NA WINNIE ATIENO GAVANA wa Tana River, Dhadho Godhana, amesema umoja wa magavana wa Pwani utasaidia kupiga jeki ustawishaji wa uchumi wa baharini. Chini ya muungano wa Jumuiya ya Kaunti za Pwani, Magavana hao wanatarajiwa kukongamana Kaunti ya Tana River mwezi Desemba kujadili jinsi eneo hilo litakavyofufua uchumi wake baada ya sekta ya utalii kudorora. […]