo umehudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania, Balozi Dkt. Ramadhani Dau, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bw.Ephraim Mafuru,Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Ndugu Arif Abbas Manji, Mwakilishi kutoka Shirika la Ndege la ATCL, Wakurugenzi wa Kampuni ya Swahili Safari India na baadhi ya wananchi kutoka Mumbai India.
The post Filamu ya Tantalizing Tanzania yazinduliwa rasmi nchini India first appeared on Millard Ayo.
Filamu ya Tantalizing Tanzania yazinduliwa rasmi nchini India

This story was originally published by Milard Ayo.
Read the full story at Milard AyoRelated stories
TravelMiss World Kufungua Milango ya Utalii
ZANZIBAR imeendelea kujitokeza kama moja ya vivutio muhimu vya utalii nchini, safari hii ikipokea ugeni wa Miss World 2026, Joheirry Molla aliyewasili visiwani humo Novemba 19, 2026, akiwa ameambatana na warembo kutoka mabara sita.
TravelAskari Tanapa, TFS mbaroni mauaji ya wabeba mkaa
KAGERA; Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia askari 13, wakiwemo wa wanyamapori wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), askari wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na askari mgambo, kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne yaliyotokea Kijiji cha Kanyamika, Kata ya Karambi, Tarafa ya Kimwani, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Taarifa…
TravelNgorongoro scoops continental gong
ACCRA: THE Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) has won the Excellence in Sustainable Tourism and Conservation Management Award at the Africa Business Forum & Awards 2026. The award recognises Ngorongoro’s contribution to biodiversity conservation, sustainable tourism development and the protection of its outstanding natural and cultural heritage. The awards ceremony was held in Accra, Ghana,…
TravelDk Kijaji: Mashindano makubwa gofu Afrika kufanyika Serengeti
MARA; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, amesema Uwanja wa Gofu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti utawezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya gofu ya Afrika na kimataifa, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii, mapato na kuitangaza nchi kupitia utalii wa michezo. Akizungumza leo Oktoba 18, 2026, wakati wa uzinduzi wa…