ANTHONY KITIMO NA KALUME KAZUNGU WADAU wa sekta ya utalii Pwani wameeleza wasiwasi kwamba wageni wanaotembelea maeneo hayo msimu huu wanabana hela za matumizi. Wakati msimu wa sikukuu unapoelekea kilele chake, idadi ya watalii wa ndani na nje ya nchi wameripotiwa kuongezeka Pwani huku hoteli nyingi zikirekodi hadi asilimia 90 ya wageni waliokodisha vyumba hotelini. […]