ZANZIBAR: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameitaka Idara ya Uhamiaji kuendelea kuwa mstari wa mbele kuchochea na kukuza utalii nchini kwa kutoa huduma bora na nzuri kwa wageni wanaokuja nchini kwa shughuli mbalimbali.
Ameeleza hayo Januari 10, 2025 Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zanzibar wakati alipotembelea ujenzi wa Bandari ya Shumba Mjini ambapo awali ilikuwa bandari bubu iliyotumiwa wananchi wageni kwenda bandari ya Mombasa, Kenya
“Tuendelee kujipanga na kuhakikisha tunakuwa na huduma nzuri ya kuwapokea wageni ili wakija wakafanya utalii watachangia utalii lakini wakipata huduma nzuri, wao pia wanaenda kuwa wasemaji wetu wazuri huko wanakotoka”
Bashungwa amesisitiza kuwa Idara ya Uhamiaji ikitoa huduma nzuri kwa wageni na watalii wanaaoingia nchini, hali hiyo itaendelea kuitangaza nchini yetu kwa Mataifa wanapotoka.
Aidha, Bashungwa ametoa pongezi kwa Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kazi kubwa ya maendeleo anayoendelea kuifanya kwa kuifungua Zanzibar kiuchumi.
Kadhalika, Bashungwa ameeleza kukamilika kwa ujenzi wa Bandari ya Shumba Mjini itasaidia kukuza uchumi na kuwawezesha Wananchi na wageni kuingia na kutoka Zanzibar.
Awali, Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Hassan Ali Hassan ameeleza kabla ya kuanza ujenzi wa Bandari hiyo wananchi wa Kisiwa cha Pemba walitumia eneo hilo kwenda Mombasa Kenya bila utaratibu ambapo kukamilika kwa bandari hiyo itawezesha kusafiri kufuata sheria na taratibu.
The post BASHUNGWA AITAKA IDARA YA UHAMIAJI KUTOA HUDUMA NZURI WA WAGENI, KUCHOCHEA UTALII. appeared first on HabariLeo.
BASHUNGWA AITAKA IDARA YA UHAMIAJI KUTOA HUDUMA NZURI WA WAGENI, KUCHOCHEA UTALII.

This story was originally published by Habari Leo.
Read the full story at Habari LeoRelated stories
TravelMiss World Kufungua Milango ya Utalii
ZANZIBAR imeendelea kujitokeza kama moja ya vivutio muhimu vya utalii nchini, safari hii ikipokea ugeni wa Miss World 2026, Joheirry Molla aliyewasili visiwani humo Novemba 19, 2026, akiwa ameambatana na warembo kutoka mabara sita.
TravelAskari Tanapa, TFS mbaroni mauaji ya wabeba mkaa
KAGERA; Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia askari 13, wakiwemo wa wanyamapori wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), askari wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na askari mgambo, kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne yaliyotokea Kijiji cha Kanyamika, Kata ya Karambi, Tarafa ya Kimwani, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Taarifa…
TravelNgorongoro scoops continental gong
ACCRA: THE Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) has won the Excellence in Sustainable Tourism and Conservation Management Award at the Africa Business Forum & Awards 2026. The award recognises Ngorongoro’s contribution to biodiversity conservation, sustainable tourism development and the protection of its outstanding natural and cultural heritage. The awards ceremony was held in Accra, Ghana,…
TravelDk Kijaji: Mashindano makubwa gofu Afrika kufanyika Serengeti
MARA; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, amesema Uwanja wa Gofu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti utawezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya gofu ya Afrika na kimataifa, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii, mapato na kuitangaza nchi kupitia utalii wa michezo. Akizungumza leo Oktoba 18, 2026, wakati wa uzinduzi wa…