NA LUCAS BARASA MASHIRIKA 73 ya watetezi wa kuhifadhi mazingira yamewasilisha ombi katika Jopo la Kitaifa la kutatua mizozo ya Mazingira yakitaka kusitishwa kwa ujenzi wa barabara inayopitia katika Hifadhi ya Kitaifa ya Aberdare. Chini ya mwamvuli wa-The Conservation Alliance of Kenya (CAK), walitahadharisha kuwa barabara kuu inayopendekezwa ya Ndunyu Njeru – Ihithe itaathiri vibaya […]